ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

Kumbe Ruge Yuko Clean!
yuko clean,na pia singer yuko clean,kisheria bado hujamfunga,
ndo maana yuko uraiani na PAP bado wanazalisha umeme na wana mpango wa kuexpand mpaka kuzalisha megawat 500,unless wawe wamepigwa stop juzi
 
Nwaigwe Kwani yeye kashughulikia mafisadi wapi? Kesi ya Lugumi imepaishwa,yule wa dakika 7 kaishia wapi? Yule wa bilioni 40 za polisi yuko wapi? Alieuza mashine ya Uhuru yuko wapi?
 
yule mzee ni dalali mzuri sana kumbe hata ishu ya bandari ya bagamoyo yumo?,
ila si wanajenga wachina na oman,ila yeye anajua kuupepeta mdomo,nadhani ndo coordinator ya shughuli nzima.
Hebu taja vitega uchumi vikubwa anavyomilki huyu babu,iwe hapa Tanzania ama south africa,ukiachia VIP
Huyu jamaa inasemekana pia anamiliki mgodi wa biramulo uko Kagera ni mwekezaji nzuri tu ndani ya Tigo pesa mi kuna mtoto wake mmoja tulisoma naye pia south africa
 
Yaaan wewe Unatetea wizi wa CCM how much they pay YOU ????
Yaani kwa mawazo yako yoote umeona mawazo ya members woote aproxmately 99.9% wanalaan huuu uchwara wa viongozi umeona hayafai ???

Asa unalialia et wakuu wakigombana mara ss
tukae na kuwacheka, wat's important mkuu kulipigania taifa akakosana na mmoja au kumlinda mmoja akawaumiza mamillion ya watz ??
Naamini unaakili timamu ndo maana uko hum tumia ubongo wako vizur CCM sio Mama wala Baba ako
Mimi sina chama ila naichukia chadema tangu watuuze. Wakati nikiwa arusha tulipigwa sana mabomu ya machozi. Damu nyingi ilimwagika kusimamia chadema.lakini walichokitenda. ...
Turudi kwenye mada, Mkuu wewe ni shahidi magufuli anamsuli /stamina ya kupambana lakini leo hii amnamtaka apambane na mtangulizi wake seriously? Kwa faida ya watu ambao wanamchamba kila kukicha? Hawampi moyo. Hawanashukrani? Hata ungekuwa ww rafiki unayemwona ni rafiki mpaka kufikia kujitoa kwa ajili yake anakusaliti kukusengenya kukusingizia mabaya, kukuchongea. Hivi uendelee kuwa naye halafu uachane na yule a naye kuffariji na Kukutia moyo? Jamani acheni utani. Hata ninyi hamwezi. Moyo wake wa nyama anajua mnachokifanya na anaumia vile vile.
Ila kwa kuwa kajitoa kafara Mungu amtie nguvu kufanya impossible kwa mijitu isiyo na shukrani kama ninyi
 
amuwezi kikwete huyu, kikwete mtoto wa mjini, anajua kuzichanga karata zake vzr...

ila pia wadau wiki hii mwanzon mwa juma, wadau wa BOT wanadai kuna-department iliwaka monto na kuunguza nyaraka mbali mbali na ukazimwa kimya kimya na hawakutaka taarifa itoke kwenye vyombo vya habar
 
amuwezi kikwete huyu, kikwete mtoto wa mjini, anajua kuzichanga karata zake vzr...

ila pia wadau wiki hii mwanzon mwa juma, wadau wa BOT wanadai kuna-department iliwaka monto na kuunguza nyaraka mbali mbali na ukazimwa kimya kimya na hawakutaka taarifa itoke kwenye vyombo vya habar
Kama ni kweli wana bahati nzuri kila mara wanawakiwa na moto
 
Pesa ya mdafu hata mia inapigwa by jay moe


Daaah hatari sana
 
Pesa ya mdafu hata mia inapigwa by jay moe


Daaah hatari sana
 
ila pia najuliza Kwann KIPILIMBA alitolewa BOT kwenda NEC (nadhan kuhakikisha ccm inashinda) na baadae kwenda NIDA na baadae kupewa usalama wa taifa na kimsingi huyu mzee alikuwa BOT upande wa risk na tehama, baada ya IPTL kuishinda TANESCO, nyaraka zikaungua kule BOT..

JPM amuwezi mtoto wa mjini JK, aliacha kachanga karata zake vzr
 
Pesa ya mdafu hata mia inapigwa by jay moe


Daaah hatari sana
 
"Handle With Care". Katika mataifa yetu machanga ambayo Taasisi nyeti ni dhaifu inahitaji umakini mkubwa sana kushughulikia mambo makubwa kama haya.
 
