Enzi za Jambazi anaitwa "Kitenga" mkoani Morogoro, miaka ya 93

kidereko

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
882
1,254
Wakuu ,

Kuna miaka morogoro Kuna Jambazi alisumbua alikuwa anaitwa Kitenga, nakumbuka alipokufa watu walikusanyika pale mortuary ya hospitali ya mkoa kwenda kumshuhudia kama ni yeye au la.

Mwenye kukumbuka historia yake atumegee kidogo, japo me nilishuhudia maiti yake, but sikumbuki matukio yake kwa sana
 
Aloo, hata mimi nilipata kumsikia huyo jambazi.

Kuna habari moja nilipata kuhadithiwa kumuhusu yeye na matukio yake ya ujambazi, eti inasemwa alikuwa na uwezo wa ajabu, alikuwa anaweza kukimbizwa na watu au polisi na mara akiwaacha wanaomkimbiza na akipinda kona na hao wanaomkimbiza wakipinda kona basi huwamuoni yeye bali watamuona Bibi kizee anatembea taratibu tu na wanapomuuliza huyo Bibi kizee (wakidhani kwamba sio kitenga) huyo Bibi huwajibu; "ndio nimemuona mtu mmoja kanipita hapa mbio"---- kumbe ndiye yeye mwenyewe Kitenga, na hapo anakuwa kasalimika.

Majambazi wanayo mauzauza mengi.🤣
 
Aloo, hata mimi nilipata kumsikia huyo jambazi.

Kuna habari moja nilipata kuhadithiwa kumuhusu yeye na matukio yake ya ujambazi, eti inasemwa alikuwa na uwezo wa ajabu, alikuwa anaweza kukimbizwa na watu au polisi na mara akiwaacha wanaomkimbiza na akapinda kona na hao wanaomkiza wakipinda kona basi huwamuoni yeye bali watamuona Bibi kizee anatembea taratibu tu na wanapomuuliza huyo Bibi kizee (wakidhani kwamba sio kitenga) huyo Bibi huwajibu; "ndio nimemuona mtu mmoja kanipita hapa mbio"---- kumbe ndiye yeye mwenyewe Kitenga, na hapo anakuwa kasalimika. Majambazi wanayo mauzauza mengi.🤣
exactly, historia yake ipo ivyo mkuu, nakumbuka mwinyi alishawai kumpa trekta sijui ili aachane na ujambazi ilisemekana
 
Kwenye daraja la shani cinema ukiwa unatoka town mkono wa kulia kuna mondo imepinda tulipo kua wadogo tulikua tunaenda kuangalia,wanasema lile tundu ni risasi,ilitakiwa apigwe kitenga,akarukia MTO Morogoro..Pia kuna ndanje
Hiyo ghasia nakumbuka ilianzia kipindi stendi ya mabasi ya mikoani ilikuwa mjini kati karibu na hilo daraja walitaka kumpora mfanyabiashara aliyekuwa kwenye basi la abood,ambush na polisi ndo ikaanzia hapo..
 
Back
Top Bottom