Enzi ulipokuwa boarding


Da pole mtoto wa Mpande!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Mpande Namkubali sana!! Mwingine ni Mboya a.k.a Commando. Je wewe ulikuwa enzi zipi? Malale,Kimario,Malissa au Kisuu?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mi nilipitia hapo dah mchaka mchaka noma hadi Round about Isee!! Afu pamoja na samaki kupatikana kwa wingi kule walikuwa hawapikwi, chakula kikuu kilikuwa ni Bondo kwa mbaazi kavu. Nashukuru weekend nilikuwa nikizamia kwa MRs Kirimba(mama pendo) yule mganga wa shule. Mnelamwana ndo alikuwa ticha mnoko kwangu henzi hizo za Headmaster Kissuu.


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Duh boarding nouma siku moja tukiwa 4m1 Bukoba Lutheran 2007 2ko prepal watu c wakawa wanapga kelele mara madam akaja akatubeba darasa zima 2kaenda kulala staff room chini kwny vumbi dah umeme c ukakatika watu wakashangilia wakijua adhabu imeisha ebana eeh tulibak mpk saa 4 usku duh kuna wengne mpk walikoroma i mic boarding!
 
daa mi nakumbuka kinyara sec vyoo vilikuwa vichafu ukiingia inabid uvue nguo,mi nkajifanya mbish nkazama nazo ile kutoka ckushtuka smell naingia clas ilikuwa ucku prepo,maduu wakaanza kulalamika harufu ya kimbo mi nasema mbna sisikii daa jamaa angu alikuwa jiran akantonya mwanangu umeharibu nenda hostel ni hatarii,nlitoka kwa aisbu mbya ctakuja kusahau!!
 
Aaaaagh....! Mkuu kumbe na wewe upo humu from CHIDYA kwa kamanda MWAITENGA na MZEE MZIMA BASE....! CHINDAMBA MATELEPHONE,YY KILA SIKU ANASOMEA CHOONI,HUWA HAPANDISHI AKISOMEA DARASANI.....! HATAREEEEE.....! SANA KAMBONA NA DARK CHAMBER,MAemeo ya hatari hayooooo...!
 
Mm nakumbuka ile systm ya kwenda mjini unaaguzwa na dom zima sasa kuna dada alijua anamimba so akatangaza kuwa anataka kwenda mjini watu c waakamwagiza akakusanya kama hamsin elfu iv(2007) mtu hakurud akapanda gari kwao mbeya mpaka jion watu wanasubr chipsi zao mtu harud ndo kajipatia nauli
 

Kolila sec moshi! Wakati naanza form one nilielekezwa chooni, choo chenyewe ni cha mabati nilipoingia kujisaidia tu walipiga mawe kile choo mpaka nikachanga nyikiwa kidogo nife
 
Kwanjeka noma,kuna mother mmoja tulimkamata mwanae kwa wizi wa viatu,alipotonywa kuhusu mwanae kukamatwa na wanafunzi,alikuja mkuku na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine,wote tulitoka nduki tukamwacha yeye na mwanae.





Ilikua kimuki nn?
 
Duh wadau acha tu Meta sekondari Mby hiyo kulikuwa na mdwanzi mmoja mwl wa nidhamu anaitwa kimatare kila siku yuko ghetin na hakosi kosa mara tai,utasikia mkanda si wa rangi ya shule balaa mtupu ili mradi akupe sitiki.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wapi masela wa BASESCO wa enzi za DINGI, BOB na KAGI?
 
xule hii noma!.mwalim anampiga mwanafunzi utadhani ana ua nyoka

mhanila wa meta sec
2012-2014
 
Umenikumbusha Rungwe Sec. enzi za mwl Adimeli. Kwa mchakamchaka nomaaa!
 
Nakumbuka wakati tuko 4rm 4 kunasiku tuligoma mchana sababu nyama ilopikwa imeoza tuligoma shule nzima. Den tukachapwa darasa letu tu .ikafika chakula cha ucku tukagoma kula. Tukaitwa na headmistres tukaombwa radhi kisha akaitwa tisha alotuchapa akatuomba radhi tukaenda kula na prepo hatukwenda .kumbe wenzetu 4rm 2 wakaja kuiga kufanya mgomo eti kisa hawajapata ndizi walichapwa na prepo walienda na kulala na njaa zao.
 
ninakumbuka siku ya kwanza kuingia bwenini tukakabidhiwa tishu paper basi mimi na mshikaji tukiwa tunatoka bush si tulidhania ni matunda tukapeleka mdomoni ili tule jamaa wacha watucheke.

We ulikuwa noma sana
 
Bwenini kwetu bwana tulikuwa na utamaduni wa kufanyiana birthday..mshikaji yeyote ambaye ana birthday kama itaangukia weekday basi tutaisukuma mpaka usiku wa jumamosi kuamkia jumapili .sasa hapo utaratibu huwa ni kuchangishana jero jero enzi za 2001-2004 ilikuwa iko juu maana tulikuwa tuna badget wali kuku, soda na biskut za kuzugia.sasa bwana ilitokea siku ya kuzaliwa njemba moja,kitu alichotufanyia sita sahau,...kachangisha raia jerojero za kutosha kisha kupotea jumamosi nzima bila kuonekana maeneo ya shulen ili tupange badget maana kunakuwa na kamati .watu tupo dillema bwenini kila mtu kisha ingia kitandani mwake tayari washakata tamaa,punde tunamuona jamaa kabeba ndoo mbili za bati huku zinatoa mvuke, raia tukasema mambo si ndo hayooooo tunajua ndoo moja itakuwa na wali nyingine kuku. Ile kuzifungua,tobaa. Ndoo zimesheeni mahindi na viazi vya kuchemsha..raia tuka maindi sana kwakuwa dinner ya shulen hatukula na njaa zinatuuma, ikabidi tule tu yale maindi na viazi uku tumemindi sana...jumatatu yake kuna mwalimu mmoja mkuda sana alikuwa anapenda kulima maindi kila msimu.bwana si akaja parade kutangaza kuwa kuna mwanafunzi kaiba maindi na viazi shambani mwake!! Watu ayaaaaaaaaaa. nikikumbuka ilo tukio uwa nacheka sana.
 
nakumbuka ilikua 2004 nipo 4m2 hedaru sekondari,kulikua na ticha mnoko sana tulimtunga jina la mbogo.akikudaka anakuambia uchague fimbo 2 au 6
ilikua ni bora uchague sita,ukichagua 2 basi ujue utakaa kwa kalio moja wiki 2
 
pole dogo naona ndio ilikuwa mwisho wa elimu yako, au? maana posti yako ngumu kusoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…