Ester Bulaya aitosa CCM, asema hawezi kuhonga

Hizi taarifa zinachanganya ni bora aseme mwenyewe inaonesha waandishi wetu wanapo hoji mtu huwa na majibu yao
 
Easter Bulaya, ni mtu wangu wa karibu. Ila mimi sina hizi habari. Nina mashaka na hizi taarifa.

Mandla.
Inafurahisha mtu wako wa karibu kakuacha huna taarifa wakati wengine wanazo,nadhani hata aliyempa kadi ya chama hana taarifa hivyo pokea taarifa kama ilivyo na usiapate ukakasi.
 
ndani ya ccm , rushwa ni sehemu ya nyaraka za kuambatanisha ndani ya fomu za kuomba uteuzi .
 
Mbona alichosema hakiendani na kichwa cha habari? Nani m kweli? Bado hajasema sababu . Aende salama CCM ni ile ile.

=====================
Update

[/SIZE][/QUOTE]
 
Sijui kama ni kweli CCM wanakaribisha rushwa chamani na itakuwa vigumu kwangu kuamini.Huko Moshi mjini kuna kijana mmoja wa Makamu anafaa kabisa kupeperusha bendera ya CCM lakini nilipomuuliza kuhusu hilo alinijibu taaluma yake inawasaidia wananchi wote bila kujali itikadi zao ikiwemo ya kichama,aliendelea kusema endapo ataingia kwenye siasa kwanza atakuwa muwongo kitu ambacho Mwenyezimungu anakichukia saana na itafika mahala itabidi atoe pesa kwa wananchi kitu ambacho atashindwa ku ACCOUNT for kwenye mizani za haki.To me he is a good candidate kwenye uwaziri unaohitaji taaluma.ni PM ni kudokeze ni nani.
 
GAZETI LA MWANANCHI

Dar/mikoani. Baada ya mchakato wa kuwania urais, sasa vita ya Uchaguzi Mkuu imehamia kwenye ubunge na udiwani hasa kutoka katika vyama vikubwa vya CCM kinachotawala na Chadema kinachoongoza upinzani.

Hadi jana, ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho kwa vyama hivyo kuchukua na kurejesha fomu, jambo moja lilijidhihirisha katika baadhi ya majimbo kwa upande wa CCM; baadhi ya majina makubwa katika siasa za ubunge yanachuana hivyo kufanya mchakato wa kumpata mteule mmoja kuwa mgumu.

Wasira, Bulaya wavaana

Mchuano mwingine mkali unatarajiwa kuwapo katika Jimbo la Bunda Mjini ambako Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira atavaana na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya.

Wabunge hao wa CCM wamekuwa wakitambiana muda mrefu na wakati mwingine waliwahi kurushiana maneno hadi bungeni, lakini mwisho wa tambo zote ni kwenye kura za maoni.

NIPASHE

[h=2]Bulaya aitosa CCM.[/h]

NA WAANDISHI WETU

20th July 2015

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

headline_bullet.jpg
Afuata nyayo za Lembeli, M/kti Halmashauri Monduli abariki madiwani kujitoa.

Bulaya-20July2015.jpg

Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya.

Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Bulaya ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na NIPASHE baada ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa rasmi nchini jana.

Tangu mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

Bulaya amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge kupitia CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama.

Hata hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na kutimiza azma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ingawa Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwa kusubiri makada kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (Cuf).

M/KITI MONDULI APIGILIA MSUMARI
Wakati ikiwa hivyo kwa Bulaya, hali bado si shwari ndani ya CCM Wilaya ya Monduli baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Edward Sapunyo, Kupigilia msumari wa mwisho na kubariki hatua ya madiwani wake 20 kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza mjini hapa jana, Sapunyo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Moita, alisema madiwani wake hawawezi kusubiri hadi Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atoe kauli kuhusu hatma yake ya kisiasa ndani ya CCM.

Kauli ya Sapunyo ambaye hatagombea udiwani uchaguzi wa mwaka huu, imekuja siku moja baada ya madiwani 20 wa jimbo hilo kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Hatuwezi kuona baba yetu anapigwa na kuanguka chini halafu tusubiri kauli yake, ni lazima tuchukue hatua mara moja…hii haivumiliki, kitendo alichofanyiwa (Lowassa) na vikao vya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kwa kukata jina lake pasipo kumpa haki ya kumsikiliza siyo cha kidemokrasia,” alisema.

Lowassa na makada wenzake wa CCM 38 walichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Katika kinyanyang’anyiro hicho, jina la Lowassa na wenzake yalikatwa katika hatua ya mwanzo, hali ambayo imezua malalamiko kwamba ikidaiwa kuwa hawakupewa
nafasi ya kuhojiwa.

“Tumepigwa, tumesambaratika (CCM) Monduli, hatuwezi kuchukua fomu za kuomba kugombea au kutetea nafasi zetu ndani ya chama hiki, tumehamia Chadema,” alisema.

Akizungumzia hali ilivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alidai kuwa siyo kweli kwamba madiwani wote wamekihama chama chao.

Kimaro alidai kuwa baadhi ya madiwani waliotangaza kukihama chama hicho wameanza kusalitiana.

Alisema madiwani hao ambao anawaita ni makada baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Monduli kuvunjwa, walifanya mkutano kwa kushawishiwa na mmoja wao.

Alisema ushawishi huo unatokana na uchu wa madaraka alionao kwa kuwa tayari wananchi wa Jimbo la Monduli, wanapenda aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Namelok Sokoine, kuchukua fomu za ubunge wa jimbo hilo.

Alisema kutokana na ugumu huo, diwani huyo wa zamani ametumia mbinu ya kuwarubuni wenzake wakihame chama hicho ili agombea ubunge kwa tiketi ya Chadema.

“Huo ni uchu wa madaraka aliyo nayo,” alisema na kuongeza: “Diwani huyo hakubaliki na wananchi wa kata yake."

Alidai kabla ya kutangaza kukihakama chama hicho, madiwani hao walikuwa wameshafanya kikao na kuweka azimio la pamoja la kuondoka CCM, lakini juzi walipotangaza uamuzi wao, walijikuta wapo madiwani watatu.

Alisema baadhi ya madiwani walimfuata ofisini kwa lengo la kumuomba radhi lakini yeye aliwaambia waende kuwaomba radhi wananchi katika kata zao.

“Madiwani wachache walikuja hapa ofisini kuomba radhi kwa Katibu wa CCM Wilaya, nikawaambia waende kuwaomba radhi wananchi,” alisema.

Akimzungumzia Lowassa, alisema anachoelewa ni kwamba hajatoa tamko lolote kama anakihama chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na mitandao ya kijamii.

“Bado tuna imani na Lowassa kuwa ni CCM, mpaka sasa hajatoa tamko lolote kukihama chama, lakini ikiwa vinginevyo itakuwa hatari kubwa,” alisema.

Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Salome Kitomari, Dar, George Marato, Musoma na John Ngunge, Arusha.

MY TAKE

kipindi hiki cha uchaguzi inabidi magazeti yetu yatoe taarifa zenye uhakika ili kupunguza kuchanganya wananchi

Bulaya aitosa CCM.

la kuvunda halina ubani, jembe linaachana na magamba
 
nilichokuwa Nakiwaza ndicho hichi ndicho kinaenda kutimia kuwa
Ester Bulaya anataka jimbo hilo hilo ambalo yumo Wasira sasa jiulize kwenye Kura za maoni
Wasira akatwe kweli? Wasira ambae kakaa sisiemu mda mrefu na ni eaziri wa kilimo na chakula asitunziwe heshima yake waje wampe Bulaya sijui.....
Bora aingie Upinzani ndo salama yake kutokana na mkoa wake ambao uko vizur kwa upinzani
 
asepe tu fisadi huyo, sasa kama alihonga mwanzo anautofauti gani hata akihama sasa.
 
Mzalendo aliye na akili zinazomtosha huwezi kumkuta CCM ya sasa...

CCM ilishapoteza dira miaka kadhaa iliyopita...
 
Bulaya kama upo humu jf ni pm please, nataka kuchangia pesa ya kuchukulia fomu
 
Team 4u wanaweweseka! Hata muendako hampati chochote ng'o.Bunda tunae kamanda alieanza harakati mapema.
 
Huyu, yule wa Mwibara, Deo, Lembeli, waondoke tu CCM maana si mahali pao, wasipoangalia hata kupitishwa wasingepitishwa

Kwa Deo Filikunjombe hawawezi kufanyia mchezo kwani ni nguzo ya ccm. Nae jamaa ni jembe la uhakika. Tayari wazee 300 wa jimbo lake wameshamchulia fomu za kugombea kwa gharama zao na kumpelekea nyumbani. Huyo hata bila kampeni anapita. Ukawa msipoteze nguvu na muda jimboni kwake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom