kwenu wanazuoni, wachambuzi, watafiti, watalaam wa JF na uongozi wa CHADEMA, asalaaaaaaaaaam Aleykum,
Bahati mbaya sijui namna ya kuijibu hii salaam. Ndefu sana ingawa inaelekea ya kiislam (lakini sivyo iandikwavyo).
Leo nataka mnieleze uhusiano kati ya chadema na Jamii forums baada ya kufanana, kuoana na kurandana katika mambo yafuatayo;
Sawa sheikh, ngoja nizipitie moja baada ya nyingine ili kuona ukweli wenyewe... Labda yaweza kuwa kweli!
(i) Rangi za ukuraza wa JAMII FORUMS zinafanana na rangi za BENDERA ya Chadema
Tuziangalie hizi bendera kwanza...
CCM:
CHADEMA:
NCCR Mageuzi:
CUF:
Zanzibar (bendera)
Sasa katika hoja yako najaribu kuangalia kwanini useme rangi ni za CHADEMA....
Rangi za Logo ya JF (ambayo ni ya muda hata hivyo na ndiyo inaweza kulinganishwa na rangi ya chama flani ama taifa flani...)
Ndani ya Logo yetu kuna rangi za Bendera ya Zanzibar, Bendera ya Tanzania, bendera ya CCM, bendera ya NCCR, CUF, CHADEMA etc.
Hoja kuwa CHADEMA na JF zina rangi sawa ni hoja ya kiuchochezi na sikubaliani nayo kwa kiwango kikubwa. CHADEMA rangi yao almost 30% ni RED na nyingine almost 30% ndiyo inaelekea kuwa karibia na ya JF nyeusi nasi tunayo na white ndiyo haikwepeki!
Naomba kuanzia leo onwards hii hoja ife na wenye mawazo ya kufananisha JF na CHADEMA kirangi basi wajue hiyo si hoja ya kusimamia.
(ii) Msimamo wa wana JF wengi na Chadema almost ni sawa.
Basi sema misimamo ya watanzanania (zaidi ya milioni 6) ambao wanaitembelea JF kwa mwezi ndiyo sawa na CHADEMA including YOU!
(iii) Baadhi ya washirika wakuu wa JF pia ni washirika na viongozi wa Chadema
Washirika wakuu sijaelewa unawalenga kina nani... Kama ni Zitto, Mnyika na Kitila basi unakuwa umechemsha kidogo mkuu... Yupo mtu 'mkubwa' zaidi ya Zitto humu na anatumia nick sawa na mimi na wewe. Tena ni mwanachama asiyekosa kila leo! Think of it,,, naye si kutoka CHADEMA bali CCM.
(iv) JF na CHADEMA wote kwa sasa wanadai wako kwenye vita dhidi ya ufisadi
Kama ni "kwa sasa" kwa maelezo yako basi unakuwa unakosea ndugu yangu... JF ni sehemu ya Jamii ya watanzania, basi watanzania wote ni wa kulaumiwa kuwachukia mafisadi.
(v) Walipua mabomu wa humu JF wanalipua na evidence (attachments) kama ilivyo kwa walipua mabomu wa Chadema (wazee wa nyaraka) ie Zito, Slaa, n.k
Hoja yoyote bila evidence ni uchochezi na ndo maana mara zote huwa tunataka ushahidi. Bila ushahidi unakuwa ni mdaku na mwongo mkubwa. Hili si suala la wewe uwe CHADEMA ama uwe CCM. Evidence ni muhimu popote. Haya si mabomu... Ni ukweli wa mambo!
(vi) Kwa kufuatilia majadiliano mbalimbali ya humu JF inaonyesha kuna uhusiano wa kisiasa, kifamilia na ule wa kupashana habari kati ya wana JF na CHADEMA...
Labda unasahau kuwa hiki ni chombo cha watu kupashana habari, kama na CHADEMA ndivyo walivyo basi si chama cha siasa tu bali cha kupashana habari. Au ulilenga kusemaje hapa mkuu? Huenda sijakusoma vema.
Kama kuna mtu nimemkwaza naomba aombe mungu amsamehe ila kwa sasa naomba kujifunza sihitaji kutukanwa wala kurushiwa maneno ya kejeri...
Hahaha, kusema huhitaji kutukanwa ama kurushiwa maneno ya kejeli unakuwa unasahau kuwa 'penye wengi pana mengi pia'. Pia kumbuka kuwa ukifanya jambo kwa kutarajiwa kupigiwa makofi, tarajia kuzomewa pia!
Ooops,,, mi nilidhani wewe maalim mkuu...? Sasa umeanza kama kiislam unaishia kikristo?
Ahansate na natumaini nimepunguza kiu yako.
haya mawili yanakuonyesha jinsi ulivyo,yaani unapenda kuchanganya mambo. Rangi zimeumbwa na mungu wala hazihusiani na chama chochote. wakati fulani Michael Jackson alifika hapa Bongo akiwa amevalia shati la kijani na surali nyeusi, alikuwa ni CCM?
Hahaha, well nadhani ulikuwa ni mtizamo wake. Kama hajaridhika na maelezo yangu na viambatanisho (ambavyo huenda akaona nimefanya ki-CHADEMA kwa kuweka attachments
🙂 ) basi anakaribishwa kutoa maelezo ya ziada.
Na hoja zinazotolewa nazo zina rangi?
Kuna KadaMpinzani, yeye rangi zake za maandishi siku za nyuma (naona nowadays kasahau) zilikuwa ni green tu. Kwa sababu hiyo tungesema JF ni sehemu ya CCM tu. Au tuondoe option ya kuandika kwa rangi ili kuepusha JF kufananishwa ama kuhusishwa na vyama flani.
Mkuu nyerererist, muige wa-jina wako. Kuna kitu zaidi nyuma ya ukuta ulio mbele yako. Think of it!