more88
JF-Expert Member
- Apr 9, 2016
- 447
- 412
Aisee hawa vijana wanaosajili line mtaani wanafanya uhalifu ambao kimsingi wanatakiwa kwenda jela.
Leo nimehakiki line nilizosajili kwa kitambulisho cha NIDA, aisee nimeshangaa yani kukuta namba kibao ambazo sijazisajili kumbe kuna uhuni wanakufanyia unaposajili kumbe kuna namba zao wanazosajili kwa kutumia hicho hcho kitambulisho chako wakijidai network inasumbua.
Tunaomba mitandao ya simu ikemee hii tabia kwa hawa vijana wao maana kwa hali hii unaweza kujikuta mtu unaenda jela kumbe anayetumia ID yako, si wewe.
Hapa najipanga kwenda kufuta usajili wa hizi namba baada ya kutumiwa SMS kutoka TCRA. Jamani, hili ni angalizo kama unataka kusajili line bora kwenda ofisini kabisa kwenye shops zao kuliko kutumia hawa vijana.