Hivi hizo zawadi lazima ziwe za kizungu ili watoto wa siku hizi watuone kwamba tu watu wa mahaba? Nikibeba pakiti ya miwa, ubuyu, korosho, karanga au matunda damu ya Lushoto nakuwa nimepotea maboya???
Wanaposema mahaba wana maana gani?
hahaha DC mbona unashtuka? Naamini kuwa zawadi hata hizo ni sawa. Muhimu iwe zawadi tu yoyote. Mimi niletee mishkaki ya kwa Muchacho tu baasii umenimaliza, chocolate kitu gani? Kwanza situmii :]]
Poa Teacher,
Ila kuna mtu kanambia kuwa nikileta mishikaki kibao kiasi kwamba watoto, dada, kaka na wageni wote home wakapata inakuwa siyo romantic...Is that true????
Haya mambo naona yanaleta kizungumkuti!!
Hicho sasa kitakuwa choyo. Nadhani cha muhimu ni kumkabidhi yeye tu sio unamwita msichana wa kazi, zawadi yenu hii au unaiweka kwenye meza! Huuuuh imehuuu???!!!
Hiyo definition ya mahaba naona kaa siyo hivi. Hiyo ni definition ya Mume anavyotakiwa kuwa kisheria....lol
Mahaba ni vile vi extra ambavyo huna wajibu wa kuvifanya kisheria, lakini vinafurahisha bibie.
Majuzi Ashadii kwa staili tofauti alileta mjadala wenye mwelekeo kama huu wa Mkuu DC,wengi humu walikubaliana naye ila mimi nilishindana nao kwa msingi kwamba waafrika traditionaly tuna namna zetu za kufanya malavidavi na si lazima tulambane.Haya mambo ya nyamnyam mmmmmhhh si wote tunayafagilia bana.
Majuzi Ashadii kwa staili tofauti alileta mjadala wenye mwelekeo kama huu wa Mkuu DC,wengi humu walikubaliana naye ila mimi nilishindana nao kwa msingi kwamba waafrika traditionaly tuna namna zetu za kufanya malavidavi na si lazima tulambane.Haya mambo ya nyamnyam mmmmmhhh si wote tunayafagilia bana.
DC hii mada kusema ukweli inategemea na mtu na mtu. Ninachokifahamu mie ni kuwa kitu kiitwacho Romantic kwetu tulio wengi ni kigeni kiasi kuwa hatuna definition ya pamoja ya nini maana yake. Mimi kama mimi mwanaume ambaye ni romantic (kwa maana yangu mie) ni yule anayejua nafasi yake kama mwanaume katika kunipa furaha, raha (simaanishi il eya kiuchumi sijui la hasha) namaanisha ile raha na hali ya kunifanya nijisikie mwanamke ninayependwa naye.... a woman of his choice. Mwanaume ambaye anakuwa in control katika kuhakikisha his lady ninaenjoy uwepo wake kwenye maisha yangu. Akiniletea au asiponiletea zawadi (nimesema zawadi si lazima iwe uwa) haijalishi (kwa ninavyomdefine romantic guy wangu) ili mradi nikiwa naye najisikia furaha. Mwanaume mwenye kijiutundu; si lazima anikumbatie au anikiss hadharani kunionyesha kuwa yuko romantic hata akiwa anakula paja la kuku, akacheza nalo kiaina pale mezani huku akinitizama kwa hali ya uchokozi kwangu ni romantic. Au tuko chumbani ajiimbishe imbishe hata ile Malaika nakupenda malaika na mjisauti wake wa chura mie I just cant explain the feeling!
Ila kuna mwingine bila kukumbatiwa mkono kiunoni wakatembea, kupewa uwa, dhahabu, kupelekwa sehemu za kushare their SRMs hajakuona romantic guy. Na vile vile sisemi kuwa mie kama mie nikipelekwa huko sipendi au nitakataa hapana ( Mbu unasikia, usijepata kisingizio hapa) kwangu mie ambaye najionaga wa kawaida sana na mwepesi wa kuridhika ukinipa retreat kubwa huwa ninajikuta naishiwa maneno kwa kweli zaidi ya kutabasamu na machozi kunitoka (nilisemaga nashindwa hata kuonyesha jinsi ninavyoappreciate) - Sijui kwa vile wa long mwe!!
Hii mada hii, mh we DC unalo unalolitafuta.
Najua wewe siyo mchoyo....Haya tutendee haki basi kwa kutupa definition ya upande wako!!
Mhhh sidhani kama kuna formula au vigezo katika kupima ukweli wa jambo hili ....
Ninachofahamu ni kuwa jambo hili ni complicated kuelezea na kuweka kwenye vipimo, ila ni suala ambalo Mpenzi au Mwanandoa anatakiwa kuwa mbunifu na kuhakikisha mwenzi wake anaridhika wakati na baada ya kufanya tendo hilo ....
Pia mahaba yanahusisha namna mtu anavyotakiwa kujiweka katika hali ambayo itamfurahisha bibiye kila wakati ikijumuisha hata kusaidia katika kazi ndogo ndogo, kuwa na kauli nzuri, kujaliana, kuthaminiana, kuheshimiana na kuwa na upendo wa dhati .....
Mimi kwangu nadhani uromantic unahusiana na vitu extra ambavyo viko tailored just for me. Tupo kwenye dunia ya customization sasa, mambo ya lamjaaliwaye hayakubaliki.
Cha msingi ni kujiskia najaliwa. Na nafikiri namna nzuri ya kuonyesha kujali ni maneno matamu, pamoja na kufanya vitu special pamoja. Take me out for food, remembering vitu muhimu kwenye schedule yangu hususan vya kazini. If I had an important presentation at work, napenda niwe treated kwa 'a good job well done'. Gimme a massage or don't ask me to cook a complicated food on that day huku ukisema leo tule simple since unajua nimechoka.
Nimekuelewa sasa Gai,
Nashukuru kwamba walau hiyo package yako ningeimudu...Naamini hata Boss ataridhia...Ila ngoja tusikie wenzine wana yapi!
Sasa amani inaanza kurudi kwani nilikuwa niki-imagine package yako, nahisi list inajaza behewa la treni ya Wahindi wa TRL!!
Babu DC!!
Hahaha natisha eee kumbe hamna kitu! kazi kweli kweli.......still it doesn't mean i wouldn't appreciate a three day vacation at Barbados :]
Nadhani wanawake ni viumbe rahisi sana kuwaridhisha, basi tu
Kwani na ww unategwa?hapo naelezea ukweli, kwa mfano eti kuna rafiki yangu kaachana na bf wake, kisa anaona shida anapoongea kiswahili wakati wa majambo, nikamshangaa sana, mie napenda full kiswahili,wasichana tunatofautiana
Pamoja kwamba hatupendi kuiga mamo ya wenzetu, ila mwaanaume akuonyeshe walau anakujali sana, anakupenda sana, na akwambie kabisa, akuhakikishie uko secure, sasa wanaume wengine wa kibongo anakupenda sana tu, ila hawezi hata kukuonyesha hayo mapenzi au kukwambia, yaani mnaenda kibubu bubu tu, kwa kweli hiyo inachosha, ni bora hata yule anayeiga na kukudanganya kitamthiliathilia, kwanza mapenzi bila kudanganyana kidogo wala hayanogi
But stil napenda sana mwanaume rijali wa kitanzania anayejua nini anafanya kuhakikisha nakuwa happy, na mie pia