Ester Bulaya aitosa CCM, asema hawezi kuhonga

Ester Bulaya aitosa CCM, asema hawezi kuhonga

Muda huu ninapoandika haya madiwani wote wa jimbo la Monduli waliokuwa wa CCM wamerudisha kadi na kujiunga na CHADEMA...

Sio hao tu bali hata wenyeviti wa vijiji na vitongoji wote wa CCM wamerudisha kadi na kujiunga chadema.









https://m.youtube.com/watch?v=2Pqi7EKVEPM

kurudisha form sio tatzo hata mlema aliwahi kufanya hvyo..

Na ujiulize kama wanaipenda chadema hawakurudisha miaka yote? Badala yake wanarudisha baada ya Kaka yako Lowasa kukatwaa?

Tutaona mengi huu mwaka na mshindi anabaki kuwa yuleyule
 
Watabaki wangapi sasa huko ccm kwa mwendo huu? Mbaya zaidi wanaoondoka woote ni wanasiasa wenye mvuto na wawajibikaji kwa wananchi
 
Alichokisema Bulaya ni kuwa "Nitagombea Jimbo la Bunda Mjini lakini sitogombea kwa tiketi ya CCM, sina ugomvi na CCM wamenilea na nimekulia huko, na kutogombea kwangu kupitia CCM kusihusishwe na mtu na nafasi ya Urais".

Ameongeza kuwa "Ila nimelitumikia Taifa langu nikiwa CCM naona nitalitumikia Vizuri zaidi nikiwa kwingine. Kumbukeni chama ni njia ya kupita ila umuhimu wa kulijenga Taifa letu ni la watanzania wote bila kujali vyama vyetu. Mungu ibariki Tanzania"
 
Huyu, yule wa Mwibara, Deo, Lembeli, waondoke tu CCM maana si mahali pao, wasipoangalia hata kupitishwa wasingepitishwa

Huyu wa mwibara sasahivi anatafuta pa kukimbilia. Sidhani kama bado anawazo la kubaki CCM baada ya mtu wake KUKATWA
 
I think CCM is doomed..kama siyo 2015 basi 2020.... Mafuriko haya yanaweza tokea au ni dalili tu... In short watu wameamka sana, CCM wanatakiwa wabadilike otherwise ule usemi wa "JK ni nabii aliyekuja kuiangusha Dola ya CCM utatimia"
 
Easter Bulaya, ni mtu wangu wa karibu. Ila mimi sina hizi habari. Nina mashaka na hizi taarifa.

Mandla.

Huo ukaribu ni Kilomita ngapi toka ulipo?? Analazimika kukutaarifu kila jambo??
 
Huyu dada anafaaa kuvaa magwanda ya CDM, hata bungeni huwa ni shujaa wa kweli. Vua gamba vaa magwanda ya wapambanaji. Karibu CDM dada
 
Kila la heri mdada, ila chama atakachoingia wawe makini na watu wa namna hii, isije kuwa ni mapandikizi type ya kina John MAGALE SHIBUDA. Na mwisho wa siku wanakuwa wasumbufu nk.
 
Huyo dada namkubali sana. Hivi karibuni alinifurahisha kwa kuhoji kuhusu UCHAGUZI MKUU KUPANGWA SIKU YA JUMAPILI amhayo Wakristo wengi wanakuwa katika ibada. Hakujali mbinu ya ccm ya kulazimisha siku hiyo ili kufanikisha giri la mkono! Rafu huwa zinachezwa kwenye majina ya watu wasiojitokeza kupiga kura kwa kumjali Mungu zaidi ya chochote kile. Karibu sanaaa, toka kwa mafisadi na wala rushwa.
 
Karibu dada utubu dhambi zako utasamehewa tusonge mbele kukomboa taifa dhidi ya adui gamba...
 
Nadhani Esther hana damu ya CCM na akiendelea kuwa huko ataendelea kuteseka sana nafsi. Tafuta kule ambako unahisi utaitendea haki nafsi yako na kuwa mtumishi mtukuka
 
Hivi kwa akili ya Ester anaamini wajita wazizaki wakyaya wachague mbunge mwanamke?
 
Rushwa imekithiri CCM.Ndo maana mpaka serikalini haya maradhi rushwa na ufisadi yamekuwa sugu.
 
Huyu, yule wa Mwibara, Deo, Lembeli, waondoke tu CCM maana si mahali pao, wasipoangalia hata kupitishwa wasingepitishwa

CCM tunapenda uongo wao wanajidai kusema ukweli..CCM sisi tunataka kulitafuna taiga wao wanajifanya wafaia nchi waende huko CHADEMA kwa wafia nchi wenzao,sisi CCM tunajali matumbo yetu na watoto wetu!!
 
Njoo huku kwetu CDM ufunguke vizuri maana huko kwenye mboga mboga ulikuwa umejibana kweli
 
Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga.

Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.

Chanzo: Nipashe

=====================
Update



Hiki ndicho nilichokuwa nakisubiria kutoka kwa bulaya....
Nilijua kitu kama hiki kingetokea kwa Ester bulaya!
As if I knew it!🙂🙂🙂
 

Attachments

  • 1437381080208.jpg
    1437381080208.jpg
    48.1 KB · Views: 172
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom