Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Na ni kawaida sana wakati wa mapunziko na chakula kucheza mpira kushindana madarasa, Hii pia ilihusisha kunyang'anyana mpira kwa mitaa wakati wa kwenda nyumbani

Mtaa ukizidiwa mtajikuta mko mtaa wa pili bila kupenda
 
Nakumbuka tulikua tunachukua Atlas na kutafuta ramani mojawapo kisha tunacheza mchezo wa kutafuta,

Yaani unachagua jina la nchi au mji kwenye hiyo ramani kisha umamwambia mwenzio;

"Nionyeshe mji fulani uko wapi?"

Hii ilitujenga sana kujua miji na nchi za dunia nzima,
Kitambo sana.
 
Nakumbuka tulikua tumachukua Atlas na kutafuta ramani mojawapo kisha tunacheza mchezo wa kutafuta,yaani unachagua jina la nchi au mji kwenye hiyo ramani kisha umamwambia mwenzio "nionyeshe mji fulani uko wapi?" Hii ilitujenga sana kujua miji na nchi za dunia nzima,kitambo sana.
Enzi hizo shule ilikuwa shule kweli.
 
Enzi zetu pepa la la 7 ilikuwa siku 1 masomo yote ma3! Maswali 50 kila somo. Shuleni kwetu aliepata 124 over 150 alienda Mzumbe... nilipata 119 over 150, nikabaki shule ya pale wilayani kwetu. Iliniuma balaa
 
Enzi zetu mwalimu wa hesabu akiingia lazima kuimba orodha ya kuzidisha yote, tulikuwa tunaiita 'hesabu za mara' sasa usiombe ikakukuta ya saba, ingawa kuliwa na wenye uwezo wa kuitandika yote bila hata kusita, hawa walikaa madawati ya mbele siku zote.
Ya 7, 8, 9 na 12 zilikuwa za moto sana "table zake"[emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Back
Top Bottom