ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

Njia ya kuzuia Haya yasitokee tena ni kurudisha rasmi ya pili ya katiba mpya jambo ambalo ni gumu kwa mfia ccm ila rahisi kwa wafia Tanzania
amini nakuambia ikiletwa ile rasimu watu wataponda tu
 
Fisadi anaibia hata polisiccm, polisiccm wanang'aa macho, wizi mchana kweupeeee! Dah! Ngoja waambiwe CHADEMA wanaandamana utawaona wanajivyofanya kuujua upolisi, lakini jamaa kawapiga 34 billion kimyaaaa.

Tena kwa kuwaibia polisiccm Lol!
 
Achukue hatua kwani alikuwa hajui nani mihusika Mkuu? alijuaje kama prof was innocent kama alikuwa hamjuui muhusika mkuu?. Kwani alipoahidi kuwalinda alimaanisha anawalinda kwa kitu gani walichotenda?watanzania tuamke kama bado tunalala?
Waafrika ndio maana tuna sifa ya ujuha. Watu wanaona ukweli hapo lakini watajibinua na kujipiga sarakasi mradi wasiuone. Kama unaogopa kubambikiwa kesi ya uchochezi ni bora kunyamaza badala ya kujiabisha. Shida kwa utamaduni wetu, watu hawaoni aibu kujifanya majuha.
 
Jibu sahii Ni hili soma ile hukumu Tena:
"
"SCB-HK understands that PAP used $75 million of the funds obtained from the escrow account to pay VIP Engineering and Marketing Limited (owned by Tanzanian businessman James Rugemalira) for its 30 per cent shareholding in IPTL," says part of the 100-page ruling.

"The funds held in the escrow account that should have been available to satisfy TANESCO's payment obligations to IPTL under the PPA (power purchase agreement) have therefore been paid to two Tanzanian parties - VIP and PAP - neither of whom made any financial contribution to the construction of the facility," it adds."

Hizo pesa zilikuwa mkopo Siyo zawadi hiyo pesa hawakuitolea jasho. Ruge Na PAP wote wezi.


Wakuu habari za muda huu,kama ilivyo ada nawaletea facts tupu bila majungu wala upendeleo wowote.
Nawaomba tutumie muda tulivu kuyasoma na kuyachambua kwa umakini.

Ni hivi,muda wa kuweka mambo yote hadharani sasa umefika,hakuna la kuficha tena...Hili sakata ambalo kila kukicha watanzania wamekua wakipotoshwa na ukweli wa jambo,hasa kwa lengo la kutaka kuwalinda wahuskia wakuu,sasa umefika mwisho,nitaeleza kwa ufupi tu.

1. PESA ZILIVYO HAMISHWA/IBIWA BANK KUU.

Taarifa rasmi na za uhakika,pia kulingana na hukumu ya jaji UTAMWA kama inavyo onesha katika viambatanisho vya hukumu iyo hapo chini,pesa hizo zilihamishwa kutoka benki kuu tarehe 5 Desemba 2013.Pesa hizi zilihamishwa bila mbia mmojawapo alie kuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa hizo kuwa na taarifa yoyote wala kujua kinacho endelea.

2:KIBALI NA SABABU YA KUHAMISHA PESA HIZO.
Taarifa za uhakika zinasema pesa hizo zilihamishwa bank kuu BoT bila mbia huyo kuwa na taarifa,zilipata kibali maalumu kutoka Ikulu (Rais wa kipindi husika),na hapa ndipo Gavana wa benki kuu alipo amua kujali maslahi ya kazi yake pasipo kujali weredi wa taaruma yake kwani hakutakiwa kuruhusu pesa hizo kuhama pasipo wabia wote wawili yani VIP na PAP kukubaliana.

Inasemekana mp-ango ulikua kuiba pesa hizo kwa makubaliano maalum ya Singa singa na taasisi hizo za juu alafu mbia wa upande mwingine afanyiwe 'MANYUVA'

3:NAMNA VIP ALIVYOPATA MALIPO YAKE YA HISA 30%.
Baada ya Rugemalira kushtuka kujua pesa zote tayari zilisha kombwa BoT bila taarifa,akakimbilia mahakamani tarehe 21 january 2014 (hapa ikumbukwe pesa ziliibiwa BoT tarehe 5 December 2013) ambayo ikawa msingi na sababu ya malipo yake halali.

Singa Singa alipoona jamaa kakimbilia mahakamani aliwaambia jamaa kuwa ni heri mumlipe jamaa madai yake bila hivyo kwa ninavyo mfahamu jamaa huyu (Ruge) hakitaeleweka!
Alikua akiwambia akina nani??bila shaka majibu mnayo taasisi kubwa kabisa kuliko zote....

4:KESI MAHAKAMANI.
Kesi ikaenda mahakamani,na madai ya Ruge kama yalivyo hainishwa katika viambatanishi hapo chini akitaka mahakama ikamate akaunti zote za PAP na mali zake zote popote pale zilipo na izizuie mpaka atakapo lipwa haki yake stahiki.
Madai yapo mengi mnaweza kusoma wenyewe chini.

5:MALIPO YA MBIA WA 30% (RUGE).
Baada ya mambo kuwa moto mahakamani,ni baada ya Ruge kuchachamaa,Singa singa na wezi wenzie walio shirikiana kuiba pesa BoT kwa kibali na baraka maalum wakaomba shitaka liondolewe mahakamani na warudi mezani wakae na kuyamaliza na Ruge.

Wakakaa na kukubaliana wamlipe jamaa ila chini ya mashariti ambayo pia mahakama iliyabariki kama mtakavyo ona ktk viambatanishi.
Walikubaliana kumlipa na yeye akataka pesa zake zote zilipwe kupitia benki ya mkombozi ambako aliamini zitakua salama kabisa.

Pia wakakubaliana Ruge aondoe mashitaka yote mahakamani lakini pia afunge mjadala na kibaya zaidi HARUHUSIWI KULIZUNGUMZIA POPOTE SUALA HILI LA ESCROW.
Hapa mtaelewa ndio maana ktk sakata zima mpaka kesho hujawahi kumsikia jamaa huyu RUGE akisema chochote wala kuzungumza mahala popote juu ya sakata hili la ESCROW ,ni kutokana na hukumu iyo ya mahakama ya jaji UTAMWA.

Mahakama pia kwa kujiridhisha kuwa pesa hizi zilikua halali kwake Mr Ruge wakamtaka pia mara tu baada ya kupata malipo yake basi wamkate kodi ya serikali ambayo ni karibu bil38,kodi hii ilikatwa juu kwa juu na bank mara tu malipo yalipo fanyika

Kwa maana hiyo,kimsingi na kisheria huyu jamaa RUGE hakuwa na pesa za ESCROW,pesa za ESCROW account zilisha ibiwa mda bila yeye kujua,yeye alijua baadae ndipo akaenda kudai haki mahakamani.Bila ivyo hasinge ambulia chochote.

Na kwa wale wanao fatilia mambo mtakubakiana kabisa na mimi,myonge mnyongeni haki yake mpeni,huyu jamaa ni mzalendo wa kutosha kabisa,kwanza nyuma alisha ishitaki hii IPTL ambayo naye alikua mbia kuwa inawalalia watanzania kwa kuwa na gharama kubwa za uendeshaji.

6:HITIMISHO
Baada ya malipo hayo ndipo jamaa akafanya yake kama anavyo laumiwa kuwa alitoa rushwa lakini kimsingi kuna maswali ya msingi ya kujiuliza:

>Kama jamaa alipata pesa alizo kuwa ameporwa bila kujua na akaja kupata mahakamani,na akalipa kodi ya serikali kama alivyo takiwa,wizi wake hapa uko wapi?

>Upande wa pili ambao ulikua na hisa zaidi ya 70% ambao ndio walio husika kuiba pesa hizo kwa msaada wa Ikulu,lakini pia kwa kutumia benki ya Stanbic kugawa mabilioni ya pesa na mpaka sasa hakuna hata alie hoji wala kutaja orodha iyo ambako kuna semekana vigogo na vinara wakubwa wa wizi huo wako huko,na bank husika bado inafanya shughuli zake bila matatizo yoyote.Pia ikumbukwe huyu mbia alie miliki asilimia 70% pamoja na utapeli wote lakini pia hakulipa serikalini kodi hata senti moja??Je kuna nini upande huo??

Swali kubwa na la msingi sana,ni kuona na kutafakari kwanini kila kukicha kelele ni zile zile za watu wa Mkombozi Bank ambao pamoja na yote mpaka sasa mahakama zimeshindwa kuwachukulia hatia kwasababu zimeona hakuna makosa aliyo fanyika kwani Ruge alikua na mamlaka ya kutumia pesa zake atakavyo.ila mbona kuna nguvu kubwa hisio ya kawaida inatumika kuwalinda hawa jamaa wa upade wa pili wakiongozwa na bwana Singa singa??

Wadau naomba niishie hapo kwa leo,tafadhari pitia hukumu hii kwa umakini hapa chini na tujadili.

Nawasilisha

View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405593 View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405598 View attachment 405599 View attachment 405600
 
Angeweza kama angepata Support. Kila kukicha ni kumkashifu,kumvunjia heshima, kudharau, kumdhalilisha kumtukana n.k Halafu eti unataka afukue vya mtangulizi wake kwa watu wasio na shukrani kama ninyi. Naamini na yy ameona ninyi si wa kuwakimbilia. Unafikiri nani atakuwa mfariji wake. Mimi nahakika Magu angeweza kufanya yasiyotarajiwa kwa kuwa ana uthubutu ila ss anamfanyia nani? Ss tuliowanafiki hata shukrani hatuna. .ili akikorofishana na wenzake tukae tumcheke. ..peleka huko upuuzi wako !!

Usiyekuwa na shukrani ni wewe unayeishi kama SHETANI.
 
Well presented, tusubiri maoni ya wananchi wengine
Duuh!!!!! Hapa Rais wetu ana kazi kubwa mno, I presume the leaders who are with our President at the Palace have briefed him regarding this scandal, as usual the President should not rely on advice given by people from the inner circle(Palace) only but should seek additional information from the outsiders since the insiders are likely to deceive the leader for their advantages. Once you go through the message(document) it seems the former president was ill advised by his insiders - I mean the inner circle who might have benefited from the loot. Truly "HAPA KAZI TU".
 
Hivi bado CCM wanayo moral authority ya kuongoza nchi hii kweli? Na sijui JPM anajisikiaje kuwa mwenyekiti wa chama kama hiki huku yeye mwenyewe akijivisha joho la mtetezi wa wanyonge. I don't understand.Kwa bahati mbaya sana katika serikali hii bado tunaona dalili za wazi za kuwalinda mafisadi badala ya kuwashuhulikia kwa nguvu zote. Mahakama zipo, mahakimu wapo, mafisadi wapo, nini tatizo? Inakera kwa kweli.
Unasahau na hawa DPP yupo, polisi wapo, watuhumiwa wapo wanajukana, sheria zipo, tatizo sina uhakika kama tanaye Rais wa kugusa pale ESCROW SAGA.
 
jamani lumumba wapo kuja kutetea huu uzi, lizabon, simiyu yetu, jingalao na faizafoxy mko wapi, kujeni humu
 
Nyie wote mnaojifanya eti ' oh magu sijui atalifukua hili sakata ' Mumuache raisi wetu kama alivyo. Afanye kwa ajili ya nani wanafiki ninyi. Kila kukicha mnamwombea mabaya. Kwanza tulivyokuwa tunanyonywa ni sawasawa kwa mi jitu yenye roho mbaya kama ninyi. Ss hivi ndiyo mnajidai kuona uchungu wa escrow. Halafu mnamtaka magu afukue lililolala. ..Hata ningekuwa mimi nisingefanya.
Mnamwita majina mabaya eti dictator. ..dictator huku unamtukana halafu unatembea barabarani?
Ukiangalia hizo Kiki za eti kutaka kuonyeshwa kwenye t.v mara tufanye mikutano. Hivi hivyo vyote vinauzito kiasi gani kulinganisha na Mapambano ya kuinua uchumi wetu.
Mi nasema hivi ninyi ni mazombi wote mnaomtukana na kumkashifu raisi wakati huo huo mkimtaka achukue hatua kwenye kashfa ya escrow!
Kuna aliemtukana akatembea barabarani? We kweli pimbi
 
Mimi sina chama ila naichukia chadema tangu watuuze. Wakati nikiwa arusha tulipigwa sana mabomu ya machozi. Damu nyingi ilimwagika kusimamia chadema.lakini walichokitenda. ...
Turudi kwenye mada, Mkuu wewe ni shahidi magufuli anamsuli /stamina ya kupambana lakini leo hii amnamtaka apambane na mtangulizi wake seriously? Kwa faida ya watu ambao wanamchamba kila kukicha? Hawampi moyo. Hawanashukrani? Hata ungekuwa ww rafiki unayemwona ni rafiki mpaka kufikia kujitoa kwa ajili yake anakusaliti kukusengenya kukusingizia mabaya, kukuchongea. Hivi uendelee kuwa naye halafu uachane na yule a naye kuffariji na Kukutia moyo? Jamani acheni utani. Hata ninyi hamwezi. Moyo wake wa nyama anajua mnachokifanya na anaumia vile vile.
Ila kwa kuwa kajitoa kafara Mungu amtie nguvu kufanya impossible kwa mijitu isiyo na shukrani kama ninyi
Wanaomsema ni CCMSscrow kwani? Unatetea ujinga tu wewe. Ye kama rais anapaswa achukue hatua. Bila kujali anamfurahisha nani.

Kama kuna uozo humo Escrow anapaswa achukue hatua. Akiacha ndo anaharibu zaidi na kuonyesha jinsi Escrow na CCM haviachani.
 
Na aache wala asishughulikie hata moja. Kwani atagombana bure na mtangulizi wake kwa mijitu isiyo na shukrani.
Magufuli nafikiri aendelee kufanya haki kwa kipindi chake na siku ya hukumu atahesabiwa haki. Naamini ataanza kupambana na wote watakaozishika pesa za serikali kama wazi ri mkuu alivyotaadhalisha kuwa kwa atakayezigusa zitamuunguza
Magufuli aanzie hapo alipo na mambo ya nyuma mumuweke mamvi wenu ili awapeleke mahakamani mafisadi wote wa kipindi cha Jk. Kwani wote uliowataja wametokea kwenye utawala uliopita
Hao wàlio rumande mda huu na waliotumbuliwa walikua kwenye utawala upi? Tumia ubongo kufikiria. Sio matako
Mweshimiwa rais kama ni kweli hizi habari basi wezi wa taifa hili wako wote wako serikalini
 
Back
Top Bottom