Ester Bulaya aitosa CCM, asema hawezi kuhonga

Ester Bulaya aitosa CCM, asema hawezi kuhonga

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga.

Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.

Chanzo: Nipashe

=====================
Update

Alichokisema Bulaya ni kuwa "Nitagombea Jimbo la Bunda Mjini lakini sitogombea kwa tiketi ya CCM, sina ugomvi na CCM wamenilea na nimekulia huko, na kutogombea kwangu kupitia CCM kusihusishwe na mtu na nafasi ya Urais.

Ila nimelitumikia Taifa langu nikiwa CCM naona nitalitumikia Vizuri zaidi nikiwa kwingine. Kumbukeni chama ni njia ya kupita ila umuhimu wa kulijenga Taifa letu ni la watanzania wote bila kujali vyama vyetu. Mungu ibariki Tanzania"
 
Kalibu dada nakukubali sana mungu akutie nguvu twende tumtoe mkoloni mweusi ccm
 
Anakaribishwa ndani ya cdm huyo mama ni mpambanaji sana
 
Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga. Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.

Source : gazeti Nipashe la leo

Rushwa ndani ya ccm ni kama samaki na maji.
Hii ndiyo sumu inayokiteketeza chama cha mapinduzi.
 
nnaona kipindi hiki propaganda zimepamba moto.

tutayasikia ya kweli na si ya kweli
 
Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga.

Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.

Source: Nipashe
Kama ndivyo,thumb up!karibu dada yetu jasiri na mpiganaji,vua gamba uvae gwanda!
 
Huyu, yule wa Mwibara, Deo, Lembeli, waondoke tu CCM maana si mahali pao, wasipoangalia hata kupitishwa wasingepitishwa
 
Hii sasa ndiyo saa ya mavuno......


Hongera kwa wote waliowekeza hata maisha yao kuufanya mfumo imara utakaochukua nchi October 2015!
 
ndani ya ccm bila kuhonga huwezi pata cheo kamwe. nilikuwa mbinga juzi mkoani ruvuma. wagombea wa ccm wanashindana kwa kuhonga. mbaya zaidi anayeongoza kwa kuhonga ndo anashabikiwa zaidi na wanaccm.
 
Kimbieni CCM hadi abaki Nepi,Mkuu wa kaya,Kinanii ..........Heshima itarudi tu,october mwisho
 
Kalibu ni aina ya pombe au ni kitu gani?

Acha ujinga wewe, mtu makini hawezi kukubali kuhonga mamilioni kwa ajili ya kura za maoni, maccm ni wapumbavu rushwa iliyokubuhu watu safi na viongozi makini wanaogopa kugombea.
 
karibuni uipiganie nchi yako achana na maharamia maccm hao yanahusudu rushwa.
 
Easter Bulaya, ni mtu wangu wa karibu. Ila mimi sina hizi habari. Nina mashaka na hizi taarifa.

Mandla.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom