Enzi za "break dance" in the 80s Avalon, Empress, Empire cinema

Hukumuzuku

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
6,684
5,034
Enzi hizo kulikuwa marufuku kuendesha magari jumapili, na usafiri wa kutegemea ulikuwa ni UDA (daladala ndiyo kwanza zilianza kuruhusiwa).

Video (au VHS) ilikuwa nadra sana na kwa wenye pesa tu kama Wahindi, Waarabu na watoto wa vigogo serikalini wenye address O'bay, Mikocheni, Msasani n.k.

Kila Jumapili kulikuwa na foleni kali kabla ya movies kwenye majumba ya Cinema kama Empire, Empress, Avalon, Odeon na "ulanguzi" wa tiketi haswa kwa movie za "X-rated".

Damn, hata movie za kihindi za Amitabh Bhachan, Mithun Chakraborty et al nilipanga foleni kuangalia, kwa vile tu zilikuwa "must see" kwa walizoziona na kuhadithia mwanzo hadi mwisho kila jumatatu darasani shule ya msingi enzi hizo.

 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka tulikuwa tuna enda pale Empire Cinema kuazima VHS zenye taharifa za habari weekly toka CNN.
 
Mi nakumbuka tulikuwa na membership pale Empire. Kila Ijumaa tunaenda kuazima movie kadhaa za weekend.
 
That was the best time which will never come back.Maana hakukuwa na mijizi(mafisadi)kama ilivyo leo hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom