ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

Nyie wote mnaojifanya eti ' oh magu sijui atalifukua hili sakata ' Mumuache raisi wetu kama alivyo. Afanye kwa ajili ya nani wanafiki ninyi. Kila kukicha mnamwombea mabaya. Kwanza tulivyokuwa tunanyonywa ni sawasawa kwa mi jitu yenye roho mbaya kama ninyi. Ss hivi ndiyo mnajidai kuona uchungu wa escrow. Halafu mnamtaka magu afukue lililolala. ..Hata ningekuwa mimi nisingefanya.
Mnamwita majina mabaya eti dictator. ..dictator huku unamtukana halafu unatembea barabarani?
Ukiangalia hizo Kiki za eti kutaka kuonyeshwa kwenye t.v mara tufanye mikutano. Hivi hivyo vyote vinauzito kiasi gani kulinganisha na Mapambano ya kuinua uchumi wetu.
Mi nasema hivi ninyi ni mazombi wote mnaomtukana na kumkashifu raisi wakati huo huo mkimtaka achukue hatua kwenye kashfa ya escrow!
kumbe tuna machizi humu jf!!!
 
Hawana wengine zaidi ya mkono

Saiv wanasema wanasheria wa tanesco wakate rufaa
Wakati nimefatlia tarifa ya zito ni kuwa hiyo ni mahakama ya mwisho sasa sjui rufani inakatwaje pia sielew daily news na habari leo yana milikiwa na nanii
Ndio maana uteuzi wa mwanasheria mkuu Tundu alicheka kwa kejeli, alijua rough atakayomchezesha😀😀
 
hivi kuna wizi mkubwa kama kuiba nyumba za serikali na kujigawia na zingine kupewa michepuko...ccm hawampi mtu cheo kikubwa bila kuwa na ushahidi ya uchafu wake ili asijekuwageuka...unafikiri ile kauli ya nitawalinda ilitoka kwa bahati mbaya...siku huyu magu wenu akichukua hatua kwenye escrow kwa kuwakamata mapapa nitaenda kukata gogo posta kwenye sanamu la yule askari mgoloko aliyevaa kaptula
 
Mbona hajatajwa wanayemuita fisadi papa,double standard ndio itaimaliza hii nchi.
 
Ndio maana uteuzi wa mwanasheria mkuu Tundu alicheka kwa kejeli, alijua rough atakayomchezesha😀😀
Tanzania yangu ccm ipo kimaslah kwani wanapiga dili kwa mfumo huohuo kesi zote wameshindwa yaan wana double cross tuu kwakua wanapiga dili na wenye kesi ili wapat 10% hakuna kesi walo wahi shinda against nation kwani kiuzalendo wanavo teuana nyadhifa kichama au walivofanya kumchagua mzee wa parole waache chuki kibatala na lisu wangechaguliwa kizalendo tuu hta bila kuwachagua bas wawape hzo kesi tupate kunufaika hta japo cku moja
 
Ni kama mzinga wa nyuki, uguse kwa tahadhari.

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme (Tanesco) imepanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) ya Uingereza ya kulitaka shirika hilo kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.4 (Sh bilioni 311).
 
Kuna watu walianza kusifia kuwa awamu Hii ni ya kupambana na Ufisadi, tukawaambia kuwa msivuke mto kabla hamjaufikia.
 
ila pia najuliza Kwann KIPILIMBA alitolewa BOT kwenda NEC (nadhan kuhakikisha ccm inashinda) na baadae kwenda NIDA na baadae kupewa usalama wa taifa na kimsingi huyu mzee alikuwa BOT upande wa risk na tehama, baada ya IPTL kuishinda TANESCO, nyaraka zikaungua kule BOT..

JPM amuwezi mtoto wa mjini JK, aliacha kachanga karata zake vzr
Hii inaitwa kuunganisha doti.
 
Na aache wala asishughulikie hata moja. Kwani atagombana bure na mtangulizi wake kwa mijitu isiyo na shukrani.
Magufuli nafikiri aendelee kufanya haki kwa kipindi chake na siku ya hukumu atahesabiwa haki. Naamini ataanza kupambana na wote watakaozishika pesa za serikali kama wazi ri mkuu alivyotaadhalisha kuwa kwa atakayezigusa zitamuunguza
Magufuli aanzie hapo alipo na mambo ya nyuma mumuweke mamvi wenu ili awapeleke mahakamani mafisadi wote wa kipindi cha Jk. Kwani wote uliowataja wametokea kwenye utawala uliopita
Yaani ni mbugila kiwango cha PHD, au ni mojawapo ya nafisadi?
 
Mi nikajua unaleta ukweli wa upande wa singasinga na zile 70% zilikoenda kumbe unarudia yaleyale tuliokwisha yasikia
 
Wakuu habari za muda huu,kama ilivyo ada nawaletea facts tupu bila majungu wala upendeleo wowote.
Nawaomba tutumie muda tulivu kuyasoma na kuyachambua kwa umakini.

Ni hivi,muda wa kuweka mambo yote hadharani sasa umefika,hakuna la kuficha tena...Hili sakata ambalo kila kukicha watanzania wamekua wakipotoshwa na ukweli wa jambo,hasa kwa lengo la kutaka kuwalinda wahuskia wakuu,sasa umefika mwisho,nitaeleza kwa ufupi tu.

1. PESA ZILIVYO HAMISHWA/IBIWA BANK KUU.

Taarifa rasmi na za uhakika,pia kulingana na hukumu ya jaji UTAMWA kama inavyo onesha katika viambatanisho vya hukumu iyo hapo chini,pesa hizo zilihamishwa kutoka benki kuu tarehe 5 Desemba 2013.Pesa hizi zilihamishwa bila mbia mmojawapo alie kuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa hizo kuwa na taarifa yoyote wala kujua kinacho endelea.

2:KIBALI NA SABABU YA KUHAMISHA PESA HIZO.
Taarifa za uhakika zinasema pesa hizo zilihamishwa bank kuu BoT bila mbia huyo kuwa na taarifa,zilipata kibali maalumu kutoka Ikulu (Rais wa kipindi husika),na hapa ndipo Gavana wa benki kuu alipo amua kujali maslahi ya kazi yake pasipo kujali weredi wa taaruma yake kwani hakutakiwa kuruhusu pesa hizo kuhama pasipo wabia wote wawili yani VIP na PAP kukubaliana.

Inasemekana mp-ango ulikua kuiba pesa hizo kwa makubaliano maalum ya Singa singa na taasisi hizo za juu alafu mbia wa upande mwingine afanyiwe 'MANYUVA'

3:NAMNA VIP ALIVYOPATA MALIPO YAKE YA HISA 30%.
Baada ya Rugemalira kushtuka kujua pesa zote tayari zilisha kombwa BoT bila taarifa,akakimbilia mahakamani tarehe 21 january 2014 (hapa ikumbukwe pesa ziliibiwa BoT tarehe 5 December 2013) ambayo ikawa msingi na sababu ya malipo yake halali.

Singa Singa alipoona jamaa kakimbilia mahakamani aliwaambia jamaa kuwa ni heri mumlipe jamaa madai yake bila hivyo kwa ninavyo mfahamu jamaa huyu (Ruge) hakitaeleweka!
Alikua akiwambia akina nani??bila shaka majibu mnayo taasisi kubwa kabisa kuliko zote....

4:KESI MAHAKAMANI.
Kesi ikaenda mahakamani,na madai ya Ruge kama yalivyo hainishwa katika viambatanishi hapo chini akitaka mahakama ikamate akaunti zote za PAP na mali zake zote popote pale zilipo na izizuie mpaka atakapo lipwa haki yake stahiki.
Madai yapo mengi mnaweza kusoma wenyewe chini.

5:MALIPO YA MBIA WA 30% (RUGE).
Baada ya mambo kuwa moto mahakamani,ni baada ya Ruge kuchachamaa,Singa singa na wezi wenzie walio shirikiana kuiba pesa BoT kwa kibali na baraka maalum wakaomba shitaka liondolewe mahakamani na warudi mezani wakae na kuyamaliza na Ruge.

Wakakaa na kukubaliana wamlipe jamaa ila chini ya mashariti ambayo pia mahakama iliyabariki kama mtakavyo ona ktk viambatanishi.
Walikubaliana kumlipa na yeye akataka pesa zake zote zilipwe kupitia benki ya mkombozi ambako aliamini zitakua salama kabisa.

Pia wakakubaliana Ruge aondoe mashitaka yote mahakamani lakini pia afunge mjadala na kibaya zaidi HARUHUSIWI KULIZUNGUMZIA POPOTE SUALA HILI LA ESCROW.
Hapa mtaelewa ndio maana ktk sakata zima mpaka kesho hujawahi kumsikia jamaa huyu RUGE akisema chochote wala kuzungumza mahala popote juu ya sakata hili la ESCROW ,ni kutokana na hukumu iyo ya mahakama ya jaji UTAMWA.

Mahakama pia kwa kujiridhisha kuwa pesa hizi zilikua halali kwake Mr Ruge wakamtaka pia mara tu baada ya kupata malipo yake basi wamkate kodi ya serikali ambayo ni karibu bil38,kodi hii ilikatwa juu kwa juu na bank mara tu malipo yalipo fanyika

Kwa maana hiyo,kimsingi na kisheria huyu jamaa RUGE hakuwa na pesa za ESCROW,pesa za ESCROW account zilisha ibiwa mda bila yeye kujua,yeye alijua baadae ndipo akaenda kudai haki mahakamani.Bila ivyo hasinge ambulia chochote.

Na kwa wale wanao fatilia mambo mtakubakiana kabisa na mimi,myonge mnyongeni haki yake mpeni,huyu jamaa ni mzalendo wa kutosha kabisa,kwanza nyuma alisha ishitaki hii IPTL ambayo naye alikua mbia kuwa inawalalia watanzania kwa kuwa na gharama kubwa za uendeshaji.

6:HITIMISHO
Baada ya malipo hayo ndipo jamaa akafanya yake kama anavyo laumiwa kuwa alitoa rushwa lakini kimsingi kuna maswali ya msingi ya kujiuliza:

>Kama jamaa alipata pesa alizo kuwa ameporwa bila kujua na akaja kupata mahakamani,na akalipa kodi ya serikali kama alivyo takiwa,wizi wake hapa uko wapi?

>Upande wa pili ambao ulikua na hisa zaidi ya 70% ambao ndio walio husika kuiba pesa hizo kwa msaada wa Ikulu,lakini pia kwa kutumia benki ya Stanbic kugawa mabilioni ya pesa na mpaka sasa hakuna hata alie hoji wala kutaja orodha iyo ambako kuna semekana vigogo na vinara wakubwa wa wizi huo wako huko,na bank husika bado inafanya shughuli zake bila matatizo yoyote.Pia ikumbukwe huyu mbia alie miliki asilimia 70% pamoja na utapeli wote lakini pia hakulipa serikalini kodi hata senti moja??Je kuna nini upande huo??

Swali kubwa na la msingi sana,ni kuona na kutafakari kwanini kila kukicha kelele ni zile zile za watu wa Mkombozi Bank ambao pamoja na yote mpaka sasa mahakama zimeshindwa kuwachukulia hatia kwasababu zimeona hakuna makosa aliyo fanyika kwani Ruge alikua na mamlaka ya kutumia pesa zake atakavyo.ila mbona kuna nguvu kubwa hisio ya kawaida inatumika kuwalinda hawa jamaa wa upade wa pili wakiongozwa na bwana Singa singa??

Wadau naomba niishie hapo kwa leo,tafadhari pitia hukumu hii kwa umakini hapa chini na tujadili.

Nawasilisha

View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405593 View attachment 405593 View attachment 405594 View attachment 405595 View attachment 405596 View attachment 405597 View attachment 405598 View attachment 405599 View attachment 405600
Kazi kweli kweli
 
Duuh!!!!! Hapa Rais wetu ana kazi kubwa mno, I presume the leaders who are with our President at the Palace have briefed him regarding this scandal, as usual the President should not rely on advice given by people from the inner circle(Palace) only but should seek additional information from the outsiders since the insiders are likely to deceive the leader for their advantages. Once you go through the message(document) it seems the former president was ill advised by his insiders - I mean the inner circle who might have benefited from the loot. Truly "HAPA KAZI TU".
yes, very likely His Honour is being mislead.. then probably tatizo likishatokea they take the easy way out and blame it on the "wapinzani" kama kweli hali iko hivi basi Mheshimiwa Rais ana kazi kubwa sana Mwenyezi Mungu amfunilie na kumwongoza aisee
 
Back
Top Bottom