Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Roya Roy,Masanja,Kungurumweupe,

..kuna yeyote yule mwenye majibu ya Waziri wa Miundo mbinu?

..nitashangaa sana kama habari hii itaishia na madai ya Mporogomyi tu, bila kuweka majibu ya waziri mhusika.

NB:

..shahada ya Construction Economics, ina maana Mrema ni quantity surveyor au?

Binafisi sijafanikiwa kupata majibu ya waziri, lakini nafuatilia. Huu ufisadi wa tanroads hauwezi kufumbiwa macho hivihivi. Lazima kieleweke.
 
..kuna yeyote yule mwenye majibu ya Waziri wa Miundo mbinu?

Waziri alisema kwamba atafuatilia kwa kuwa alishasikia fununu hizo kitambo na kwamba ana wiki 6 tu ndani ya ile ofisi, kwa hiyo bado anahitaji muda zaidi ili kuchunguza ukweli wa tuhuma hizo.

By the way kuna mtu ana tangazo la nafasi hiyo ya kazi? Nina uhakika kwamba lazima kwenye basic qualifications watakuwa wametaja wanataka shahada za namna gani kwa ajili ya hiyo nafasi kwa kuwa ni kitu ambacho kiko more technical, na hivyo mtu hawezi kusema kwamba mtu mwenye degree yoyote anaweza kuingia hapo.
 
Yaani mimi mtu akishatamka WORLD BANK na ndugu zake ndo namuona anatulostisha kabisa..Hata akina Balali and co..walikuwa na utumishi uliotukuka huko World Bank, lakini mpaka leo ndo wametufukarisha.

Please whoever wants to make a point, atupe ila siyo hizi siasa za best student Olevel na resume ya World Bank nk..Na kama nimemuelewa Mporogomyi..anauliza hivi: IWEJE APPLICANT AMBAYE HAKUWEMO KWENYE TOP FOUR WALIOKUWA RECOMMENDED KUAJIRIWA APATE AJIRA? Interview haikuwa na maana tena! Ndilo swali linahitaji jibu..mengine ni longo longo tuu hapa..

Tatizo la watanzania...kwa sababu ya unafiki wetu..watu hapa wataanza kuligeuza hili swala kwenye ukabila kwamba jamaa anaonewa kwa vile ni mchagaa! Wakati watu wanauliza maswali na wanahitaji majibu! Period.

Masanja, you have said everything!

Jmushi na......... , mbona hamchangii rafiki zangu?! Au kwa vile anayeongelewa ni mrema wa tanroads?!
KULIKONI??!!
 
yaani sasa wadanganyika tumebakia kukimbilia huku na huko maana tunakwenda kusikilisa hii hadithi ya ufisadi kila mahali,leo bot,kesho epa,mtondogoo meremeta,mara tangold,ujakaa sawa kiwira.bado ujamaliza kusikilisa unasikia tena tanroad,mwisho imekuwa kizungumkuti
 
Keil said:
Ina maana huziamini data za Mh. Mbunge ambaye aliyasema hayo Bungeni na yeye (Mrema) akiwa ndani ya mjengo? Habari imetaja majina 4 ya watu ambao baada ya usaili (interview) walikuwa recommended kuchukua hiyo nafasi, lakini mtu ambaye hakuwamo kwenye orodha ndiyo akaja kupewa hiyo nafasi. Je, hapo ametumia njia gani kupata hiyo ajira? Au kuna inteview mbili zilifanyika kwa nyakati tofauti? Na kibaya zaidi records lazima zipo unless kama watu walicheza na ma-file na hata wale walio conduct interview wapo wanaweza kuulizwa na kutoa majibu kama Waziri atakuwa na nia ya kushughulikia hilo swala.

Keil,

..hatuwezi kutegemea kauli ya Mbunge peke yake ktk suala hili.

..nakumbuka kuna Mbunge alimshambulia Waziri wa Fedha kuhusu suala la mtumishi mmoja wa TRA.

..waziri alipokuja kutoa majibu ikabainika kwamba Mbunge alipewa hadithi nusu-nusu. ilibidi Mbunge aombe radhi kutokana na aibu aliyoingia.

..for the sake of fairness majibu ya Waziri ni muhimu hapa.

Sikonge said:
Juu ya Ukabila mie naunga mkono. Huu ugomvi ulikuwepo, upo na utaedelea kuwepo. Siyo siri kuwa makabila mengi yanawaonea wivu Wachaga, Wahaya, Wasukuma, Wakinga, Wanyakyusa ...... Ukifika Bukoba, Mwanza, Arusha/Kilimanjaro, Mbeya .... kwa kweli utashangaa kama uko Tanzania (baadhi ya maeneo). Kuna mikoa imesahaulika kabisa na tujikumbushe bajeti ya ujenzi wa Barabara ya Mramba. Sasa watu wakiona hata TANROAD iko chini ya Mchaga, na pesa zote zaenda huko kwa kweli unataka kulia.

Sikonge,

..kabla ya kujiaminisha kwa suala zito kama dhuluma ya kabila moja dhidi ya wananchi wenzao ni vizuri mhusika akafanya utafiti wa kina.

..yale malalamiko dhidi ya Mramba yalikuwa hayana msingi. mbunge alikuwa akilalamika kuhusu miradi ambayo iko katika stages tofauti.

..Mradi wa barabara ktk jimbo la Mramba ulikuwa ktk stage ya ujenzi. wakati mradi aliokuwa akilalamikia mbunge ulikuwa ktk stage ya usanifu. ndiyo maana ule mradi wa jimboni kwa mramba ukatengewa fedha nyingi zaidi ya mradi aliokuwa jimboni kwa mbunge.

..CEO wa Tanroads alikuwa raia wa Ghana mpaka sept mwaka jana. lakini tayari wananchi hapa jamii forums baada ya kusikia kwamba amekuwa replaced na Mchaga basi wamefikia kuita Tanroads kijiwe cha Wachaga.

..kuhusu upendeleo kwa miradi ya barabara kilimanjaro ni vizuri wana jambo forums wakapitia Tanroads, iko ktk website yao, na tuelezwe kama kuna upendeleo wowote ule.

..nadhani Watanzania tunaelekea ktk kuamini kwamba maendeleo yanapatikana kwa upendeleo tu. hatuamini tena ktk kufanya kazi kwa bidii, kujitolea, ushirika, etc etc.
 
Tunarukaruka kama Manyani hatujui ni mti gani tunaupenda tukabangaize! Thread nzima imekosa mwelekeo maana hakuna kinachoeleweka kinaendelea.

Nitachangia kwa mtazamo wangu kutokana na kauli ya Mbunge na mitazamo ya wachangiaji hapa.

1. Mbunge kahoji; Jinsi Mrema alivyopata kazi kwa mlango wa nyuma huku hakuwa kwenye Semi Fainali ya Usaili. Hili ni halali na muhimu kujua ni vipi Mrema aliweza kuletwa na kupewa kazi. Je kuna kumbukumbu za kuonyesha ni jinsi gani mchakato wa kutafuta CEO mpya ulivyofanyika? Je kuna provision gani za kuruhusu late applicants kama Mrema aliwasilisha CV yake wakati usaili umeanza? Je Alichaguliwa kwa Merits zipi na lile jopo lililomchagua yeye na si wengine?

2. Mbunge kahoji; Mshahara na marupurupu ya Mrema ni ya Kifisadi. Hili halina nguvu na tena lawezakuwa Mbunge alitumia hoja hii ili kulazimisha hoja yake ya Kwanza na ya tatu (kutishia wafanyakazi) zipate nguvu.
Kama Mghana aliyekuwepo alikuwa analipwa mshahara na marupurupu hayo hayo, kwa nini Mtanzania asilipwe hivyo hivyo? Kwa nini Mtanzania aendelee kuwa Daraja la Tatu lakini wengine wabebwe na kulipwa First Class? Je Mbunge na hata Wachangiaji wengine humu tumesahau kuwa tumelia kwa muda mrefu kuhusu Mishahara midogo na kupuuzwa? Je tunasahau katika mfumo wetu mpya wa Uchumi ambao umeachana na Ujamaa, ni kuwa mishahara si maamuzi ya Kamati kuu bali ni uwezo wa ushawishi wa anayetaka kazi kutaka alipwe mshahara unaolingana na Elimu, Uzoefu, Ufanisi na Utendaji (track record)? Kuna mwana JF katoa maoni kuwa akiwa Mtanzania alipwe Shilingi kwa kufuata viwango vya mishahara ya Serikali, lakini akiwa ni Mgeni asiye Mtanzania, basi tumlipe ki-ulaya ulaya, this does not make any sense. Kwa nini ajira ya kazi hiyo hiyo iwe na mishahara ya kiubaguzi?

3. Mbunge kahoji; Mrema alitishia ajira za mfanyakazi aliyefuata sheria. Hili ni haki na halali kuhoji kwa nini Mrema atishie maslahi ya mwingine kisa mfanyakazi kufuata kanuni? Hili pia linahitaji uthibitisho, maana mpaka sasa limekaa ki-umbea umbea na Mbunge sidhani kama amewasilisha vielelezo ikiwa ni pamoja na mfanyakazi kuandika barua ya kulalamika kwa Bodi ya Tanroads au kwenda Idara ya Kazi kuwasilisha malalamishi. Ikiwa itabainika Mrema ni kweli alitumia vitisho kupindisha kanuni, je ni hatua gani zichukuliwe kutokana na mwongozo wa kiutendaji (employee hand book)wa Tanroads?

4. JF inahoji; Wasifu wa Mrema. Kuna wanaosema ni mchumi wa ujenzi, project management, kafanya kazi katika mashirika mbali mbali ndani na ya imataifa katika masuala ya miuondo mbinu. Swali linarudi kwa wana JF, je ni lazima CEO wa Tanroads awe Mhandisi wa Ujenzi? what about Chemical Engineer, Electrical Engineer, Geologist, Architect, Lawyer, Economist, Accountant, Agro Economist, Nuclear Phycist?

Je kwa kuwa kazi ni kujenga barabara ni lazima awe ni mhandisi wa ujenzi (civil engineer) au kuwa na shahada ya Uhandisi wa Ujenzi ni added value na bonus?

Kazi ya CEO ni nini? ni kuchukua supatu, sululu, jembe, kisu, wrench, boiler na kuingia kazini au ni kusimamia uendeshaji mzima wa Taasisi kuhakikisha malengo ya Taasisi na kazi zake zinafanyika kwa Ufanisi? Je si kuna Wataalamu wa Research, Archirtect, Soil composition, Surveyors, Construction design, Civil Engineereing, Chemical Engineering, Accountants, Marketing, Environmental studies na fani nyingine ambao wamo katika Idara za Tanroads na wajibu wao ni kufanya kazi za kitaaluma kutumia Utaalamu wao kuhakikisha kila kitu ni sawa?

Hivyo basi kama track record ya Mrema ni mbovu na hana uwezo wa kutuonyesha alichofanya iwe Tanzania au kwingineko, basi si suala la Elimu yake bali ni ukosefu wa Ufanisi ambao tupigie kelele na kuhoji kwa nini kapewa majukumu makubwa wakati uwezo hana. Lakini kama kuna proven track record ya kazi alizosimamia na mashirika aliyofanya kazi, basi kulalama kuhusu CV yake ni waste of time.

5. JF na Ukabila; Badala ya kuangalia merits za mtu, tumeangalia ni kabila gani na ni yapi ambayo tunadhania kwa hisia kayafanya kwa Upendeleo wa Kikabila. Mzee Mwanakijiji kaanzisha mada nzuri sana inayoshibana na suala la Ukabila, Udini na kauliza kama 58% au 68% ya Kamati kuu ya CCM ni Waislamu, je ni sawa kudai CCM ina Udini?

Swali ni hili, jee Mrema alipofika Tanroads, ni Wataaalamu wangapi na Wakandarasi wangapi ambao ni mahiri ni Wachaga? Ikiwa 75% ya Wafanyakazi wataalamu wa Tanroads na Contractors ni Wachaga, tutamlaumuje Mrema kuwa yeye ni Mkabila? Je mnaodai ana ukabila, mna vithibitisho gani kuwa anafanya kazi kwa kutumia Ukabila na kutoa Upendeleo wa Mikataba kutokana na Ukabila?

5. Hisia na Upembuzo Yakinifu wa JF; Hapa JF ni Jungu Kuu ambalo lina watu kutoka makabila mbali mbali, fani mbalimbali na upeo tofauti. Kuna walioko Tanzania na walioko Ughaibuni.

Niaanza kwa kuzungumzia Ufanisi na Elimu. Suala la Tanroads na CEO wake si la kwanza kutuvuruga JF. Watanzania tunachanganya sana suala la Usomi na Uwezo wa kufanya kazi. Elimu ni nyenzo ya kufanya kazi, inasaidia kufanya kazi, lakini elimu haina maana mtu atakuwa mahiri na mwenye ufanisi, muadilifu au mnyenyekevu. Sisi tumejenga Tafsiri na kasumba potofu kuwa Ukiwa na Shahada na Udakitari, basi wewe ni bingwa. Kipimo cha Ufanisi wa mtu si Elimu na Shahada alizonazo, bali ni matendo yake, uwezo wake wa kuelewa mambo, Uwezo wa kuwa Mbunifu.

Kwa Tanzania ya sasa tunatafuta Malaika maana tumekulia na kuiva kutokana na watu wazembe, wavivu, wasio na tija na waliokosa motisha. Je kuwa na PHD ndio solution? hapana. Tanzania itaanza kuwa fanisi pale siku watu watyakapoamua kujipa motisha wa kuamka na kwendha kuchapa kazi, kutumia juhudi na maarifa waliyonayo.

Tanzania itapata maendeleo katika Utendaji wa mashirika,Serikali, Taasisi, Watu binafsi, Wafanyakazi na Wakulima , tukiamua kuachana na visingizio na visababu visivyo na msingi na focus yetu kuwa kuzalisha mali kwa bidii, ufanisi, ubora, tukiwa wabunifu, wenye tija na kuchochea motisha.

Tunalilia mishahara mikubwa, lakini hatuzalishi vya kutosha ili kukidhi matumizi ya uzalishaji na mishahara ya wafanyakazi. Je tutawezaje kupiga hatua? Ni vipi Mzungu, Mhindi, Mkenya, Mwarabu, Mchina wakija Tanzania wanakuwa na Ufanisi na Juhudi za kuchapa kazi lakini tukipewa hatamu sisi wenyewe tunashindwa kujiongoza na kujiendesha?

La mwisho ni kupotea kwa Watanzania katika mfumo wa Uzalishaji mali na Uchumi. Tumekomaa sana katika Ujamaa, mawazo yetu bado yako katika Ujamaa wa kulazimisha kuwa kuishi kimaskini ndio fahari ya Mtanzania. Tunaona "ubepari" kuwa ni unyama na kuwa na mishahara mikubwa ni Ubepari na Unyonyaji. Tunaona kuishi katika Ufukara ndio Utu, sawa, haki na thawabu, na labda pia ni kutokana na mapokeo yetu potofu ya Imani zetu hasa Ukristo kuwa ni Rahisi kwa masikini kuingia Mbinguni kuliko Tajiri ambaye ni sawa na Ngamia kupita tundu la sindano!

Ni mentality hii ambayo inatufanya tuone ni halali kwa Odhiambo, Montgomerry, Olatunde, Zhang, Iqbal na Al Muneiz walipwe mishahara ya Kimataifa wanapofanya kazi Serikalini mwetu au kwenye Mashirika yetu. Tunahalalisha wao kuwa Mabepari na Wanyonyaji bila hata kuwa na kinyongo zaidi ya kulalamika kuwa mbona sisi mishahara yetu ni kiduchu. Mbaya zaidi, ikiwa hawa Wageni wakazi ndio wenye makampuni yao na yanafanyakazi Tanzanzia, ufanisi wetu huwa marudufu ya Watanzania wenzetu wanaofanya kazi katika mashirika ya umma na Serikali.

Lakini tukisikia Masauni, Mallya, Mutakyamirwa, Bundala, Ngonyani, Ole Saibul, Marwa, Mchafukazi na wengine ambao ni Wazawa na wanalipwa fedha nono, huwa tunajenga chuki na kuanza kuwalaumu kutumia dini, ukabila na hata kuhoji elimu zao.

Badala ya kudai kwa Serikali na Waajiri wetu kuwa viwango vya mishahara yetu havitoshi na ni vidogo kulingana na kazi na ujuzi na hata kukidhi ukali wa maisha, tunawasakama wale wachache ambao wameweza kupata upenyo kuvunja mfumo mbovu wa Kiuchumi na Kiitikadi.

Najua tutaka kujua Mattaka, Idrisa, Kimei, Ndulu na ma CEO wengine wote tujue mishahara yao, ili tupime nini? Ufanisi au ni kulalama bila kuwa na mwelekeo?

Suala la Mrema, kama kuna yaliyosemwa na Mbunge yatathibitika kuwa ni kweli, basi hatua za kinidhamu zichukuliwe. Jiandaeni kuangua kilio mkidai afukuzwe mkakuta kuwa katika mkataba wake wa ajira kuna kipengele cha kulipwa fedha bwelele akifukuzwa kazi!
 
Kishoka,

..huyo Mrema hana muda mrefu kama CEO wa Tanroads.

..lakini hata wakati CEO ni Mghana wachangiaji wa jamii forums walikuwa hawaishi kushutumu upendeleo tanroads.

NB:

..kama ni ukabila mbona kila jamii inaweza kuutumia? there must be something more than ukabila kinachowafanya Wachaga wachomoze kulinganisha na wenzao.

..kuna kipindi niliuliza kwamba Mahakama ya Rufani majaji wanawake watatu kati ya wanne ni kina mama wa kichaga. nikauliza kama ni ukabila.

..jibu nililopata ni kwamba hawa wenzetu wamezingatia sana elimu kwa mtoto wa kike tangu "mwaka 47."

..sasa kuna jamii hapa Tanzania zimebobea ktk kuwaweka ndani watoto wa kike, na kuwacheza ngoma. halafu watu wanalalamika ukabila.
 
Hili swala la tanroads lilikua ni BOmu linalosubiri kulipuka wakati wowote. Sasa hali ni hii.

Yule mghana alipoondoka, Serikali ilitangaza kazi kwenye magazeti ya nafasi ya CEO wa tanroads, then one of the recrutiment firms ikapewa kazi ya kushortlist watu wanaostahili. Cha kushangaza ni kwamba baada ya kushortlist watu na kupeleka majina Wizara ya Miundo mbinu wakajibiwa kwamba hao waliokua shortlisted they are too academic and hawana experience ya mambo ya barabara.

So wizara ikawafuata baadhi ya watu ikawaambia waomba kazi hiyo, mmoja wapo alikua ni profesa mmoja wa engineering, mwingine alikua ni Engineer na ni PHD holder na mwingine alikua ni engineer na PHD holder na wa mwisho alikua ni Bw. Mrema.

Interview ilipofanyika ilionekana Bwana Mrema ndio kashinda, lakini cha kushangaza hata wale walikua kwenye interview panel walihsngazwa na uwezo wa mrema kujibu maswali na kujiamini, kumbe ukweli ni kwamba alikua kashapewa maswali ya interview mapema kabisa so akawa anajua anachoenda kuulizwa ni nini.

Baadae ilikuja kufahamika kwamba huyu jamaa anaurafiki wa karibu sana na Fisadi Chenge. Pia huyu jamaa, imekuja kufahamika kwamba ni kati ya watu waliogawa tenda za TANROADS kwenye mazingira ya kutatanisha kweli mpaka mamlaka ya Usimamizi wa manunuzi PPRA waliandika barua Wizara ya Miundombinu wakiitaka imchukulie hatua kali za kisheria kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya Umma.

Huyu jamaa, pamoja na kutokua na vigezo na kubebwa hadi kufukia hapo alipo ameshaliingizia taifa hasara kubwa kupita kiasi. Mikataba ya ujenzi wa barabara imekua ikipewa wazabuni wenye bei kubwa kabisa kwa lengo la yeye kupata 10%.

Huyu jamaa hafai kabisa, afukuzwa kazi na kufunguliwa kesi ya jinai
 
Hili swala la tanroads lilikua ni BOmu linalosubiri kulipuka wakati wowote. Sasa hali ni hii.

Yule mghana alipoondoka, Serikali ilitangaza kazi kwenye magazeti ya nafasi ya CEO wa tanroads, then one of the recrutiment firms ikapewa kazi ya kushortlist watu wanaostahili. Cha kushangaza ni kwamba baada ya kushortlist watu na kupeleka majina Wizara ya Miundo mbinu wakajibiwa kwamba hao waliokua shortlisted they are too academic and hawana experience ya mambo ya barabara.

So wizara ikawafuata baadhi ya watu ikawaambia waomba kazi hiyo, mmoja wapo alikua ni profesa mmoja wa engineering, mwingine alikua ni Engineer na ni PHD holder na mwingine alikua ni engineer na PHD holder na wa mwisho alikua ni Bw. Mrema.

Interview ilipofanyika ilionekana Bwana Mrema ndio kashinda, lakini cha kushangaza hata wale walikua kwenye interview panel walihsngazwa na uwezo wa mrema kujibu maswali na kujiamini, kumbe ukweli ni kwamba alikua kashapewa maswali ya interview mapema kabisa so akawa anajua anachoenda kuulizwa ni nini.

Baadae ilikuja kufahamika kwamba huyu jamaa anaurafiki wa karibu sana na Fisadi Chenge. Pia huyu jamaa, imekuja kufahamika kwamba ni kati ya watu waliogawa tenda za TANROADS kwenye mazingira ya kutatanisha kweli mpaka mamlaka ya Usimamizi wa manunuzi PPRA waliandika barua Wizara ya Miundombinu wakiitaka imchukulie hatua kali za kisheria kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya Umma.

Huyu jamaa, pamoja na kutokua na vigezo na kubebwa hadi kufukia hapo alipo ameshaliingizia taifa hasara kubwa kupita kiasi. Mikataba ya ujenzi wa barabara imekua ikipewa wazabuni wenye bei kubwa kabisa kwa lengo la yeye kupata 10%.

Huyu jamaa hafai kabisa, afukuzwa kazi na kufunguliwa kesi ya jinai

Mhafidhina,

Kwa hilo la kupewa maswali ya Interview, nitakupinga kwa kitu kimoja. Maswali ya Interview siyo mtihani wa Mock au Form Four.

Kama mtu umeshafanya kazi kwa muda mrefu na kufanya interview nyingi, maswali huwa ni yale yale, from one corner of the wordl to the other.

Mmesema Mrema kafanya kazi kimataifa, je huko alikokuwa si alifanya interview, je ni ugumu gani kujua kuwa anaweza kujibu swali?

Nitakupa mfano, miaka mitatu iliyopita, nilikuwa natafuta kazi nyingine katika shirika ninalofanya kazi. Kwa kipindi cha miezi mitatu, nilifanya zaidi ya interview 20 na masuali pamoja yalikuwa ni kutoka kwa watu tofuati wa idara tofauti na wasiojuana, yalikuwa na common theme.

Ni ujinga na upumbavu mkubwa ambao unapaswa kuepukwa na sisi hasa tunaojiita wasomi kuanza kuropoka kuwa mtu alipewa maswali ya Interview.

Nitakuambia maswali ya msingi ambayo aliulizwa kwenye interview,

1. Tell us about your self
2. Why should we hire you?
3. What can you bring to our company?
4. What is your vision foer this company and its future projects?
5. What are the obstacles of buuilding good roads in Tanzania?
6. How will you handle contracts disputes?
7. How and what ways you will motivate your employees to be efficient, creative and be productive?

Hata kama aliulizwa swali la Kiufundi kama asphalt in chemical composition ngapi, ni upuuzi kutamka na ni aibu kudai eti alipewa pepa!

Na hao ambao walimshangaa Mrema kwa umahiri na kujiamini kwake kunaniambia kuwa hawajui kufanya interview, ni watu biased na zaidi wana poor exposure na wamezoea ku-interview one dimensional candidates. Kama hawajamaa walishangaa na kuzubaa kwa umahiri wa Mrema kujieleza na kujibu maswali, basi tuna tatizo Tanzania na hawa wanaofanya interviews ni wabovu!

Kuongea kwa ufasaha na kujiamini si suala la pepa, ni uwezo wa mtu. Ndio maana nimesema kigezo si Elimu na Vyeti bali ni ufanisi.
 
Mhafidhina,

..kama Chenge[msukuma] ndiyo kamkatia pande Mrema[mchaga] ina maana kilichopo hapo ni uswahiba na siyo ukabila.

..kama ameboronga kazi achukuliwe hatua kama Mrema, siyo kumhukumu kutokana na kabila lake.

Rev.Kishoka,

..kwa kweli sikutaka kwenda huko ulikokwenda.

..tunaambiwa applicants wa awamu ya kwanza walikataliwa kwa kisingizio kuwa walikuwa too academic.

..baada ya hapo wizara ikawafuata Professor wa Engineering, two PhD holders, na Mr.Mrema.
 
Yule mghana alipoondoka, Serikali ilitangaza kazi kwenye magazeti ya nafasi ya CEO wa tanroads, then one of the recrutiment firms ikapewa kazi ya kushortlist watu wanaostahili. Cha kushangaza ni kwamba baada ya kushortlist watu na kupeleka majina Wizara ya Miundo mbinu wakajibiwa kwamba hao waliokua shortlisted they are too academic and hawana experience ya mambo ya barabara.

So wizara ikawafuata baadhi ya watu ikawaambia waomba kazi hiyo, mmoja wapo alikua ni profesa mmoja wa engineering, mwingine alikua ni Engineer na ni PHD holder na mwingine alikua ni engineer na PHD holder na wa mwisho alikua ni Bw. Mrema.

Interview ilipofanyika ilionekana Bwana Mrema ndio kashinda, lakini cha kushangaza hata wale walikua kwenye interview panel walihsngazwa na uwezo wa mrema kujibu maswali na kujiamini, kumbe ukweli ni kwamba alikua kashapewa maswali ya interview mapema kabisa so akawa anajua anachoenda kuulizwa ni nini.

Baadae ilikuja kufahamika kwamba huyu jamaa anaurafiki wa karibu sana na Fisadi Chenge. Pia huyu jamaa, imekuja kufahamika kwamba ni kati ya watu waliogawa tenda za TANROADS kwenye mazingira ya kutatanisha kweli mpaka mamlaka ya Usimamizi wa manunuzi PPRA waliandika barua Wizara ya Miundombinu wakiitaka imchukulie hatua kali za kisheria kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya Umma.

Huyu jamaa, pamoja na kutokua na vigezo na kubebwa hadi kufukia hapo alipo ameshaliingizia taifa hasara kubwa kupita kiasi. Mikataba ya ujenzi wa barabara imekua ikipewa wazabuni wenye bei kubwa kabisa kwa lengo la yeye kupata 10%.

Huyu jamaa hafai kabisa, afukuzwa kazi na kufunguliwa kesi ya jinai

All in all this sounds typical Uswahili na Utanzania. Everything is about hisia na mkiulizwa proof, mnajitafuna vidole.

Nimeuliza very basic questions, lakini kila linalokuja "kumuumbua Mrema" limekaa kinafiki, kizabinazabina na halina ushahidi.

I am not defending Mrema, but I am criticizing the practice of Tanzanians to take advantage of hearsy and personal vendettas to validate arguments.

Je kuna ushahidi kaiba? Unasema ni fisadi na kalitia TANROADS hasara, ni contacts ngapi alizoziidhinisha tangu awe CEO? ni contracts ngapi ambazo alizikuta zimeshasainiwa?

What is his track records? tuleeteeni dataz tuzibanjue na si maneno ya mitaani!
 
Mhafidhina,

..kama Chenge[msukuma] ndiyo kamkatia pande Mrema[mchaga] ina maana kilichopo hapo ni uswahiba na siyo ukabila.

..kama ameboronga kazi achukuliwe hatua kama Mrema, siyo kumhukumu kutokana na kabila lake.

Rev.Kishoka,

..kwa kweli sikutaka kwenda huko ulikokwenda.

..tunaambiwa applicants wa awamu ya kwanza walikataliwa kwa kisingizio kuwa walikuwa too academic.

..baada ya hapo wizara ikawafuata Professor wa Engineering, two PhD holders, na Mr.Mrema.

Joka,

Ndio hilo ninalozungumzia la kutukuza Vyeti. Majority ya Watanzania wanafikiri kuwa the more certificate you have the more efficient and competent you are! nope that is stone age mentality.

Hao Academicians walifeli si kutokana na vyeti, bali hawana kazi hata moja na uwezo kuonyesha kuwa wanaweza kuongoza shirika.

Nimeongelea awali, kwa nini tunafikiri Tanroads ni lazima iwe na CEO ambaye ni Civil Engineer na si Nuclear phycisist, Lawyer au architect?

What matter is if the candidate has an experience in Management and the field itsef.

Kwa wasifu wa Mrema uliowekwa hapa, unaonyesha kuwa yeye kafanay kazi katika mambo ya miundo mbinu na ana shahada si ya Uchumi Ujenzii tuu, bali ni Project Management.

Kuwa na sifa ya Project Management na ukiwa na track record nzuri, ni an excellent reference than PHD in Civil Engineering with no work history than teaching.

Si ajabu hao accademician waliulizwa swali kuwiana na fani zao kama kwa kutumia ujuzi wao wameweza kuzalisha kitu au kujenga kitu kutumia Utaalamu wao, na wakashindwa kujibu swali kutokana na kukosekana na uzoefu au ubunifu.

Same would be said of a PHD ni Law, hoping he could make a great attorney or a judge while the best he can do is read and write the laws but not manouver to represent a client or debate at a negotiating table!
 
..tunaambiwa applicants wa awamu ya kwanza walikataliwa kwa kisingizio kuwa walikuwa too academic.

..baada ya hapo wizara ikawafuata Professor wa Engineering, two PhD holders, na Mr.Mrema.

Ina maana huyo Prof aliyefuatwa yeye siyo academician? Na hao wenye PhD nao hawakuwa academicians?

Hapa naona kuna mchanganyiko wa habari. Mhafidhina unaweza kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu hao ma-Dr wawili na Prof kwamba hawakuwa academicians. Tofauti ya hao wa awamu ya pili na wale wa awamu ya kwanza waliokataliwa ni ipi?
 
Mkurugenzi TANROADS 'amkaba koo' Mbunge

*Ni aliyesema bungeni kuwa Mkurugenzi huyo hana sifa
*Yeye ataka amthibitishie uhalali au ufeki wa vyeti
*Wasifu wake waonesha alivyobobea katika tasnia ya ujenzi


Na Eben-Ezeri Mende

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kasulu, Bw. Kilontsi Mporogomyi (CCM) kumshambulia bungeni Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Bw. Ephraem Mrema, akidai hana sifa za kushika wadhifa huo, Mkurugenzi huyo ameibuka akimtaka athibitishe madai hayo.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Bw. Mrema alisema hawezi kujitetea kuwa vyeti vyake ni halali au bandia, ila anachohitaji ni Mbunge huyo kuthibitisha tuhuma hizo.

"Mimi nilikuwa bungeni jana (juzi) na sikusikia kwamba nilikuwa natakiwa kujibu tuhuma zozote za kuwapo katika ngazi niliyopo kwa kutumia vyeti feki. Kama kuna uthibitisho wa hilo, Bw. Mporogomyi athibitishe," alisema Bw. Mrema.

Akichangia makadirio na matumizi ya Wizara Miundombinu juzi, Bw. Mporogomyi alisema Mkurugenzi huyo alipaswa kuwa na sifa ya Uhandisi ambapo yeye (Bw. Mrema) si Mhandisi bali ana Shahada ya Usimamizi wa Miradi aliyoipata mwaka 1987.

Aliwataja waliostahili kushika nafasi hiyo kutokana na kuwa na sifa hizo kuwa ni Bw. Boniface Nyiti, Bw. Venance Ndyamukama na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Bw. Chacha.

Alilalamika, kwamba Bw. Mrema analipwa fedha nyingi kana kwamba ni mgeni kutoka nje ya nchi. Alitaja viwango hivyo kuwa ni mshahara wa mwezi dola 8,500 za Marekani, posho ya nyumba dola 2,200, pensheni dola 850, usafiri dola 500, bonasi kwa mwaka dola 102,000, likizo ya mwaka dola 3,000 na mwisho wa mkataba atalipwa dola 10,000 pia anapopanda daraja anapewa dola 150 kwa siku mara siku 60.

Alisema baada ya Bw. Mrema kuchukua nafasi hiyo, waliokuwa wakistahili kuipata, walitimuliwa na kurudi wizarani, baada ya kuonekana tishio kwake, lakini wizara pia iliwarudisha kwake ili wawe mameneja wa mikoa, jambo lililoshindikana kutokana na nafasi hizo kuwa na watu.

Hata hivyo, alisema wafanyakazi hao bado wapo na hawana idara yoyote wanayofanyia kazi, lakini wanaendelea kulipwa zaidi ya sh. milioni mbili kwa mwezi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Bw. Mrema mwaka 1983 alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Ukadiriaji wa Majenzi katika Chuo Kikuu cha Westminster, London, Uingereza na mwaka 1987 alipata Shahada ya Uzamili katika Utawala na Maendeleo ya Miradi katika Chuo Kikuu cha South Bank, London, Uingereza.

Mwaka huo huo, Bw. Mrema alihitimu Mafunzo ya Juu ya Taasisi ya Wakadiriaji Majenzi ya Uingereza inayotoa utambulisho wa kimataifa wa Ukadiriaji Majenzi (Chartered Quantity Surveyor).

Kati ya mwaka 1983 na 1985, Mkadiriaji wa Majenzi Mwandamizi Greater London Council. Kuanzia mwaka 1985 hadi 1987 alikuwa Mkadiriaji Majenzi Mwandamizi London Borough of Lambeth. Kati ya 1987 na 1993, alikuwa Mkadiriaji wa Majenzi Mkuu London Borough of Haringey.

Kati ya mwaka 1993 na 1996 alikuwa Mshauri katika kampuni ya Broadwater Association Ltd ya Tottenham, Meneja wa Mradi Kampuni ya Genstates Limited na baadaye Mkuu wa Ukadiriaji Majenzi katika kampuni ya Pacific Construction ya London.

Kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2002, alikuwa Mtaalamu Mwandamizi wa Ununuzi katika Ofisi ya Rais na kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2005 alijiunga na Kampuni ya Ujenzi ya Konoike akiwa Meneja Mradi na Mshauri wa Ufundi.

Baada ya hapo kati ya mwaka 2005 na mwaka juzi aliajiriwa kuwa Mshauri wa Ufundi katika Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kuanzia Septemba mwaka juzi alikuwa Mshauri wa Benki ya Dunia kabla ya kujiunga na TANROADS.


Source: Majira
 
Katika Tanzania si jambo la ajabu kabisa mtu kupewa madaraka katika fani asiyosomea. Mnakumbuka tulikuwa na Sarungi kama waziri wa ulinzi wakati ni doctor wa mifupa?. Huyu Mrema walahi kaisomea fani hiyo na kuifanyia kazi kwa muda fulani, sioni ubaya katika hilo la yeye kuwa CEO.

Kuhusu issue ya mishahara hapangi yeye bali anapangiwa na bodi ambayo inajumuisha watu wengi na isitoshe huenda hata yeye kakuta mishahara hiyo imeshapangwa, sasa yeye afanye nini?

Jamani kuwa rafiki na Lowasa ni kosa?. Lowasa ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Amesoma na watu, ameenda jeshini na watu, amefanya kazi na watu. Na hakuna binadamu aliye kamili 100%, hivyo Lowasa kama binadamu amefanya makosa kwa hili la Richmond na amewajibika ili uchunguzi uendelee kufanywa vizuri. Kwa hili pia sioni sababu ya kumsakama Mrema kuwa rafiki wa Lowasa. Binadamu yeyote anayo haki na uhuru kujichagulia marafiki hivyo kwa hilo sioni ubaya kabisa.

Suala la Mrema kuwa CEO kwa kupitia mlango wa nyuma nadhani ingekuwa ni vyema na busara tukaletewa ushaidi kwa hili kabla ya kuanza kulichambua. Hivyo mwenye ushaidi tafadhali alete hapa kwani hiki kijiwe tuko huru kuchambua mambo bila woga.

Suala la kunyanyasa wafanyakazi si zuri hata kidogo na kama ni kweli huyu Mrema alifanya na anafanya na kama ushaidi upo basi hakuna haja ya kupoteza muda bali ni kumchukulia hatua za kisheria mara moja.
 
Mim naona hapa suala la kujadili ni performance yake na sio mshahara.
Tujiulize je utendaji wake wa kazi unaendana na kiwango cha malipo ya mshahara??
Tuhuma dhidi yake ya kunyasa wafanya kazi uchunguzi ufanyike kama ni kweli basi achukuliwe hatua zinazostaili,pia uchunguzi ufanyike kuona kama ni kweli aliajiriwa kwa kushikwa mkono
 
wakuu nimesoma thread hii tangu mwanzo hadi mwisho, naomba kuwasilisha kwenu
1.0 kama bwana mrema ni mla rushwa hatufai, na awajibike kwa hilo. hili nalo linahitahi ushahidi pasipo shaka, kwa kuwa tuhuma za mbunge zimekaa kimawenge mawenge. inawezekana mbunge anatumiwa na wale walioikosa hiyo nafasi

2.kuhusu sifa za mrema, hilo liko wazi, yeye ni mmoja wa watu wenye taalumua adimu yaani chartered quantity surveyor, hapa nchini nadhani chartred quantity surveyor ni wawili tu, kama wameongezeka ni kwa miaka hii mitatu ya mwisho, mwingine ninayemfahamu ni mtu mmoja anaitwa frank kanza, yeye ameajiriwa na noremco norway. quantity surveyor ni moja ya taalumu tatu za ujenzi, yaani engineer, architect, na yeye mwenyewe, ninavyofahanu na nitaleta hapa jf, quantity surveyors all over the world are construction managers, or project managers, nchi kama kenya kuna chief government quantity surveyor. yeye ndo mtaalamu namba moja wa mikataba yote ya ujenzi. bcoz, he is professionally rich, in procurement, arbitration, construction cost, construction management etc.

3. nafasi ya ceo wa tanroads, ilitangazwa kimataifa, na ushindani ulikuwa mkubwa sana. waliotajwa na mbunge walikuwa wahandisi wa muda mrefu hapo wizarani, boniface nyiti alikuwa regional engineer muda mrefu kilimanjaro. yeye ndo alituangusha sana, kwani yeye na nalaila kiula walihujumu kabisa mradi wa 2bn mwaka 1989!wa kujenga zile barabara za vijijini, wakampa kazi ile fisadi becco, mradi ule ni hadithi ndefu. usaid/world bank ndo walikuwa wafadhili na walichukia sana. kama kuna mtu wa world bank alikuwa kwenye intavyuu bwana nyiti asingepita. ndyamukama wengi mnamfamu, amekuwa meneja wa tanroads hapa dsm kwa kipindi kirefu sana na mnajua utendaji wake ulivyokuwa wa kusua

ni wazi kuwa mbunge ametumiwa na hawa walikokosa hii nafasi. kule tanroads wanamwona mrema kuwa ni wa kuja, kumpiga vita wanatumia vigezo vya kikabila, kitaaluma lakini ukweli uko wazi

ninajua tanznia institute of quantity surveyor, ardhi university wanajadili jambo hili na huenda muda si mrefu watatoa tamko kuhusu vita hii. tulisubiri

nawakumbusha kuwa, 1980, aliyekuwa waziri mkuu alienda ulaya kutafuta msaada, namna ya kuwa na wataalamu ambao wangeweza kuliokoa taifa kutokana na cost kubwa za ujenzi, kwa kusimamia scarse resources tulizo nazo ili kupata product nzuri, waingereza wakamsaidia kuanzisha idara ya consttruction economics pale uclas. nia ilikuwa ni kupata quantity surveyors wa kutosha kila wilaya, kudhibiti tender collusions, tender inflatiosn, contracts na kadhalika.

hata hivyo, kuna vita kati ya wahandisi ambo wengi wamejiunga na wanasiasa dhidi ya watu hawa

ahsanteni.
 
Ile kuwa karibu na Lowassa/Chenge tayari Mrema kanuka na halina ubishi, lakini bado kuna mambo muhimu yawekwe hadharani, je tangazo la kutafuta CEO lilitaka qualifications zipi?ni akinanani walisimamia hiyo enterview? je wakati huo waziri wa miundo mbinu alikuwa nani? na waziri mkuu alikuwa nani?
 
Back
Top Bottom