Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Kuna mwalimu alikuwa anatufundisha tebo wakati tuko darasa la 2. Ukikosea unapigwa na kufinywa. Kabla ya kujaribiwa uwezo wako wa tebo, uliitwa mbele ya darasa na kuombwa kuanza kuimba tebo moja moja - ya kwanza hadi ya 12. Kipigo kilipozidi, tukagundua mbinu. Tukaandika tebo ngumu ngumu kwenye sakafu. Tukifika kwenye tebo ngumu, tunapiga chabo kwenye sakafu. Mwalimu hakuwahi kugundua.
 
Ilikua ni kawaida kucheza mpira na nguo zako za Shule halafu kesho yake hizo hizo nguo unaingia nazo darasani bila kuzifua!
Kwel kabsa,kwenye mechi wengne wanavua wengne mashat meupe.Mwl D.kawa alpenda kutuita weusi ksa kuna weupe( mashat na tuliovua ndo weusi)
 
17. Kwenda shule na kidumu cha maji na mzigo wa kuni

18. Kufagia choo na darasa kwa zamu

19. Kupewa kiunga na mti wa kuumwagilia

20. ukaguzi wa usafi kila Jumatatu na Jumatano

21. Mtihani wa mwisho wa darasa la saba walimu wanoko na monta lazima achezee makofi.

22. kuweka kioo chini ya sketi za wanawake ujue kavaa chupi ya rangi gani

23...
 
Enzi zetu mwalimu wa hesabu akiingia lazima kuimba orodha ya kuzidisha yote, tulikuwa tunaiita 'hesabu za mara' sasa usiombe ikakukuta ya saba, ingawa kuliwa na wenye uwezo wa kuitandika yote bila hata kusita, hawa walikaa madawati ya mbele siku zote.
Hapo namkumbuka Mwl M.maugo drs la NNE alkuwa na kauli mbiu operation table&watoro. Anakuja na bakora kumi mkononi akiondoka hana hata moja.alkuwa anasurubu balaa,ngoma table ya 9 ilkuwa inanipa san majeraha.1988
 
Nakumbuka tulikua tunachukua Atlas na kutafuta ramani mojawapo kisha tunacheza mchezo wa kutafuta,

Yaani unachagua jina la nchi au mji kwenye hiyo ramani kisha umamwambia mwenzio;

"Nionyeshe mji fulani uko wapi?"

Hii ilitujenga sana kujua miji na nchi za dunia nzima,
Kitambo sana.
Km tulkuwa wote,unanikumbusha michezo ya drs la 5. Mji wa antananalvo ulnitesa sana kuutafuta hadi Leo nakumbuja,nililazmika kuazma Atlas ckulala hadi nlpo upata.( Madagascar)
 
Enzi zetu shule za mjini walifanya mitihani ya MOCK, kijijini tulifanya MITIHANI YA KATA.
Huo mtihan wa mock kuuckia Mara ya kwanza walim wakiuongelea ilkuwa umitashumta kufika shulen nikawambia wenzang mwez wa saba kuna mtihani wa moka.wakanishangaa kumbe moka ni viatu. Wala haukuja zaidi ya kupga pepa ya kata.kumbe walfanya watoto wa town... Duh tumetoka mbali.MTU anakuwa wa kwanza ktk kata national ikja hayumo!!!!
 
Kuna shule ya msingi moja ilikuwa kazi ni kuwatumikisha wanafunzi kama vibarua katika mashamba ya wanakijiji. Mwanzoni tulikuwa tunakwenda huko mashambani kulima mchana/jioni baada ya masomo. Baada ya hela kukolea, kukaanza kwenda saa za asubuhi. Kuna wakati tulikuwa tunaambiwa kuwa kesho asubuhi msije shuleni hapa, tuonane kwenye shamba la mzee fulani ambalo liko sehemu fulani na majembe yenu.
Hatari hii.
 
Kukimbia mchaka mchaka kila saa 12:30 asubuhi ole wako uchelewe utakiona cha moto
 
Daaah! nimekumbuka mbali sana nimeishia kucheka,darasani hatukua na saa tuliweka alama ya kivuli cha bati kwamba kivuli kikiwa hapa basi ni break time mnajianda kusikia kengere unakimbia nyumbani kuwahi kiporo cha jana halafu unarudi shule
Maisha hayakua na classes tulipendana sana,waliosoma kipindi hicho tunaita shule za kulipia ni wale vilaza waliofail std 7
Hiyo ya kivuli cha bati namkumbuka mashimba William yy alkuwa anaenda kugonga kengele bila kuwa na SAA mlad kivul kmefika 12:20 kumbe majra hubadlka kla baada ya miez 3. Kuna cku algonga SAA 5 tukatoka nje talyo jiri Mwl wa zamu anakumbuka...ilkuwa soo
 
17. Kwenda shule na kidumu cha maji na mzigo wa kuni

18. Kufagia choo na darasa kwa zamu

19. Kupewa kiunga na mti wa kuumwagilia

20. ukaguzi wa usafi kila Jumatatu na Jumatano

21. Mtihani wa mwisho wa darasa la saba walimu wanoko na monta lazima achezee makofi.

22. kuweka kioo chini ya sketi za wanawake ujue kavaa chupi ya rangi gani

23...
Kula like zangu mkuu
 
Baada ya kuhitim ly wiki lnalofata unapta shulen w/ funzi wakiwa mctalin Mara "nyuma geuka,heshma kwa mkuu toa".......
 
Ahahahahhaaa Kama kuna bingwa wa kuibia majibu ya hesabu na Mimi nilikuwa mmoja wao, yaani hata Kama upo desk la tatu ukiandika namba ya swali kule Mimi najua namba ngapi wewe umiza kichwa hapo Mimi nasubiri jibu na nitaandika jibu kama lako, Kuna siku tulipata wawili tu yule jamaa bingwa wa hesabu na Mimi, ila Mimi jibu Lina utata halina njia ikabidi niitwe nikaonyeshe njia ubaoni niliyofanya hadi nikapata jibu darasa zima wakaguna, nilipewa chaki sijui hata nianzie wapi, watoto walicheka kweli darasani, maana walijua mchezo wangu nikachapwa yakaisha
 
Nakumbuka kuna mwaka drs la 5-7 tulienda council kufata madaftar tukaambiwa kla MTU abebe 40.wachache wanaojielewa wale wa ly walzidisha no.maana ilkuwa ni mwendo wa kuchapa lapa.Pta popote mlad ukfka shule we kabiz 40.nlkuwa drs niljilaum sana maana baadae tulianza kuuziwa na jamaa walo chimbia madaftar majumban.kwa vle wako karbu wote walkuwa wamekomaa walbeba had 70/80
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom