Kumbi za Sinema Dar es Salaam enzi hizo

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,133
tukumbushane zamani kidogo,dsm kukikuwa na kumbi za cinema kama,empress,empire,newchox,avalon,cameo,odeon na drive in,,empress ndo ulikuwa ukumbi wa wajanja,hasa watoto wa ilala,kila jmosi kulikuwa na movie ya usiku mpaka asubuhi,watoto wa mtaani(changudoa)walikuwa wanajaa sana,cameo na odeon zilikuwa za wadosi,avalon na newchox ilikuwa mixer,na drive in,linajieleza lenyewe,,cijui wewe inakukumbusha nini?
 
Nakumbuka tulikuwa tukitoka ukonga tunashuka kongo na mchikichini kisha tunatembea kwa mguu hadi empire ndio ulikuwa ukumbi wangu na nilikuwa nakaa seat za staff .Jamaa walikuwa wanashangilia movie utafikiri ni mpirani. Kipindi hicho hakuna hata station moja ya Luninga kwa Tanzania bara
 
Drive in cinema,,mwisho wakuangalia snema wanamuweka maiko Jackson lile goma lake la threlar,,,full kucheza.

,,,Marehemu shehe yahaya Hussein akiweka TV kuubwa nje pale kwake kinondoni garden karibu na shule ya msingi,,,mnatazama ndondi za Muhammed ally,,YAKALE DHAHABU,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
tukumbushane zamani kidogo,dsm kukikuwa na kumbi za cinema kama,empress,empire,newchox,avalon,cameo,odeon na drive in,,empress ndo ulikuwa ukumbi wa wajanja,hasa watoto wa ilala,kila jmosi kulikuwa na movie ya usiku mpaka asubuhi,watoto wa mtaani(changudoa)walikuwa wanajaa sana,cameo na odeon zilikuwa za wadosi,avalon na newchox ilikuwa mixer,na drive in,linajieleza lenyewe,,cijui wewe inakukumbusha nini?
Avalon used to be my favorite seconded by Empress, nimekumbuka mengi ya utotoni.
Drive in ilikuwa ya kifamilia zaidi.
 
Mku kuna ukumbi upo hapo maeneo ya mnazimmoja haujautaja
Bila Shaka utakuwa unazungumzia Star Light.

Enzi hizo kumbi zangu pendwa zilikuwa Empire, Avalon, Drive In.
Sinema kali za enzi hizo zikiwa:
-Disco Dance ...Gourang Chakraborty aka Mithun akicheza kama Jimmy.
-Shaheshah....Amitabh Bachchan.
-Kaalia....Amitabh B
-Naseeb...Amitabh B
-Muqaddar Ka Sikandar...Amitabh B
-Anand...Amitabh B
-Agneepath ...Amitabh B akishirikiana na Mithun C.
-Deewar...Amitabh B.
-Andhaa Kaanoon...Amitabh B, Hema Malin

-Warbus...Romano Kristoff
-Commando....Arnold Shwarzenegger akicheza kama John Matrix.
-Enter the Dragon...Bruce Lee, JIm Kelly, John Saxon.

Dah enzi hizo zilikuwa tamu sana wallah. Hatukuwa na stress za kipuuzi. Maisha yalikuwa murua kabisaaaaa.
Wakati huo mnaangalia movie kama mpira...yaani ikifika katikati kunakuwa na mapuzmiko movie linazimwa wadau mnaenda kuchimba dawa na kununua viburudisho (Cheuro, tambi, kacholi, bagia na soda) halafu mnarudi kuendelea na muvi.
 
Nakumbuka baba alikuwa anatupeleka Drive inn kila J2 ya mwisho wa mwezi.
 
Kuna movie nazikumbuka kama:
1.KILL SQUAD
2.ENTER THE NINJA
3.WAR BUS
4.DEATH BEFORE DISHONOUR
5.AMERICAN NINJA
6.BLOOD SPORT
7.NO RETREAT NO SURRENDER
Na nyingine nyingi tu za action.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naongezea No.8.IN THE LINE OF DUTY PART 4.Nakumbuka hekaheka za kugombea ticket Empire Cinema,hizo movie zote hapo juu na nyinginezo zikiingia nilikuwa zinaanzia Empire..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Movie nyingine iliyokuwa kali ni RULES OF ENGAGEMENT ya Samuel Jackson aliyekuwa Kamanda wa Kikosini cha Marekani kilichokwenda Yemen kumuokoa aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Yemen,infact walifanikiwa kwa hilo lakini walipata upinzani kutoka vikundi vya kigaidi vilivyopinga Majeshi ya Marekani kuingia nchini mwao.Vikundi hivyo vilishambulia jengo la ubalozi wa Marekani na kuchoma moto bendera ya Marekani, lakini kikosi hicho mahiri cha Marekani kilifanikiwa kumuokoa Balozi wao,na baada ya Kamanda Samuel Jackson kuona hali ile aliamuru kikosi chake kufungulia mapigo dhidi ya vile vikundi ambapo madhara yalikuwa makubwa wale combatants na raia ambao hawakuwa na silaha waliuawa kwa wingi, hali iliyopelekea Kamanda Samuel Jackson kufikishwa Mahakama kuu ya Kijeshi (COURT MARSHAL) kujibu tuhuma za kusababisha mauaji ya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia. Wale Defending Officers walimtetea na mwisho wa siku kesi ilikuwa DISMISS alionekana hana cha kujibu na hivyo kuachiwa huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Cameo
2.Odeon
3.New Chox
4.Avalon
5.Empress
6.Empire
7.Star Light
8.Drive Inn.
Enzi zile za mapicha ya zama hizo
"Hell up in Harlem"
"Escape from hell"
"Inversion USA"
"War bus"
"Mountain of the Cannibal God"
"Allan Quaterman and the lost city of gold"



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom