Eti JF ni CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti JF ni CHADEMA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Samvulachole, Aug 23, 2007.

 1. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2007
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Wengi wanaamini hilo

  Discuss
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  hapana,

  nadhani bado tunatawaliwa na ile kasumba ya kutokukubali kukosolewa. Miaka fulani nilipokuwa naishi Zbar ukitokea kupinga muenendo mbovu wa serikali unaulizwa "Ami weye CUF nini yakhe?",

  ...enzi zile ukipinga unaambiwa NCCR mageuzi, na sasa nguvu ya Upinzani imehamia CHADEMA huku bara, nasi tutaitwa CHADEMA, kisa madongo!

  Demokrasia kaaazi kweli kweli, jamaa wanatutega kama Bush,...

  "You are either with us, or against us!",...
   
 3. Bi. Senti 50

  Bi. Senti 50 JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 291
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Si udiscuss wewe mwenyewe. Mambo ya Imani peleka kwenye dini. Unaboa.

  thanks.
   
 4. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Saaaaafi sana. Unajua hata wanaotakakuusema upinzani sasa, kama ni Zanzibar watasema CUF, kama ni Bara watasema CHADEMA! Ni wazi hizi ndizo ngome kuu za upinzani sasa, na wanaotaka kubomoa upinzani wameelekeza nguvu zao huko...watu hawa wasio na aibu wala huruma na maisha ya wanyonge, wanataka kubomoa hata hicho kidogo kilichopo kinachowatia wananchi tumaini kwamba walau kuna mahali pa kupumulia kisiasa!
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mada kama alivyosema SAMVU, discuss nami sina budi kusema DISCUSS amigos..................
   
 6. T

  Tabasamu Senior Member

  #6
  Aug 23, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna thread moja Mwafrika wa Kike alikuuliza kuhusu hii tabia yako ya kusema sisi hivi, sisi vile. Mbona hatuoni hao wengine wakisema? Kwenye falsafa hiyo wanaita fallacy huwezi kusemea watu ambao hawajasema ni sawa na kusema kila mtu anajua hivyo. wewe ndiye unayeamini hivyo hivyo jisemee nafsi yako badala ya kuanza kusema wengi wanaamini hivyo.
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Samvulachole,

  Sidhani kama JF=CHADEMA. Hata kama kuna mtu alitaka iwe hivyo basi kakosea mahesabu maana JF iko huru mno kiasi kwamba haitakuwa rahisi kuwalazimisha wachangiaji kufuata mkondo mmoja.

  CCM wako madarakani kwahiyo wao wanapondwa mno na ni kawaida maana kama kuna makosa basi wao ndio wanafanya. Uongozi ukienda chama kingine basi mashambulizi mengi yatahamia huko.

  Muhimu tu ni kuendelea kujaribu kila jambo bila kuogopa.
   
 8. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #8
  Aug 23, 2007
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Lakini wale wanaodhani kuwa kila kitu kilichofanywa na serikali ya CCM kinapingwa JF basi anaangalia watu flani. Kuna watu wako imara sana kuitetea CCM hadi nakuwa insipired na michango yao.

  Unaweza kuwachukulia wengi kuwa wapinzani kwakuwa wana mwelekeo unaoshabihiana kiitikadi. Binafsi napenda sana kusoma michango ya mugongomugongo na huwa najifunza mengi toka kwake.

  Kuna watu kama Kulikoni na fikiraduni hawa pia wakiamua kuitetea CCM na wakatoa hoja inakuwa ni hoja kwelikweli. Tatizo wengi wa wanaoitetea CCM huwa hawajui kuwa wanapingana na ambao wametoka humo na huenda wanaijua CCM kuliko waijuavyo wao. Hapo ndipo patamu; mtu kama Kitila ambaye amewahi kugombea UVCCM anaijua CCM vema na akiwa anapingana na mpenzi tu wa CCM basi unajikuta unakata tamaa kwa majibu yanayoonekana kukumaliza nguvu na mapenzi yako kwa chama tawala.

  Afterall; mimi si CHADEMA, lakini nammiss mwenyekiti wangu Augustino Lyatonga Mrema. Bado naamini ana hoja nzuri japo hajapata upenyo. Kama kachemka basi ndio hivyo tena; ndiye chaguo langu kwenye politiki za Tz
   
 9. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #9
  Aug 23, 2007
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Shua; sifa hulewesha. Muhimu ni kuchukulia challenges za wanaokupinga kuweza kujiimarisha. Ndiyo maana watu wakirusha mawe sana FD hujibu kifupi kuwa tutaendelea kuongoza kwa kishindo. That implies something beyond the written words.

  Usiombee waingie hao CHADEMA madarakani; watakandamizwa maswali lukuki na lawama juu ya lawama hadi wapaone hapatoshi. Siasa ndivyo zilivyo, na waswahili walisema 'Mkubwa ni jaa' kila takataka hutupiwa yeye!
   
 10. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  teh teh...............mzee wa suti na raba !
   
 11. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka kauli kama hii iliwahi kutolewa na waheshimiwa: Harold Jaffu, Prince Bagenda, Thomas Ngawaiya, Enock Ngombale-Mwiru na wengine ambao sasa wanazunguma lugha tofauti. Waliowahi kumfahamu Mrema walimtema mapema mwaka 1995 baada ya mdahalo, kabla ya uchaguzi mkuu; waliochelewa kidogo walimtema mwaka 1996 alipoanza kampeni za chinichini kuwafukuza "wasomi" katika chama; waliochelewa zaidi walimtema mwaka 1999 alipohamia TLP siku chache kabla hajafukuzwa NCCR-Mageuzi.

  Waliochelewa mno (akiwamo Askofu Kakobe) ni wale waliotabiri kwamba Mrema ni chaguo la Mungu, wakasubiri matokeo ya uchaguzi wa 2000, baadaye wakashuhudia Mrema akijivalisha joho na kukabidhiwa "digrii" na mkewe Rose, pale Sinza katika nyumba inayosemekana kununuliwa kwa ruzuku ya chama na kuandikishwa kwa Rose Mrema. Miongoni mwao ni akina Ngawaiya! Hata hivyo, hao wameondoka, bado anao wengine, ambao kwa bahati nzuri na wewe umo. Unastahili pongezi. Endelea mkuu, ipo siku mtafanikiwa. Mchango wenu tunauona.
   
 12. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #12
  Aug 23, 2007
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Ah, unanikatisha tamaa sasa wewe. Utakuwa CHADEMA tu. Nasubiri bomu lake la Wizi wa Mkapa lilipuke na asipolilipua kufikia December mwaka huu nami namtupa mkono. Rushwa ile ya Milioni 900.
   
 13. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aha! wOrM, usikate tamaa hivyo! Zidi kupambana, msaidie mzee wako, ingawa zama zake zimepita. bado ana mchango katika jamii ya watz.

  Sasa mbona unataka kunivua uanachama wangu? Mie nilishatangaza hapa kwambia niko CUF, hasa yanapoguswa masuala ya Zenji. Sioni aibu kujitangaza, eti nisionekane nina upande. Mimi nina upande kwa sababu sipendi kuwa popo.

  CUF ni chama tawala kilichonyimwa fursa kwa mitutu kule Zenji. Huku Bara naona upepo umebadilika na kukipendelea CHADEMA, ndiyo maana CCM hawalali wanataka kuua mtoto ambaye bado anazaliwa. Hawana huruma kabisa, na baadhi yenu humu mnatumika bila kujua! You want to commit chamacide!
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  JAMBOFORUM = CHADEMA + [minority CCM] + ZANZIBARIAN=CUF] + NA[Non-Alaine]
  Assuming CCM+CUF is minimal or approaching to zero then. and NA is approaching to zero as well.

  Then
  JAMBOFORUM is approximaly/Equivalent to CHADEMA.

  Followup the proof above therefore you can deduce that

  JamboForum is Idara ya Uenezi ya CHADEMA complementing another daily newspaper... which is good very Innovative tactics of which ..CCM and CUF have never come tought of it...

  It is therefore believed that these guys are very innovative and hence the citizens can elect them to lead the country as they will come up similar innovations like these... including making sure the mines contracts are renewed annually to make sure the country benefit from these mine contracts due to dynamic changes of different conditions which of course will always be a challenge...

  It is with these facts, therefore I would like all of you to give them a big applause for their innovations

  HUREE JF, HUREEE CHADEMA
   
 15. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe nahaya unayamudu? Ulisoma na Lowassa au Mudhihir? (just kidding)
   
 16. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kichwamaji

  Unaniua mbavu mzee!!! unajua wananchi huru kama mimi yaani twaweza kuwakosoa wote kwa urahisi na kwa uhuru kamili jamaa walioko kwenye vyama hawawezi,,, sasa lazima tuifanye hio kazi..

  Unajua lisemwalo lipo, naombeni msipuuze haya tunayosema hata kidogo!!!!
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Aug 23, 2007
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Wanachama wa JF sasa mnaanza kutoa shutuma ama ni imani tu mlizo nazo zinapelekea kutoa suluhu za namna hii?

  Hata mugongomugongo sijawahi kusikia akitoa kauli za namna hii. Namtumia mugongomugongo kwakuwa yu wazi juu ya msimamo wake kisiasa na pale anapoona serikali inakwenda kombo hutoa mawazo ambayo huwa changamoto kubwa kwa forum. Kumbuka ndiye aliyetuletea "Great Stuff" na ndiye alianzisha "The Autonomyof Stupidity". Nampongeza kwani hajawahi kutoa conclusion ya "JF ni sawasawa na CHADEMA".

  Ninachoona kinaendelea hapa JF huwa ni watu wakizidiana lugha hufikia kutanguliza unazi wao kwa vyama vyao na kusahau utaifa. Nampongeza Kitila Mkumbo ambaye mara nyingi akiona wenzake ndani ya CHADEMA wanakwenda kombo basi hukosoa kiungwana na kuonesha wazi kuwa hajakubali hoja ya mmojawapo wa wanachama wenzake.

  JF as JF si ndugu na wala haina uhusiano kabisa na CHADEMA bali wanachama wake na wasomaji wake ni watanzania ambao wana mawazo na mitizamo tofauti. Ningeomba kukiri kuwa Moderators wanaweza kuwa wapenzi wa CHADEMA au CCM (japo sijawahi kuona mwelekeo huo) lakini JF as JF ikiwa na wapenzi wa CHAMA ama vyama flani basi ni rahisi wengi kudhani iko biased. Changamoto kwa wengine kama SAU, UMD, UDP, TLP, NCCR, NLD n.k ni kuwa na wasemaji wenye uwezo wa kujieleza kama wa vyama hivi viwili (CCM & CHADEMA) ili nao tuwasikie wana hoja zipi na hapo iwe rahisi kwa watanzania kung'amua nani mkweli na nani mwongo.

  Siku nikionesha unazi (au moderator yeyote) tafadhali tufahamishe ili tujirudi na kama tukionekana kuendeleza misimamo ya kuegemea upande mmoja basi fanya kutushauri kiungwana ili ikiwezekana tukubali kuwapa fursa wale ambao hawako biased waweze kuwa Moderators na nawahakikishia mimi sintotia neno bali kubakia kuwaachia Moderators wale ambao watanzania wamewakubali.

  Kuna wakati nafikiria sababu za vyama vingine kutokuwa na members huwa nakosa jibu; labda hawoni umuhimu wa kufanya hivyo au vyama vyao bado vichanga na vinahitaji volunteers ambao watajitolea kuwa wasemaji wao.

  Aidha, nawapongeza wote ambao huandika JF sehemu tofauti (si siasa tu) wakiwa wametanguliza maslahi ya taifa mbele. Ni uungwana sana kufanya hivyo na inapendeza pale tunapotoa mapendekezo kwa wale tunaowajadili (serikali ama taasisi na watu binafsi) juu ya nini kifanyike kuboresha kilichoharibika ama hata pongezi.

  Ni mawazo tu.

  Invisible
   
 18. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Unaungwa mkono! Only that unaweza ku-claim u-neutrality lakini usipoonekana ni tatizo... na adhari zake nadhani zinajulikana...

  kama wasemavyo... issue sio kutenda haki tu... bali ionekane pia kwamba haki imetendeka... hii ni pamoja na watu kupewa uhuru wa kutoa maoni... sio eti kwa sababu sio mazuri kwa chama fulani mtu yule ashambuliwe hapa ndio JF, wanaweza kujenda au kubomoa...

  Watch Out... tumesema kwa ajili ya kuwa na sustainable baraza.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Aug 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kilitime, mwalimu wako wa logic inabidi afikishwe mahakamani. Vinginevyo inabidi utueleze hii logic yako umeisoma chini ya mwalimu gani?

  unasema:
  That is fine, lakini unasema hivi:

  You can't assume CCM + CUF is minimal while you have already stated boldly, CHADEMA + [minority CCM]
  what is the basis of this assumption?
  Why would NA change directly proportionally to change in CCM+CUF unless NA is somehow tied to CCM + CUF?

  You are trying to say that if 5 = 2 + 1 + 2

  then 5 = (change in 2 + 1) will directly change (2)

  what you fail to say is that 5 can be equal to 1 + 1 + 1 + 1 + 1 or we can even break that into decimals and still get to 5!

  But this is what got me: the most absurd logical conclusion I have ever seen in my career!

  Now, when you speek JF una maana gani?

  Wale wanaochangia? Kama ni hawa, inakuwaje wawe wawakilishi wa Jamboforum nzima?

  Wale waliojiandikisha? Una uhakika gani waliojiandikisha (na hawachangii) ni wachache kuliko waliojiandikisha na wanachangia? Na unajuaje mitizamo yao ya kisiasa? Hivyo hata tukiwachukua hawa bado hatuwezi kuwafanya wawe wawakilishi wa JF

  Wale Wasiojiandikisha lakini wanaangalia kila kinachoendelea? Kama hawa nao ni sehemu ya JF unakabiliwa na tatizo la kundi hilo la pili pia.

  Hivyo, ili kuweza kusema JamboForums = something then we have to add all the three groups. If we do that, we are faced with the same problem. Tunajuaje kuwa kundi fulani ndilo lina watu wengi na jingine lina watu wachache? Hatuwezi.. UNLESS tunapojiandikisha tuweke option ya nani mwanachama wa chama gani na nani si mwanachama. Na tukifanya hivyo ni lazima tuondoe option ya wasio na chama kwani itasumbua hesabu zetu.

  In short, your deduction is simply and grossly flawed even to a novice! Next time, please get some help before you come up with these things.
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  haya basi wooote mnajua hesabu jamani tumekubali, wengine hazipandi ok shule mmeenda na inawasaidia ! mambo mengine vipi ?
   
Loading...