Epuka uhalifu unaofanywa na wasajili laini za simu, piga *106# kuhakiki namba zilizosajiliwa kisha weka namba yako ya NIDA

more88

JF-Expert Member
Apr 9, 2016
447
412
Aisee hawa vijana wanaosajili line mtaani wanafanya uhalifu ambao kimsingi wanatakiwa kwenda jela.

Leo nimehakiki line nilizosajili kwa kitambulisho cha NIDA, aisee nimeshangaa yani kukuta namba kibao ambazo sijazisajili kumbe kuna uhuni wanakufanyia unaposajili kumbe kuna namba zao wanazosajili kwa kutumia hicho hcho kitambulisho chako wakijidai network inasumbua.

Tunaomba mitandao ya simu ikemee hii tabia kwa hawa vijana wao maana kwa hali hii unaweza kujikuta mtu unaenda jela kumbe anayetumia ID yako, si wewe.

Hapa najipanga kwenda kufuta usajili wa hizi namba baada ya kutumiwa SMS kutoka TCRA. Jamani, hili ni angalizo kama unataka kusajili line bora kwenda ofisini kabisa kwenye shops zao kuliko kutumia hawa vijana.
 
Ambacho nimeshindwa kuielewa hii mitandao ya simu ni kwann wameweka option ya kuangalia namba zinazotumia kitambulisho chako lakini ukitaka kuziondoa kma huzijui, inakubidi uende ofisini kwao.
 
Halafu hata wào ofisini utasikia kidole hiki kimegoma, mpaka nikamuuliza yaani nipo hapa network inasumbua ngoja nifuatilie, kuna mdada mkoani walipitisha vidole vyake vyote jamani vitano!

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Dawa yao wewe piga simu kwa Kampuni husika ripoti kwamba simu zako zimeibwa na unaomba wafunge hizo line.

Kisha Beba kitambulisho chako nenda ofisini kwao, omba kurenew line na taarifa zote za M/Tigopesa au kama ni mitandao mingine. Viasi vyote vitakavyokuwa kwenye hizo line ni halali yako kisheria, hakuna atakayekuwa na mamlaka ya kuja kukudai.
 
Hii safi sana
 
nimepiga simu nshazifunga Shida itakuwa namba za siri kwenye kutoa hzo pesa
 
Ambacho nimeshindwa kuielewa hii mitandao ya simu ni kwann wameweka option ya kuangalia namba zinazotumia kitambulisho chako lakini ukitaka kuziondoa kma huzijui, inakubidi uende ofisini kwao.
Ndo maana bdo napata sms za tuma kwenye namba hii
 
Huu mpango umekaa vizuri ni hatua nzuri kuelekea kupunguza uharifu wa mitandao hasa wale matapeli wa miamala.
 
nimepiga simu nshazifunga Shida itakuwa namba za siri kwenye kutoa hzo pesa
Nenda kwenye Ofisi zao pamoja na kitambulisho chako. Waambie umezisahau namba za siri wakusaidie Ku reset..

Wao Jukumu lao ni kuhakiki kwamba wewe kweli ndiye mmiliki halali Wa hizo namba. Na tayari zimesajiliwa kwa details zako..
 
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom