Eti maziwa yatachafuka!

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
3,018
1,147
Siku za hivi karibuni nimekumbana na kisa hiki. Rafiki yangu ananiambia mke wake hataki kushiriki nae kisa ananyonyesha. Hoja yake ya mke ni myth iliyoshamiri ndani ya jamii kwamba sperms huchafua maziwa na kudhoofisha mtoto!
Anahitaji msaada wa kitaalam, uzoefu na maoni ya wadau
 
Mwambie aachane na ujinga. Sperm zinaingia kwenye sehemu za siri za mwanamke (vagina na kama cervix iko wazi zaweza kufika kwenye uterus) wakati maziwa yanatengenezwa kwenye matiti. Kwa hiyo haziwezi hata siku moja kusafiri hadi kwenye matiti.

Ila kitu ambacho huweza kutokea ni suala la kuongezeka kwa hormone ya aina ya oxytocin wakati wa tendo la ndoa. Hormone hi huweza kusababisha maziwa kujaa sana kwenye matiti. Na kama mama hatanyonyesha mtoto hadi asubuhi, yanaweza kuanza kuharibika na kumsabishia mtoto kuchafuka tumbo. Ila tatizo dogo sana hilo (medically). Ngono inazuiliwa walau ndani ya siku 40 baada ya kujifungua kumruhusu mama viuongo vikae vizuri. Baada ya hapo ni kuchukua tahadhari dhidi ya mimba tu.
 
hakikisha kuna mpango madhubuti tu wa kuzuwia mama kupata ujauzito.

ningemshauri akapate vidonge vya uzazi wa mpango MAALUM kwa mama wanaonyonyesha.

hayo mengine ni hiyo myth tu uliyoisema
 
Siku za hivi karibuni nimekumbana na kisa hiki. Rafiki yangu ananiambia mke wake hataki kushiriki nae kisa ananyonyesha. Hoja yake ya mke ni myth iliyoshamiri ndani ya jamii kwamba sperms huchafua maziwa na kudhoofisha mtoto!
Anahitaji msaada wa kitaalam, uzoefu na maoni ya wadau

Huyo anatakiwa arudishwe shuleni
 
Kuna watu wengi sana wanaamini hiki kitu.

Huyo anatakiwa arudishwe shuleni

Mbona wapo wasomi wengi wanaamini hivyo. Mimi nilikuta na jamaa ambaye alikuwa University (married) lakini alikuwa bado anaamini kuwa hilo linatokea. Mbaya zaidi alikuwa kwenye medical related course. Shuke hawawezi kufundisha kila kitu ila watu wengi hatuna tabia ya kujitafutia maarifa zaidi hata pale ambapo tunakabiliwa na tatizo linalohitaji ufumbuzi ambao tunaweza kuupata kwa kujisomea.
 
sikuwahi kusikia hii kitu hapo kabla hadi miezi michache nyuma humu JF

watu walikuwa wakizungumzia kumbemenda mtoto ikabidi niombe definition!

kazi kweli kweli
 
Siku za hivi karibuni nimekumbana na kisa hiki. Rafiki yangu ananiambia mke wake hataki kushiriki nae kisa ananyonyesha. Hoja yake ya mke ni myth iliyoshamiri ndani ya jamii kwamba sperms huchafua maziwa na kudhoofisha mtoto!
Anahitaji msaada wa kitaalam, uzoefu na maoni ya wadau

en.. hamna kitu kama hicho... ila ajitahidi kufata uzazi wa mpango
 
sikuwahi kusikia hii kitu hapo kabla hadi miezi michache nyuma humu JF

watu walikuwa wakizungumzia kumbemenda mtoto ikabidi niombe definition!

kazi kweli kweli

Kweli teacher,

Kuelimika ni zaidi ya kusoma. Ila gharama zake ni kubwa mno. Lazima ukubali kutafuta maarifa kwa gharama yoyote. Na hayo maarifa huwezi kuyapata kwenye udaku ambapo wengi wetu tumewekeza.
 
mfumo mzima wa masuala ya uzazi katika jamii yetu umegubikwa na utamaduni usio misingi ya kisayansi.

zaidi ya hili, kuna la watu kukataza watu wajawazito kufanya tendo la ndoa hasa wakikaribia siku za kujifungua kwa kuogopa mtoto kuzaliwa na sijui ukoko (dont ask me what ukoko is)

lakini wacha waje wenye kukubaliana na hii hoja ili mjadala upate kunoga zaidi
 
Hahahahahah

Hilo lipo sana. Hata mimi kuna wakati nilijikuta nataka kuwa muhanga wa hizo imani.

Hapa ndio unapogundua kuwa ukombozi wa kweli (na hasa hasa kwa wanawake) utatokana na elimu na siyo kitu kingine. Kuna watu wana pesa nyingi lakini kwa kukosa elimu (maarifa) wanatabika na mahirizi/pete na uchafu mwingine wa akina Shekh Yahaya Hussein.

Pia kuna mambo mengine ya kijinga sana ya kuwafunga watoto kitovu kiunoni au dawa nyingine ili kukinga dhidi ya michango ambayo ki ukweli na utapiamlo (malnutrition).

Kweli safari bado ndefu
 
Hao watoa mada kwenye zile "Kitchen Party" zao wanalo jukumu la kutoa shule kuhusu hilo.

Hao nao ni vipifu na mbumbu wa kutupa. Mambo ya msingi kabisa yanatakiwa yatolewe na mfumo rasmi wa elimu. Tayari myths nyingi zinazohusiana na mambo ya uzazi wataalamu wanazijua. Wanatakiwa watoe elimu kwa umma kuondoa hizo fikra potofu.
 
Hahahahahah

Hilo lipo sana. Hata mimi kuna wakati nilijikuta nataka kuwa muhanga wa hizo imani.

Hapa ndio unapogundua kuwa ukombozi wa kweli (na hasa hasa kwa wanawake) utatokana na elimu na siyo kitu kingine. Kuna watu wana pesa nyingi lakini kwa kukosa elimu (maarifa) wanatabika na mahirizi/pete na uchafu mwingine wa akina Shekh Yahaya Hussein.

Pia kuna mambo mengine ya kijinga sana ya kuwafunga watoto kitovu kiunoni au dawa nyingine ili kukinga dhidi ya michango ambayo ki ukweli na utapiamlo (malnutrition).

Kweli safari bado ndefu

seriously!!

inabidi tuweke list ya hizi mila za uzazi wazi .....tupate kuelimishana huh!
 
hakikisha kuna mpango madhubuti tu wa kuzuwia mama kupata ujauzito.

ningemshauri akapate vidonge vya uzazi wa mpango MAALUM kwa mama wanaonyonyesha.

hayo mengine ni hiyo myth tu uliyoisema
thanks G, au pia watumie condom
 
seriously!!

inabidi tuweke list ya hizi mila za uzazi wazi .....tupate kuelimishana huh!

Nhhheeee

Mbona yapo mengi sana. Unakuta mtoto kafungwa vitu kila mahali hadi anakuwa kama ng'ombe wa mmsai.

Kazi bado kubwa sana.
 
Siku za hivi karibuni nimekumbana na kisa hiki. Rafiki yangu ananiambia mke wake hataki kushiriki nae kisa ananyonyesha. Hoja yake ya mke ni myth iliyoshamiri ndani ya jamii kwamba sperms huchafua maziwa na kudhoofisha mtoto!
Anahitaji msaada wa kitaalam, uzoefu na maoni ya wadau

Kinachoathiri mtoto ni mama au baba kula uroda nje ya ndoa.
 
Hao watoa mada kwenye zile "Kitchen Party" zao wanalo jukumu la kutoa shule kuhusu hilo.

Tatizo vigezo vinavyotumika kwenye kuteuliwa kutoa mada kwenye "vicheni" party ni uwezo wa mtoa mada kwenye kutamka matusi na kutaja viungo vya uzazi bila aibu lakini wengi wao hawana elimu ya kisayansi ya kuweza kuchanganua mambo kama hayo!
 
hata hilo la kuganda maziwa ati usiponyonyesha kwa muda mrefu ni upuuzi......mbona ya ngombe hayagandi??? natunakamua asubuh na jioni....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom