Ester Bulaya hakuwa na mpango wa kuhama CCM ila...

Ester Bulaya hakuwa na mpango wa kuhama CCM ila...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
SIASA

.

Najua nina watu wangu wanaopenda stori za siasa sasa stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia CCM Ester Bulaya pamoja anaonekana kwenye headlines mpya za Chadema baada ya kuhamia chama hicho anasema hakutegemea kuhama chama cha Mapinduzi (CCM).

.

‘Kuhama inatokea na mazingira lakini mimi sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuhamia Chadema lakini mienendo, tabia, future ya kuwatumikia wananchi ilikuwa imepotea mimi nimekulia CCM na am proud for that wamenilea lakini walinilea kwenye misingi ya uwazi na ukweli kile walichonifunza nikitaka kukitumia hawataki sasa kama kuna wengine kile nilichofundishwa huku wao wanakiaminia kutoka moyoni na midomo mwao niende kujiunga nao lakini wote tukiwa na ndoto za kuwatumikia wananchi' -Ester Bulaya

.

‘Unajua kuna tofauti ya utumishi na mtu kufikiri utumishi ni cheo wanaofikiri ubunge ni cheo ni wale ambao hawatimizi wajibu wao wanataka ubunge kutaka madaraka Fulani, mimi ni mtumishi naenda kuwatumikia wananchi mabosi wangu ni wananchi ukiwa unadhani ya kwamba ubunge ni cheo utavimba kichwa na utashindwa kutimiza wajibu wako, bunge bosi wake ni wananchi‘ – Ester Bulaya.​

Chanzo: MillardAyo
 
Hayo maneno ya mwisho yana maana sana.Wengi wanafikiri ubunge ni cheo na hivyo huishia kujiwezesha wao wenyewe na familia zao.
 
Hayo Maneno Kuntu Kutoka Mwanadada Ambaye Ni Mwaminifu Katika Utumishi, Kwani Ni Ukweli Usiopingika Kwa CCM Kuhubiri Wasichotenda, Ukidumu Nao Hautaweza Kuwatumikia Wananchi.
 
Huyu Dada emechelewa kweli kuijua kweli, na sasa ameijua kweli basi hiyo kweli utamuweka huru,
 
Haya aone huko aliko kama atakuwa na uhuru wa mawazo kinyume na Mbowe tu let a lot mtazamo wa chama kama alivyokuwa mjeuri akiwa CCM na kama ata achiwa na akina nanilii wa JF (siku akijaribu ataitwa majina yote wazazi wasiopenda watoto wao kuyatamka).

Dr.Slaa tu sasa hivi wanamtukana kwa kusimamia principles za jitihada zao itakuwa yeye ndio keshakuwa msukule tena asahau tu kuhusu neno freedom of speech and free will.
 
Huyu Dada emechelewa kweli kuijua kweli, na sasa ameijua kweli basi hiyo kweli utamuweka huru,

Ngoja Na Mimi Nichungulie Makabrasha Yake Ya Maovu a.k.a Kashfa Niliyonayo Ili Ikiwezekana Jamii Nayo Ijue Upande Wa Pili Wa Shilingi.
 
Haya aone huko aliko kama atakuwa na uhuru wa mawazo kinyume na Mbowe tu let a lot mtazamo wa chama kama alivyokuwa mjeuri akiwa CCM na kama ata achiwa na akina nanilii wa JF (siku akijaribu ataitwa majina yote wazazi wasiopenda watoto wao kuyatamka).

Dr.Slaa tu sasa hivi wanamtukana kwa kusimamia principles za jitihada zao itakuwa yeye ndio keshakuwa msukule tena asahau tu kuhusu neno freedom of speech and free will.
Ndugu,
Mtoto akililia wembe hupewa...!

Ninachofahamu kilichomfanya kuondoka CCM sio hiki anachotaka kuwaaminisha wananchi.

Ukweli hupanda ngazi na ninatumaini sio siku nyingi ukweli utawafikia walengwa.

Tuvute subira!
 
Kwa gharama ya nani hiyo subira ivutwe??!!!
 
Kapi jike hilo na lina oili chafu.
Uchanga wa kisiasa umeshamgharimu.
Anajifikiria she's bigger than politics, nobody will miss her.
Aendage!!
 
Huyu Dada emechelewa kweli kuijua kweli, na sasa ameijua kweli basi hiyo kweli utamuweka huru,

Huyu dada ni kweli alikwa na mtazamo huu chanya tangia awali, tumemshuhudia BUNGENI akiwa mwiba mkali kwa CCM. Huyu dada pamoja na Deo Filikunjombe, walifikiri CCM ingeweza kubadilika ikafanana na misingi yake waliyokuwa wakiiamini wao. Natumaini ya kuwa kwasasa Ester Bulaya atakuwa na uhuru zaidi wa kuwatumikia wananchi katika misingi ya haki na ukweli halisi. Binafsi namuunga mkono kwa kuhamia CHADEMA, na bado namsihi mh. Deo Filikunjombe ya kuwa atabaki mwenyewe kwenye hilo kundi la ndege wasio fanana na yeye.
 
Wasira kazi anayo,na huko kwenye kamati ya ushindi ya ccm alikowekwa hataweza kufurukuta make hata kura za maoni kapita kwa mbinde,kwa jembe ester bulaya mjengoni atapasikia redioni:A S 103:
 
hata lowasa hakuwa na mpango wa kutoka ccm. bali dhuluma zikamkimbiza...
 
Huyu mwanamke wangempa viti maalum toka lini wajita na wakurya wa Bunda wakaongozwa na mwanamke.
 
Back
Top Bottom