Enzi zetu bwana!! Mambo yalikuwa hivi...

Tukiwa Ndiyo Tunatoka Darasa 6 Kwenda La Saba Kuna Jinga Lisilojulikana Likaandika SISI DARASA LA SITA TUKO MBIONI KUINGIA DARASA LA SABA TUNA MGOMO BARIDI KWA HERI 1977 KARIBU 1978 Aisee Tulikula Fimbo
Huu sio uhenga ni zaidi yake.
Huu mwaka mama yangu ndo kamaliza teacher's college anaanza kazi serikali ya Nyerere.
Salute!
 
>Soksi za pundamilia
>Mchakamchaka
>Kipindi cha mitihani mnatoka nje ili kumpisha mwalim aandike mtihani ubaoni
>Kipindi chakufunga basi lazima ngumi zipigwe ( ntafunga shule na wewe)
>Darasani mkifaulu kwenda ngazi ingine ya elim basi 10 ni wengi sana.
>Rula/mkebe tunanunua kipindi cha mtihani hasa ile yakuvuka ngazi ya elimu
>Walimu walikuwa wanaheshimika sana
>Ukifaulu kwenda sekondari basi utaona wewe ndio wewe.
>Kutoka na uhaba wa vyombo vya habar unaweza kwenda shuleni mkajikuta watano kumbe siku iyo hakuna shule(likizo/dharula nk) hii watoro ndio sanasana.
>Kampula zilizotoboka unavaa na kipensi ndani.
>Kuna waliokuwa wananuka mikojo.
Kula like zangu mkuu
 
Nilikuwa mpandisha bendera kisa nilijiunga scauti.. Na scauti hakaguliwi usafi anaheshimika hatari
 
Back
Top Bottom