Enzi ulipokuwa boarding

Daa wanajamvi mie nakumbuka tulipo fika 2 form one pale Mazwi secondary, tulikumbana na kwataa kwa wiki sita nakumbuka jamaa walitupigasana mabuti na mitama
Ahahahaaah!!! Mkuu Mazwi ya wapi? Ya Headmaster Yamsebo!!
 
Umenichekesha sana!!

Nakumbuka pale Mzumbe SEC ukiumwa Malaria unapewa SOFT DIET(Wali topetope na kabichi). Basi watu tulikuwa tunaumwa kila siku. Tatizo sasa mpaka Daktari wa shule(hata sio daktari), akuandikie(21days SD). Hapo ndugu chereko tu hahaha

hahaha bro umenikumbusha mbali.. dah!! boys kulikuwa na vituko
 
kwa waliosoma mawenzi sec ilikuwa tunapata luch shule ila wavulana waliokuwa bweni walikuwa wanamind hivyo walikuwa wanaenda kunachukua madishi hata ya madarasa matano wanaenda kuyaficha wanakula badae ila walikuwa wakikamatwa wanaletwa assembly cha kushangaza kila dishi walikuwa wanakula watu wawili .
Halafu kulikuwa na wengine wanaenda jikoni wanachota krimu wa juu kwenye sufuria ya maharage
Kwa kweli thoz dayz a nice 2 remember
 
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako,unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote.Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.Waligawana msosi wao wawili wakatosheka,baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!

Nakumbuka kibaha mwaka huo tupo kidato cha kwanza, intake kubwa ilitoka usukumani, na kibaha ilikua punga(wali) daily, siku moja msukuma mmoja alibidi aende kulalamika kwa mkuu, 'Wajameni sisi tunataka mabondo(ugali) mawali atushibagi' ikaongelewa hiyo baraza, jamaa alipata kibano toka form 2 mbaya.
 
kwa waliosoma mawenzi sec ilikuwa tunapata luch shule ila wavulana waliokuwa bweni walikuwa wanamind hivyo walikuwa wanaenda kunachukua madishi hata ya madarasa matano wanaenda kuyaficha wanakula badae ila walikuwa wakikamatwa wanaletwa assembly cha kushangaza kila dishi walikuwa wanakula watu wawili .
Halafu kulikuwa na wengine wanaenda jikoni wanachota krimu wa juu kwenye sufuria ya maharage
Kwa kweli thoz dayz a nice 2 remember
KIBAHA SEC.kuna mwalimu alikua akiitwa MPALAZA alikua wa kilimo na ufugaji.Tulipokua form 1 alikua akisema ni heri form one kumi kufa kuliko nguruwe mmoja wa shule ee bwana nilikua nachukia balaaa.
 
Duh, basi mi nakumbuka tukiwa Old Moshi sec...
kwanza ni bifu tulilokkua nalo na Moshi tech...yani kuna siku tulitembea mpaka huko Moshi tech..kuanzisha vita tu!
Ila nakumbuka zaidi nilipoingia form one nikaitwa na majamaa (na walikuwa wakurya.. kutokana na lafudhi zao-afu nikakumbuka stori nlizokua nasikia kuhusu wakurya ati wakija kusoma sekondari ni wababa kabisa na wao vita ni jambo la kawaida kwao)
basi wakaniita nje ya bweni pale Hanang...wakanipa kiatu kinachonuka uvundo..wakasema nipige simu nyumbani nimwambie baba pesa zimeisha...kwa hiyo nikajifanya ninaongea na baba yangu. Basi nikatunga stori nilipokata simu nikawaambia amesema, atanitumia baada ya muda. Hivyo wakajifanya wana huruma sana...wakanipa shilingi mia, wakasema dogo kajinunulie maandazi na soda ila kabla hujanunua uje na maziwa na mkate mkubwa...duh! nilitoka jasho....
ilibidi niingie bwenini nichukue pesa zangu nikawanunulie...!!!!
tangu siku hiyo...mimi na njia ya hanang siendi...
sanasana nilikua natembea na wale majamaa vipofu, ukiwa nao hawakusumbui...hicho ndo kilichonisave....GUD OL' DAYZ....Auld Lang Syne...

Ahahahaha!!
 
Nakumbuka kibaha mwaka huo tupo kidato cha kwanza, intake kubwa ilitoka usukumani, na kibaha ilikua punga(wali) daily, siku moja msukuma mmoja alibidi aende kulalamika kwa mkuu, 'Wajameni sisi tunataka mabondo(ugali) mawali atushibagi' ikaongelewa hiyo baraza, jamaa alipata kibano toka form 2 mbaya.
Na wale masai waliosema sisi haiwesi kula ugali bila nyama na masiwa!
 
katika vituko,siku moja minaki jamaa ali drop town akarudi na pilau ya ukweli ya maskan si tukiwa ni fom3 akaliweka chini tushee ujamaa, akatokea form2 mmoja naye akaingiza mkono akatoka na tonge mshkaji mmoja anaitwa godlisten akamdaka mkono halafu akamwambia 'nilishe' dogo akamlisha afu akausugua chini mkono wa dogo ili asijirambe wala asiringishie amekula pilau akamwambia nenda
 
KIBAHA SEC.kuna mwalimu alikua akiitwa MPALAZA alikua wa kilimo na ufugaji.Tulipokua form 1 alikua akisema ni heri form one kumi kufa kuliko nguruwe mmoja wa shule ee bwana nilikua nachukia balaaa.
Ahahahaaaah!
 
Siku tukila wali na maharage jioni most of form 1 tulikuwa tunavimbiwa. Shughuli inakuwa usiku bwenini. Ebanaee utafikiri mabomu ya gongo la mboto. Bahati mbaya vitanda vilikuwa double deck, fomu1 chini fomu2 juu. Walichukia mabomu yale na tulipataga shida sana. Kila jambo na wakati wake!
 
Vp ladies,mbona hamtupi mikasa yenu,tunaamini mnayo,mnataka kutuambia wote mmepitia internazionale schools!
 
Kwanjeka noma,kuna mother mmoja tulimkamata mwanae kwa wizi wa viatu,alipotonywa kuhusu mwanae kukamatwa na wanafunzi,alikuja mkuku na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine,wote tulitoka nduki tukamwacha yeye na mwanae.
Ahahaha hapo kwenye blue nona lazima mtoke mkuku, Mama wengine wamechanganyikiwa
 
Nakumbuka kantalamba enzi za milinga nikiwa form wani 1991 tulilazimishwa na form 2 kwenda kupalilia mahindi usiku wa mbalamwezi. Tulipofika shambani tukatoroka na kujificha kanisa lililokuwa jirani na bweni la mirambo. Siku ya pili tukiwa tumerejea mabwenini usiku wakaja form 2 wakiwa wamevaa chupi na vichwani wamejifunika nyasi. Walituchapa fimbo mno. Kuna jamaa alikuwa hatari sana alikuwa anaitwa Bob T (bob tumbo)
Hiyo ilikuwa siku ya kukatwa mikia (kugraduate u form 1) tarehe 9 mwezi wa 9 saa tisa.
 
Nakumbuka mashindano ya kujamba niko f. 3.tulikuwa tunakulamaharage changanya na sukari na ugali mwingi mkitoka prepo tunakula kiporo tena cha beans ,kwenye saa 4.tunatulia kwenye cube mtu akitoa ushuzi muhimu ni ile sauti na lazima mwingine ajibu.kulikuwa na milio kama ya trekta,ndege ,filimbi ...
 
we mama mbavu za...nguu--
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom