Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Mitihani ni LUGHA, MAARIFA na HISABATI. Hisabati hakuna swali la kuchagua hata moja.

Kitu ambacho sikukielewa wakati huo hata leo ni neno SAYANSI KIMU. Huenda hata ww unaesoma hapa hukijui.
Hii ilikuwa ni sayansi ya kujikimu. Kukufundisha mbinu mbali mbali za kumudu harakati za maisha ya kila siku.

Nilijifunza kunyoosha, kupika ubwabwa .. Kuchemsha maji ya kunywa.. Hili somo linapaswa kurejeshwa mashuleni.. Hapa ndipo ustaarabu unapofundishwa.
 
Duh umenikumbusha shule yetu tulikuwaga tunaimba kwaya majigambo ngojera soga nyimbo za mabata wadogo wadogo wanaogelea,sizitaki mbichi hizi,sadiki na chitemo uvivu wangu nyumbani nikiwa hapa njiani nakufa hapa kwanini dah haya mambo hayapo sasa watoto kila kukicha wanawehuka Mara kucheza chura,sijui kamatia chini mungu saidia serikali angalia hila rudisha michezo shuleni na elimu ya ujamaa na uzalendo wa taifa
 
Hili somo tulikua tunafundishwa mpaka jinsi ya kupiga mswaki.
Kuna hili somo ..na somo la Siasa na Uraia lilifutwa miaka ya tisini katikati.. Nimekuja kugundua yalikuwa masomo muhimu sana..

Sasa hv uongozi Wa serikali unalalamika vijana sio wazalendo na sio RAIA wema.. Wakati hawajafundishwa kuwa RAIA wema.. Warudishe haya masomo.
 
Nimewahi kuwa mwalimu shule moja ya sekondari eti hawajui mwimbo wa taifa, mwimbo wa Tanzania Tanzania niaibu watato akili zao zipo kwenye kubeti tu
 
Hapo No 6, kuna pichu zilikua zinaitwa VIP na viatu vya safari buti na hivyo vya ngozi ya mbwa jina limenitoka, goshiii. kweli ya kale ni dhahabu aise; mkuu umenikumbusha mbali sana.
 
Yani enzi hizo kulikuaga na wanafunzi wale maskauti ,walikua wanakula mazoez kama wajeda tena maporini huko
 
Hiyo No:10 inaelekea ni enzi za karibuni kama mlikuwa mnavaa suruali shuleni Ifunda Tech. pamoja na baridi yote ile tulikuwa tunavaa kaptula enzi zetu 197...
 
Back
Top Bottom