Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

nakumbuka miaka ya 96-97 loleza,mlinzi alikuwa natabia ya kutuchungulia wakati wa kuoga. Cku hiyo kapita bafuni wanafunzi walipomuona wakatoka wote uchi wakaanza kumwita wacha atimue mbio akajua wanataka kumbaka. Jamaa hakurudia tena
Angekamuliwa mpaka damu!
 
Nakumbuka F1 kipindi nikiwa Ruvu Sec mateso yalikuwa makali mno kiasi kwamba tulikuwa tuishi katika mabanda ya vyombo......Nasema mateso yalikuwa makali mno siwezi kusimulia.
Kama ulipitia shule za boarding zamani,hamna haja ya kwenda JKT.
 
Duh, basi mi nakumbuka tukiwa Old Moshi sec...
kwanza ni bifu tulilokkua nalo na Moshi tech...yani kuna siku tulitembea mpaka huko Moshi tech..kuanzisha vita tu!
Ila nakumbuka zaidi nilipoingia form one nikaitwa na majamaa (na walikuwa wakurya.. kutokana na lafudhi zao-afu nikakumbuka stori nlizokua nasikia kuhusu wakurya ati wakija kusoma sekondari ni wababa kabisa na wao vita ni jambo la kawaida kwao)
basi wakaniita nje ya bweni pale Hanang...wakanipa kiatu kinachonuka uvundo..wakasema nipige simu nyumbani nimwambie baba pesa zimeisha...kwa hiyo nikajifanya ninaongea na baba yangu. Basi nikatunga stori nilipokata simu nikawaambia amesema, atanitumia baada ya muda. Hivyo wakajifanya wana huruma sana...wakanipa shilingi mia, wakasema dogo kajinunulie maandazi na soda ila kabla hujanunua uje na maziwa na mkate mkubwa...duh! nilitoka jasho....
ilibidi niingie bwenini nichukue pesa zangu nikawanunulie...!!!!
tangu siku hiyo...mimi na njia ya hanang siendi...
sanasana nilikua natembea na wale majamaa vipofu, ukiwa nao hawakusumbui...hicho ndo kilichonisave....GUD OL' DAYZ....Auld Lang Syne...
Mkuu hapo kwenye red ni bweni la Ilboru au shule ingine?
 
Ilikuwa inaudhi sana,mtu katoka zake likizo ndefu kwao kijijini,akirudi shule amekonda atapewa pole nyingi kwa kuugua,sasa ole wako ujenge shavu ukiwa shule,duh!watu wanaponda mbaya.
 
nakumbuka mbali sana kipindi hicho nilikuwa nimekonda kama vile mgonjwa mana unakuta mt umekonda mpaka unatisha
 
ahhahahahahah, mnenikumbusha mbali mimi wakati nko A'level weruweru sec school tulikuwa tunalima sana sana kuna siku tumevuna mahindi hafu mnayakusanya pamoja mnatengeneza kama kamlima hivi kinaitwa( biwi) watu wa moshi hapo mnenipata sasa kulikuwa na biwi moja kubwa tukalala hapo chini hafu ilikuwa usiku kwenye sa moja hv watu wanapiga kazi mim na rafiki zangu kama wanne hv tukalala chini ya hilo biwi aisee si akaja headmistress akatulamba fimbo sasa tukahisi ni mtu tu anatupiga wew tukaanza kumsema yule mtu oya oya acha mambo yako ya kifala duh kushtuka hv kumbe ni headmistress wacha tukimbie. uzuri akutushika sura yani ingekuwa bonge la soo.
 
wakati niko O'level st.matthw tulikuwa aturuhusiwi kuwa na simu sasa msichana mmoja akawa na simu walimu wakapata taarifa kwamba kuna mwanafunzi anasimu wakafanya msacho wa kushtukiza kwa huyo dent na wakati wanaingia huyo dent alikuwa anaongea na hiyo simu alipoona tu walimu akazima simu unajua aliificha wapi? dah yule ni noma aliificha kunako yan mwalimu alimkagua kila mahali akuona ile simu kumbe msichana kaificha sehemu ya siri yani alitoa kali yam mwaka
 
Kwa wale walisoma Azania High School enzi hizo kunacombination ya PCM pekee yake.Tulikuwa tunajiita tuko HOTELINI kila kitu safi kabisa..Yaani mambo yakuwa safi kabisa kuna hostel master anaitwa Mzee Meja anasema vitukuu mwende mjini lakini kurudi mwisho saa 6 usiku teteeee.
 
pugu kunamwalimu alikua anaitwa mabagala...siku akivuta bangi yake vibaya anawakurupusha kumi na moja alfajiri
 
Eban man umenkumbusha mbali ile mbya,mi nlikuw form 1 miaka 12 iliyopita pale Mtwara Tech School,hakuna k2 nlikuwa cpendi kama mchakamchaka, kaka, toilet ndo lilikuwa chaka langu la kuhide,kumbe viranja wakuda wakanshtukia bas cku 1 nko toi naskilizia wana warud msoton kwa mbli nkasikia mayowe,kidume nkasema yes maboya wanarud ngoja nitoke toi nizuge nlikuwa nao,kaka!Ile nafungua mlango 2 si nkakutana na kilanja mmoja hv alikuwa mnoko kama shule ya babake,yule bwna akanipa bonge la konzi alaf kw jnc alvyokuwa na nguv nkahc kama dodo imedondokea kichwan akanchomoa nje nkaruka kifrog frog cha kutosha,khe!hko nje c nkakutana na wadau wengne wny kamchezo kama kangu...Otea nini kilifata
 
Wakati tupo A level kuna eneo maarufu sana jirani na shule linaitwa Makanyagio. Piga ua ilikuwa never miss wakati wa chai hata kama wanafunzi wengine wapo assembly. Hii ilikuwa kununua kesi LIVE na utawala wa shule maana ilikuwa ni nje ya shule. Wakati mwingine tukipigwa ambush tukashtukia mapema ilikuwa mbio mbaya mtaani. Kama tukichelewa kushtukia basi ni kukamatwa na mboko mtindo mmonja. How I miss my school! It is shame sasa haipo tena shule hiyo.
 
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.

Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako, unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.

Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote. Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.

Waligawana msosi wao wawili wakatosheka, baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.

Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!

heee form one tulikuwa na zamu ya kulinda geti la kuingia shule sikuhiyo nilipangwa na mvulana mmoja wa form 2 kumbe alikuwa ananipenda akashindwa kunitongoza matokeo yake mdogowake tuliekuwa nae form one ndo akafanikiwa kunibanjua ctasahau hiyo sku.

Pia wakati wa kipindi cha dini before prepo nilitajwa kuimbisha wimbo mbele ya shule nzima nilikuwa na aibu balaa nikaimba kwa kujiumauma nilipomaliza nikarudi kukaa kwa aibu sjui nlipatwa na nini nikaamua kutoka nje ya chumba cha dini ile kutoka tu nikajamba ushuzi mkubwaa ukasikika na woteee looo niliona nouma sikurudi dini wala sikwenda prepo haikuishia hapo asubuhi mchakamchaka wasiniimbe nn mbona nilikoma ila coz nilikuwa mpole sana baada ya skumbili soo ikaisha ila nlipata soni mno.
 
Nakumbuka miaka hio Tosa (nikiwa Form 5) tulikuwa tunaishi Bweni la Mandela, juu gorofani. Huko tulikuwa tunaishi katika chumba kimeandikwa 'enter at your own risk.' Siku ya siku nilikuwa sijaenda darasani na wenzangu wawili, ilikuwa ni mishale ya saa 5 asubuhi. Mara ticha kaja, kuingia ndani, sisi wote darini na kurudisha lifuniko. Huko juu mwenzetu mmoja kapaniki, kakanyaga pasipo penyewe--puuuuuuuuuuu hadi kwa ticha--adhabu yake pension miezi mitatu! Mambo hayo
 
Tarehe 1 april, 1996 imenikumbusha mbali.tuliwapiga form 1 wakakimbilia porini mmoja akatenguka mkono.Kilichofuatia kilikua kizaa zaa.nakumbuka lile parade la kutambuana pale mazengo.room yetu ya G5 ilikaa wiki nzima bila kula kwa kuogopa kufukuzwa shule.
 
Nakumbuka shida ya maji tuko form one. Jamaa mmoja katafuta maji kakosa akakuta nyuma ya bweni maji yanatoka kama chemchemi. Akanawa miguu akajing'arisha na sabuni mbuni( yaani kabla ya kukauka vuzrri unapaka sabuni miguuni inakuwa kama ndo mafuta ta ngozi. Komesha akasukutua vizuri na kurudi bwenini bila kujua kuwa chemchemi ilikuwa ni septic chamber:hat:
 

Me nakumbuka 2livyokuwa golan(school) cku ya wal na nyama kuna jamaa 1 albeba wal wake akiendw dom kuula bas kuna jamaa mwngne akamgonga kwa baat mbaya bas ile saan yake ikadondoka na kujifunka chini,basi jamaa akamalizia 2 kumiminia mchuz palepale chini na akaanza kula mpaka anakalibia chini akaacha,daaaaaaaaaaah nlcheka balaaaaaaaaa

hii kalii,nimecheka mpaka basiiii!
 
Tarehe 1 april, 1996 imenikumbusha mbali.tuliwapiga form 1 wakakimbilia porini mmoja akatenguka mkono.Kilichofuatia kilikua kizaa zaa.nakumbuka lile parade la kutambuana pale mazengo.room yetu ya G5 ilikaa wiki nzima bila kula kwa kuogopa kufukuzwa shule.

nyie vijana wa mazengo fujo zilikuwa nyingi. mkiona demu anakatiza miluzi mnapiga hadi midomo inawakaa upande
 
Back
Top Bottom