Kuweni makini na wanaosajili line mtaani, wanajifanya mtandao unasumbu na kutumia taarifa zako kusajilia line nyingine. Fanya uhakiki wa line zako

Mr mutuu

JF-Expert Member
Jan 27, 2023
2,027
10,040
Jana nipo mtaani jioni wakapita madogo wawili wanasajili line, hawa sio wageni sana machoni huwa nawaona mara moja moja, basi nikawaita nikawa nasajili namba ya halotel. Sijawahi kuwa na line ya halotel hapo kabla.

Katika kusajili sarakasi zikawa nyingi mara mtandao unasumbua, mara ngoja nijaribu kutumia mashine ya mwenzangu, ikachukua muda kidogo. Kwasababu nilikua nimekaa mahali napata kinywaji nikawunulia soda pale wakiwa wanasubiri mtandao ukae sawa ikachukua let's say dakika 40 zoezi kukamilika wakinipa line yangu ya halotel.

Sasa leo nimeamka sijui nikachezwa na machale gani, nikawa naona kama hawa madogo kuna ujanja wamenifanyia, nikaingia menu ya *106# nicheki usajili namba za halotel zilizosajiliwa na nida yangu, aisee, nakuta nina namba za halotel 4!

Nikawa kama siamini, kumbuka jana ndio mara ya kwanza nasajili line ya halotel maishani mwangu! Nikaziandika hizi namba tatu ambazo sipo nazo pembeni nikazipiga zote hazipatikani.

Nikashikwa na hasira kweli, nikawa najiuliza hivi mtu akifanya uhalifu mkubwa kwa kutumia identity yangu si naweza kwenda jela bure au waanze ujinga wa ile hela tuma kwenye namba hii si ntaonekana nimeanza utapeli mjini.

Basi leo mchana kuna shughuli namalizia nimeamua kula sahani moja na huyu dogo, kwanza naanzia polisi naenda kuchukua rb, naenda halotel lazima watakuwa wanamjua aliyenisajilia hizi line naamsha noma huko mpaka kieleweke. Nataka niende makao makuu kabisa na waniambie ni hatua gani wanamchukulia huyu tapeli+ nizifutie usajili hizi line.

Nimeshafanya upelelezi wa mtaa nimeambiwa sehemu wanapokutana asubuhi kufanya morning briefing kabla hawajaanza kazi, kesho naenda kumwinda hapo ikiwezekana nimalizane nae 'kimtaa mtaa'.

Rai yangu, kuweni makini na hawa wasajili line ikiwezekana tuwe tunahakiki usajili wetu mara kwa mara, usajili wa line unabeba identity yetu ipo siku mtu anatumia identity yako akafanya tukio kubwa ukaja kuozea jela bure.
 
Inawezekana kwa vile mtandao ulikuwa unasubiri walikuwa wanajaribu wanafikiri hazijakubali kumbe kule usajili umefanikiwa. Yote yanawezekana wanaweza kuwa wamefanya kwa makusudi au bila kukusudia
 
Inawezekana kwa vile mtandao ulikuwa unasubiri walikuwa wanajaribu wanafikiri hazijakubali kumbe kule usajili umefanikiwa. Yote yanawezekana wanaweza kuwa wamefanya kwa makusudi au bila kukusudia
Line mpaka isome Kule ni lazima aiweke kwenye simu na ai activate kwa kuunga kifurushi chochote, na kuinganisha na miamala ya kipesa.... Hakuna Cha bahati mbaya hapa
 
Inawezekana kwa vile mtandao ulikuwa unasubiri walikuwa wanajaribu wanafikiri hazijakubali kumbe kule usajili umefanikiwa. Yote yanawezekana wanaweza kuwa wamefanya kwa makusudi au bila kukusudia
Kaka hao jamaa ni makusudi.
Haya malalamiko nimeyashuhudia hadi mtaani sio tu humu JF.
Ukisajili laini kama mtandao umegoma ni umegoma mzee hakuna cha kusema sijui haukujua labda ilikua ishajisajili.
 
Punguza jazba. Nenda ofisini kwao kazifute ni bure tu,epuka ugomvi usio na faida
 
Sawa lakini haileti mantiki kusajili line 'kiujanja janja'
huwa wanaenda kuziuza hizo lines kwa wahalifu au watu ambao wana zitumia vibaya. so si bahati mbaya ni makusudi na wanapata pesa sana line moja ni kuanzia tsh 30,000 mpaka 100, 000 inategemeana. kuna wengine wanasema wanauza mpaka tsh 300,000 inategemeana na mhitaji anataka akaifanyie nini
 
Punguza jazba. Nenda ofisini kwao kazifute ni bure tu,epuka ugomvi usio na faida
Sio jazba Hawa wanatakiwa kufukuzwa Hio kazi maana sio waaminifu, tatizo Kila kitu tunapenda kichukulia simple tu
 
Back
Top Bottom