Madikizela
JF-Expert Member
- Jul 4, 2009
- 675
- 437
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala ameendelea kukiponda chama hicho akisema ni cha wanafamilia wanaokitumia kujinufaisha.
Shitambala ambaye alikihama chama hicho, alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata ya Majengo jijini Mbeya.
MwanaCCM huyo alisema Chadema chama hicho hakitaweza kupiga hatua kutokana na kuwa sawa na genge la wachache ambaao ni wana familia wanaokitumia kujinufaisha.
Alisema CCM ndicho chama kinachoonekana kutokuwa na mwenyewe.
Alisema vingine vipo chini ya watu wachache hali ambayo vimekuwa vikipeana
madaraka wao wenyewe.
Tunataka chama kitakachokuwa cha Watanzania wote, ambao wakawa na kauli juu ya chama chao. Hatuhitaji chama kinachoongozwa na genge la wahuni.
Mtu kakianzisha kaweka hati nyumbani kwake, mwingine kaenda kaoa mke kwa mwenye chama kapewa uenyekiti.
Matokeo yake kinakuwa chama cha baba, mtoto na mkwe, hicho si chama, alisema na kuongeza: Mimi nilikuwa Mwenyekiti wao Mkoa wa Mbeya lakini nina historia ya kushindana nao katika suala la migomo.
Ndiyo maana sina historia chafu ya kukamatwa wala kufikishwa mahakamani kwa kuongoza migomo ama maandamano yasiyo na kibali. Hii yote ni kwakuwa napenda amani ndiyo
sababu sikukubali kufanya vurugu
SOURCE: Habari leo