Esther Bulaya (MB) Achemka Katika Interview EATV Chanel 5...!

Esther Bulaya (MB) Achemka Katika Interview EATV Chanel 5...!

Status
Not open for further replies.
Esther Bulaya wala siyo kiongozi kama anavyojitanabaisha. Tena anajitahidi sana kukaa karibu na Halima Mdee ili amsaidie mambo ya kiuanaharakati, lakini wapi! Hawezi kuwa mwanaharakati hata chembe.

We nawe! Kwa kuwa huyo wa kwako ndio mwanaharakati wa maana sana? Hamna kitu pale!!
 
kilichotokea ni typically wabongo kujifanya smart na busy wakati mtu huna lolote!! kujifanya mzungu wakati unatoka chankologo!! hata kuelewa swali tu shida!! bora ya zitto kasema akiacha siasa atatafuta university awe lecturer, wakati bi mdada atakuwa anasoma vitabu na kusikiliza hotuba ili aweze kukidhi mahitaji yake madogo madogo big up!!!
 
Huyo ndiye mwakilishi wa ''kundi maalumu'' la vijana wa CCM.Nani alaumiwe:muhusika mwenyewe kwa udhaifu wake au waliomchagua/kumteua?Mwakilishi mwingine wa vijana wa CCM anatoka Arusha.
Ukiwasikiliza hawa wawakilishi unashindwa kuelewa kama kweli wanafahamu uzito na umuhimu wa nafasi zao.
 
Mbunge wa viti maalum kupitia kundi la vijana toka chama cha mapinduzi akiwakilisha mkoa wa Mara wilaya ya Bunda alikuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha ''hot mix'' kinachorushwa kupitia kituo cha television cha EATV - Chanel 5!

Akaulizwa swali kuwa nje ya siasa anapenda kufanya shughuli gani?mojawapo ya shughuli aliyoitaja kwamba huifanya ni pamoja na kusoma vitabu na kusikiliza hotuba za wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Mwalimu Nyerere na Mandela!
Katika kukoleza maelezo yake akasema anapenda sana kusoma kitabu kinachoitwa ''How to be a Good Political Leader''. Mtangazaji akamuuliza jina la Author wa hicho kitabu lakini mheshimiwa mbunge akashindwa kumtaja kwakuwa alikuwa hamkumbuki pamoja na kuomba apewe muda ili amkumbuke!!

MY TAKE:
Kwa mtazamo wangu si rahisi mtu kusahau jina la author wa kitabu unachokipenda kukisoma mara kwa mara! Pengine Mh.Esther alikuwa anatafuta mileage kwamba ni msomaji mzuri wa vitabu lakini kachemka kwa kutomjua author wa kitabu akipendacho!

Mkuu Mwita Maranya, huyu ni mbunge wa CCM tena wa viti maalumu (kapewa ulaji ili alale bungeni) aliyependekezwa na Wassira ili apate ulaji kwa sababu tu anatoka mkoa wa Mara. In short, hana jipya na ikumbukwe pia kuwa wabunge ama viongozi tu wa CCM hawana issue zaidi ya ubabaishaji na ndiyo maana hawapendagi changamoto ama maswali ya papo hapo kwani wanakuwaga hawajuwi wajibu nini. Yaani mtu apendelee kusoma gazeti la uhuru section ya barua ya mhariri kisha asijuwe huyo mhariri ni nani, inakuja kichwani hii? Hawa watu wa CCM bwana!
 
80% ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo kama Ester, tofauti yao hawasagwi Mashine zao!
 
Mbunge wa viti maalum kupitia kundi la vijana toka chama cha mapinduzi akiwakilisha mkoa wa Mara wilaya ya Bunda alikuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha ''hot mix'' kinachorushwa kupitia kituo cha television cha EATV - Chanel 5!

Akaulizwa swali kuwa nje ya siasa anapenda kufanya shughuli gani?mojawapo ya shughuli aliyoitaja kwamba huifanya ni pamoja na kusoma vitabu na kusikiliza hotuba za wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Mwalimu Nyerere na Mandela!
Katika kukoleza maelezo yake akasema anapenda sana kusoma kitabu kinachoitwa ''How to be a Good Political Leader''. Mtangazaji akamuuliza jina la Author wa hicho kitabu lakini mheshimiwa mbunge akashindwa kumtaja kwakuwa alikuwa hamkumbuki pamoja na kuomba apewe muda ili amkumbuke!!

MY TAKE:
Kwa mtazamo wangu si rahisi mtu kusahau jina la author wa kitabu unachokipenda kukisoma mara kwa mara! Pengine Mh.Esther alikuwa anatafuta mileage kwamba ni msomaji mzuri wa vitabu lakini kachemka kwa kutomjua author wa kitabu akipendacho!

Ni sawa na mtu akurupuke kuitaja Movie bora kwake ni Olympus has Fallen...
Then akiulizwa Star nani?...kisha aanze kuuma uma kucha na kushindwa kumtaja Gerrald Buttler...

Shenz type kwa wakurupukaji woote.
 
Yani ili mradi na yeye aonekane yupo kwenye kundi la wapenda kusoma vitabu.
Sifa nyingine hizi!!
 
Mtangazaji naye alibofoa kwa kusema esta bulaya ni mbunge wa chama tawala cha upinzani ccm hahah nilicheka sana
 
Katika nadhaharia mbalimbali za ujibuji maswali, unatakiwa ulisikilize swali kwa makini, jipe muda na jiridhishe kama umelielewa. Mara nyingi watu/wanasiasa/viongozi na waombaji wa kazi wanakurupuka kujibu maswali. Sikuisikiliza hiyo interview, lkn kama hilo ndo jibu alilolitoa huyo dada, mmmhhh kazi ipo. Kusoma kitabu si kazi aliyoikusudia hasa muuliza swali. Nafikiri mbunge ameonesha hobi yake swala ambalo hakuulizwa. Inawezekana pia hana kazi zaidi ya huo uwakilishi!!!

Baadaye!
 
uyu dada anajilazimisha sana kuonekana ni bora, lakini kiukweli bado sana

Hana upiganaji wowote mnafiki tu.Lini kusoma vitabu ikawa kazi? Je angeulizwa interest zake ni nini?angesema anapendelea kuoga sehemu za wazi?
 
Huyu Esther Bulaya hana uwezo wa kujieleza hata huko bungeni kaingia kwa mbeleko tu.

Siamini kama ni Ritz uliyeandika maneno haya. Au ulitoka nje bila kuzima tarakilishi? Kama umekuwa mkweli kiasi hiki hongera.
 
Last edited by a moderator:
Mie nimeshangaa jibu lake. Maana kaulizwa nje ya siasa hupenda kufanya kazi gani? Eti anasikiza hotuba za Martin Luther King jr, Nyerere na Mandela. Hivi kusikiliza ni kazi? Au mie ndio mshamba! Yaani kuna watu ambao kazi zao ni kusikiliza hotuba tu?
Nilitegemea aseme labda anafundisha, au analima anafanya biashara au hata anaandika vitabu n.k na si kusikiliza tu kama kazi yake zaidi ya siasa.
Wewe ndo mshamba! hotuba za wanaharakati zimechangia sana katika kuwapa watu hamasa. vijana wengi hata leo wanasikiliza hotuba za viongozi wa zamani, wanafalsafa, wanaharakati na watu hupata elimu kwa kusikiliza kama vile kusoma! Nakushauri utafute muda uwe unzisikiliza kwa makini hotuba za hayati baba wa taifa (ziko nyigi mitaani kwa bei ya tzs 2,000 tu). Utajifunza mengi kwa kusikiliza pia!
 
lakin adrian nimemfutilia vipind vyake vingi kiukwel yuko vizur katika swala la kuuliza maswal kwa wagen wake studio na huwa hajali we ni kiongoz au msanii.. anafanya kile kilichokupelekaa studio wakat watangazaj wengne ni tatzo akiona kiongoz ni ful kujichekesha tu.
 
Wewe ndo mshamba! hotuba za wanaharakati zimechangia sana katika kuwapa watu hamasa. vijana wengi hata leo wanasikiliza hotuba za viongozi wa zamani, wanafalsafa, wanaharakati na watu hupata elimu kwa kusikiliza kama vile kusoma! Nakushauri utafute muda uwe unzisikiliza kwa makini hotuba za hayati baba wa taifa (ziko nyigi mitaani kwa bei ya tzs 2,000 tu). Utajifunza mengi kwa kusikiliza pia!

hujumuelewa mkuu umekurupuka. kamaanisha kitu kingne nje ya siasa, mandela na nyerere bado ni wanasiasa.
 
Esther Bulaya poa tuu. Tunajua na wewe unajua kuwa uwezo wako ni mdogo sana kama upo. Lakini wewe gangamala tuu mwanangu - si unajua mbeleko ziko nyingi ? Tutakubeba tuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom