Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,841
Reaction score
7,756
Habari wadau wa JF.

Enzi zetu bwana mambo yalikuwa tofauti kabisa na zama hizi. Ngoja niwamegee kidogo na ninyi mwongeze mambo yenu enzi zenu.

1. Ulikuwa ukienda kuandikishwa darasa la kwanza unaambiwa uzungushe mkono kichwani ushike sikio kupima umri wako. Ukishindwa kufikia sikio subiri mwakani.

2.Shuleni tuliimba nyimbo za kizalendo na kusifia viongozi wa chama na serikali.

3. Hatumalizi mwaka bila mwana mazengaombwe kuja kutoa burudani na viini macho.

4. Kuadhibiwa na mzazi asiye wako ni kawaida sana.

5. Maswali ya mitihani ni migumu kuanzia msingi hadi secondary. Ni vigumu kupata jibu kama kichwa kigumu. Saivi daaaaaahhhhh.

6. Viatu vyetu na chupi zote sawa hakuna mjanja. Wote sare mfano viatu vya mbwa na gogo.

7. Ukimaliza shule ya Msingi au sekondari yani wewe ni mtu mzima haswa. Unaweza hata kuoa.

8. Viongozi wa serikali wakipita tulikatiza vipindi kupanga foleni pembeni ya barabara ili kuwapungia mikono.

9. Elimu ya kujitegemea hatukuwa nyuma shuleni. Yaani EK.

10. Ukimaliza shule huoni aibu kuvaa sare zako za shule nyumbani. Mfano kaptula au suruali.

11. Popote uendapo hata weekend hukosi kitabu mkononi au mfukoni.

12. Msomi utamjua kwa kuchomeka kalamu kwenye mfuko wa shati.

13. Hakuna idadi ya viboko vya kumchapa mwanafunzi.

14. Umande na mvua ni kawaida sana hasa wakati wa kuisaka elimu ya Msingi.

15. Kufanya kazi kwenye mashamba na majumba ya walimu ni mambo ya kawaida sana.

16. Kila mzazi alipenda mtoto wake aishi kwa mwalimu.

17.................endelea
 
Enzi zetu kila mkitoka shule, mnazunguka nyuma ya shule kushuhudia ngumi, hizi ngumi huwa ni kwa zamu,zamu yako ikifika siku hiyo utazichapa tu na atayechaguliwa!
 
Habari wadau wa JF.

Enzi zetu bwana mambo yalikuwa tofauti kabisa na zama hizi. Ngoja niwamegee kidogo na ninyi mwongeze mambo yenu enzi zenu.

1. Ulikuwa ukienda kuandikishwa darasa la kwanza unaambiwa uzungushe mkono kichwani ushike sikio kupima umri wako. Ukishindwa kufikia sikio subiri mwakani.

2.Shuleni tuliimba nyimbo za kizalendo na kusifia viongozi wa chama na serikali.

3. Hatumalizi mwaka bila mwana mazengaombwe kuja kutoa burudani na viini macho.

4. Kuadhibiwa na mzazi asiye wako ni kawaida sana.

5. Maswali ya mitihani ni migumu kuanzia msingi hadi secondary. Ni vigumu kupata jibu kama kichwa kigumu. Saivi daaaaaahhhhh.

6. Viatu vyetu na chupi zote sawa hakuna mjanja. Wote sare mfano viatu vya mbwa na gogo.

7. Ukimaliza shule ya Msingi au sekondari yani wewe ni mtu mzima haswa. Unaweza hata kuoa.

8. Viongozi wa serikali wakipita tulikatiza vipindi kupanga foleni pembeni ya barabara ili kuwapungia mikono.

9. Elimu ya kujitegemea hatukuwa nyuma shuleni. Yaani EK.

10. Ukimaliza shule huoni aibu kuvaa sare zako za shule nyumbani. Mfano kaptula au suruali.

11. Popote uendapo hata weekend hukosi kitabu mkononi au mfukoni.

12. Msomi utamjua kwa kuchomeka kalamu kwenye mfuko wa shati.

13. Hakuna idadi ya viboko vya kumchapa mwanafunzi.

14. Umande na mvua ni kawaida sana hasa wakati wa kuisaka elimu ya Msingi.

15. Kufanya kazi kwenye mashamba na majumba ya walimu ni mambo ya kawaida sana.

16. Kila mzazi alipenda mtoto wake aishi kwa mwalimu.

17.................endelea
Enzi zetu mwalimu wa hesabu akiingia lazima kuimba orodha ya kuzidisha yote, tulikuwa tunaiita 'hesabu za mara' sasa usiombe ikakukuta ya saba, ingawa kuliwa na wenye uwezo wa kuitandika yote bila hata kusita, hawa walikaa madawati ya mbele siku zote.
 
Hahahahahaha! Namkumbuka Mwalimu Wangu Chief Essau Kashiki 1977 Hesabu Za Kichwa Anatoa Maswali Akiwa Nje Darasa Zima Mfanye Kazi Yake Mara Au Table Unaambiwa Imba Kashehe Table Ya 7 Na 9 Mwalimu Taita Hesabu Za Kushitukiza Duuh! Mbali Sana Siku Ya Kufunga Shule Ilikuwa Inaitwa Siku Ya Kuagana Zinapigwa Ngumi Mwanzo Mwisho
 
Mtoro ASIYEPENDA masomo HUISHIA NYUMA ya madarassa,,, huku madaftari kaweka MFUKO WA NYUMA,, huku akiwa na KANDAMBILI ZA MGOGO,,,, pia SIKU YA KJUFUNGA SHULE kuna wanaokuja na MABUTI YA MGAMBO,, mbele NONDO kuwatafuta wabaya wao,, au YAI VIZA kwa ajili ya MWALIMU MKUDA,,,, PIa MWANAFUNZI Mwenye akili ndy anapendwa na waalimu
 
Back
Top Bottom