Kwani yeye kashughulikia mafisadi wapi? Kesi ya Lugumi imepaishwa,yule wa dakika 7 kaishia wapi? Yule wa bilioni 40 za polisi yuko wapi? Alieuza mashine ya Uhuru yuko wapi?
Na aache wala asishughulikie hata moja. Kwani atagombana bure na mtangulizi wake kwa mijitu isiyo na shukrani.
Magufuli nafikiri aendelee kufanya haki kwa kipindi chake na siku ya hukumu atahesabiwa haki. Naamini ataanza kupambana na wote watakaozishika pesa za serikali kama wazi ri mkuu alivyotaadhalisha kuwa kwa atakayezigusa zitamuunguza
Magufuli aanzie hapo alipo na mambo ya nyuma mumuweke mamvi wenu ili awapeleke mahakamani mafisadi wote wa kipindi cha Jk. Kwani wote uliowataja wametokea kwenye utawala uliopita
 
Wakuu habari za muda huu,kama ilivyo ada nawaletea facts tupu bila majungu wala upendeleo wowote.
Nawaomba tutumie muda tulivu kuyasoma na kuyachambua kwa umakini.

Ni hivi,muda wa kuweka mambo yote hadharani sasa umefika,hakuna la kuficha tena...Hili sakata ambalo kila kukicha watanzania wamekua wakipotoshwa na ukweli wa jambo,hasa kwa lengo la kutaka kuwalinda wahuskia wakuu,sasa umefika mwisho,nitaeleza kwa ufupi tu.

1. PESA ZILIVYO HAMISHWA/IBIWA BANK KUU.

Taarifa rasmi na za uhakika,pia kulingana na hukumu ya jaji UTAMWA kama inavyo onesha katika viambatanisho vya hukumu iyo hapo chini,pesa hizo zilihamishwa kutoka benki kuu tarehe 5 Desemba 2013.Pesa hizi zilihamishwa bila mbia mmojawapo alie kuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa hizo kuwa na taarifa yoyote wala kujua kinacho endelea.

2:KIBALI NA SABABU YA KUHAMISHA PESA HIZO.
Taarifa za uhakika zinasema pesa hizo zilihamishwa bank kuu BoT bila mbia huyo kuwa na taarifa,zilipata kibali maalumu kutoka Ikulu (Rais wa kipindi husika),na hapa ndipo Gavana wa benki kuu alipo amua kujali maslahi ya kazi yake pasipo kujali weredi wa taaruma yake kwani hakutakiwa kuruhusu pesa hizo kuhama pasipo wabia wote wawili yani VIP na PAP kukubaliana.

Inasemekana mp-ango ulikua kuiba pesa hizo kwa makubaliano maalum ya Singa singa na taasisi hizo za juu alafu mbia wa upande mwingine afanyiwe 'MANYUVA'

3:NAMNA VIP ALIVYOPATA MALIPO YAKE YA HISA 30%.
Baada ya Rugemalira kushtuka kujua pesa zote tayari zilisha kombwa BoT bila taarifa,akakimbilia mahakamani tarehe 21 january 2014 (hapa ikumbukwe pesa ziliibiwa BoT tarehe 5 December 2013) ambayo ikawa msingi na sababu ya malipo yake halali.

Singa Singa alipoona jamaa kakimbilia mahakamani aliwaambia jamaa kuwa ni heri mumlipe jamaa madai yake bila hivyo kwa ninavyo mfahamu jamaa huyu (Ruge) hakitaeleweka!
Alikua akiwambia akina nani??bila shaka majibu mnayo taasisi kubwa kabisa kuliko zote....

4:KESI MAHAKAMANI.
Kesi ikaenda mahakamani,na madai ya Ruge kama yalivyo hainishwa katika viambatanishi hapo chini akitaka mahakama ikamate akaunti zote za PAP na mali zake zote popote pale zilipo na izizuie mpaka atakapo lipwa haki yake stahiki.
Madai yapo mengi mnaweza kusoma wenyewe chini.

5:MALIPO YA MBIA WA 30% (RUGE).
Baada ya mambo kuwa moto mahakamani,ni baada ya Ruge kuchachamaa,Singa singa na wezi wenzie walio shirikiana kuiba pesa BoT kwa kibali na baraka maalum wakaomba shitaka liondolewe mahakamani na warudi mezani wakae na kuyamaliza na Ruge.

Wakakaa na kukubaliana wamlipe jamaa ila chini ya mashariti ambayo pia mahakama iliyabariki kama mtakavyo ona ktk viambatanishi.
Walikubaliana kumlipa na yeye akataka pesa zake zote zilipwe kupitia benki ya mkombozi ambako aliamini zitakua salama kabisa.

Pia wakakubaliana Ruge aondoe mashitaka yote mahakamani lakini pia afunge mjadala na kibaya zaidi HARUHUSIWI KULIZUNGUMZIA POPOTE SUALA HILI LA ESCROW.
Hapa mtaelewa ndio maana ktk sakata zima mpaka kesho hujawahi kumsikia jamaa huyu RUGE akisema chochote wala kuzungumza mahala popote juu ya sakata hili la ESCROW ,ni kutokana na hukumu iyo ya mahakama ya jaji UTAMWA.

Mahakama pia kwa kujiridhisha kuwa pesa hizi zilikua halali kwake Mr Ruge wakamtaka pia mara tu baada ya kupata malipo yake basi wamkate kodi ya serikali ambayo ni karibu bil38,kodi hii ilikatwa juu kwa juu na bank mara tu malipo yalipo fanyika

Kwa maana hiyo,kimsingi na kisheria huyu jamaa RUGE hakuwa na pesa za ESCROW,pesa za ESCROW account zilisha ibiwa mda bila yeye kujua,yeye alijua baadae ndipo akaenda kudai haki mahakamani.Bila ivyo hasinge ambulia chochote.

Na kwa wale wanao fatilia mambo mtakubakiana kabisa na mimi,myonge mnyongeni haki yake mpeni,huyu jamaa ni mzalendo wa kutosha kabisa,kwanza nyuma alisha ishitaki hii IPTL ambayo naye alikua mbia kuwa inawalalia watanzania kwa kuwa na gharama kubwa za uendeshaji.

6:HITIMISHO
Baada ya malipo hayo ndipo jamaa akafanya yake kama anavyo laumiwa kuwa alitoa rushwa lakini kimsingi kuna maswali ya msingi ya kujiuliza:

>Kama jamaa alipata pesa alizo kuwa ameporwa bila kujua na akaja kupata mahakamani,na akalipa kodi ya serikali kama alivyo takiwa,wizi wake hapa uko wapi?

>Upande wa pili ambao ulikua na hisa zaidi ya 70% ambao ndio walio husika kuiba pesa hizo kwa msaada wa Ikulu,lakini pia kwa kutumia benki ya Stanbic kugawa mabilioni ya pesa na mpaka sasa hakuna hata alie hoji wala kutaja orodha iyo ambako kuna semekana vigogo na vinara wakubwa wa wizi huo wako huko,na bank husika bado inafanya shughuli zake bila matatizo yoyote.Pia ikumbukwe huyu mbia alie miliki asilimia 70% pamoja na utapeli wote lakini pia hakulipa serikalini kodi hata senti moja??Je kuna nini upande huo??

Swali kubwa na la msingi sana,ni kuona na kutafakari kwanini kila kukicha kelele ni zile zile za watu wa Mkombozi Bank ambao pamoja na yote mpaka sasa mahakama zimeshindwa kuwachukulia hatia kwasababu zimeona hakuna makosa aliyo fanyika kwani Ruge alikua na mamlaka ya kutumia pesa zake atakavyo.ila mbona kuna nguvu kubwa hisio ya kawaida inatumika kuwalinda hawa jamaa wa upade wa pili wakiongozwa na bwana Singa singa??

Wadau naomba niishie hapo kwa leo,tafadhari pitia hukumu hii kwa umakini hapa chini na tujadili.

Nawasilisha

View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405593 View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405598 View attachment 405599 View attachment 405600
Mweshimiwa rais kama ni kweli hizi habari basi wezi wa taifa hili wako wote wako serikalini
 
Na aache wala asishughulikie hata moja. Kwani atagombana bure na mtangulizi wake kwa mijitu isiyo na shukrani.
Magufuli nafikiri aendelee kufanya haki kwa kipindi chake na siku ya hukumu atahesabiwa haki. Naamini ataanza kupambana na wote watakaozishika pesa za serikali kama wazi ri mkuu alivyotaadhalisha kuwa kwa atakayezigusa zitamuunguza
Magufuli aanzie hapo alipo na mambo ya nyuma mumuweke mamvi wenu ili awapeleke mahakamani mafisadi wote wa kipindi cha Jk. Kwani wote uliowataja wametokea kwenye utawala uliopita

 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom