Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

Eban man umenkumbusha mbali ile mbya,mi nlikuw form 1 miaka 12 iliyopita pale Mtwara Tech School,hakuna k2 nlikuwa cpendi kama mchakamchaka, kaka, toilet ndo lilikuwa chaka langu la kuhide,kumbe viranja wakuda wakanshtukia bas cku 1 nko toi naskilizia wana warud msoton kwa mbli nkasikia mayowe,kidume nkasema yes maboya wanarud ngoja nitoke toi nizuge nlikuwa nao,kaka!Ile nafungua mlango 2 si nkakutana na kilanja mmoja hv alikuwa mnoko kama shule ya babake,yule bwna akanipa bonge la konzi alaf kw jnc alvyokuwa na nguv nkahc kama dodo imedondokea kichwan akanchomoa nje nkaruka kifrog frog cha kutosha,khe!hko nje c nkakutana na wadau wengne wny kamchezo kama kangu...Otea nini kilifata

mbavu zangu mieee....

hii ya kudoji mchakamchaka ilinikuta tena nikiwa uchi wa mnyama naoga nyuma ya bweni kwenye ile sehemu ya kufulia nguo. basi nikajificha chini ya uvungu wa masink, i was ki-portable then kwa hiyo niliweza ku-fit. mwenzangu niliyekuwa naye alikuwa tipwa tipwa so akashindwa kujificha huko uvunguni so akaambulia viboko vya mwalimu wa zamu. imagine alichapwa akiwa uchi tena amelowa. ila namshukuru sana hakunitaja maana sijui nigeliaje siku hiyo!
 
Mambo ya table lida na misosi ya shule sijui nkikumbuka napata aidia kwamba ufisadi ulianza kitambo sana na karibia kila mtz ni fisadi tu..

umeona eeeh.

kuna table leader wetu mmoja wa kijaluo yeye alikuwa anaweka obvious kabisa. yaani kale kabakuli ka kupimia wali ikifika kwake anakashindilia balaa wote tunamwangalia wala hatusemi kitu
 
mazengo complex....tupo sana tu nakumbuka yote hayo kumi ng'ombe wa shule wakati fulani aliibiwa na wezi wamifugo na tukaamrishwa saa kumi ya usiku tuanze msako cha ajabu wengine walitembea hadi msalato girls na wakaingia hadi mabwenini kutafuta ng'ombe kazi ilikuwa kurudi wakati makundi mengine yamerudi saa 2 sisi tulirudi saa 8 na njaa vijasho vikitutoka......boarding naitamani kinoma.

Jamani mazengo to msalato ni mbali sana....ama kweli watu mlipata kisingizio!
 
thread hii imenikumbusha enzi nasoma ifunda tech. School: Tulikuwa na secondmaster wa kijaluo aliyeitwa saka, mzee alikuwa mpole sana ila alikuwa ni mbaya sana kama atakukamata na hatia kwa vile anaweza akakupa adhabu hata ya mwezi mzima. Alfajili moja alikwenda mabwenini kushtukiza zoezi la kukimbia mchakamchaka. Alipofika katika block no.3 la bweni la seuta akagundua kwamba kuna wanafunzi ndani kama wa5 bado wamelala, akawaamsha na kuwaamuru watoke na wenyewe wajitaje majina yao akiamini kwamba watatii. Wale majamaa walishajua kuwa kwa giza lile si rahisi awakariri sura zao hivyo badala ya kutaja majina yao halisi wakajitaja kwa majina ya wachezaji wa simba wa wakati ule: Hussein masha, mohamed mwameja, alfred kategile, george masatu na edward chumila. Alipomaliza kuandika majina yao akawaambia waungane haraka na wenzao ktk mchakamchaka. Kituko cha mwaka ni pale muda wa assembly ulipowadia na s/master huyo kuwasoma watuhumiwa wake ili awape adhabu, kila mtu aliangua kicheko na alipoambiwa kuwa hayo ni majina ya wachezaji wa timu ya simba na yy aliangua kicheko na kuondoka zake.

hahahahahahah!
 
umeona eeeh.

kuna table leader wetu mmoja wa kijaluo yeye alikuwa anaweka obvious kabisa. yaani kale kabakuli ka kupimia wali ikifika kwake anakashindilia balaa wote tunamwangalia wala hatusemi kitu
labda alikua anahakikisha anashiba vyema ili aweze kukitumikia vyema cheo chake cha utebo lida..
 
Umenikumbusha enzi hizo nasoma mlimanicity high school, yani madarasa yetu yalikuwa pale samaki samaki! Alaf pale kwenye parking ndio zilikuwa bustani zetu! Nakumbuka pale vodashop ndio lilikuwa dom langu niliteseka sana kufata maji the game!

Sito sahau enzi hizo
 
n'shomire una vituko !! kha!
 
Umenikumbusha enzi hizo nasoma mlimanicity high school, yani madarasa yetu yalikuwa pale samaki samaki! Alaf pale kwenye parking ndio zilikuwa bustani zetu! Nakumbuka pale vodashop ndio lilikuwa dom langu niliteseka sana kufata maji the game!

Sito sahau enzi hizo
Hii ilikua mwaka gani mkuu usije ukawa ulikua classmate wangu, pale shoprite ulikua uwanja wetu wa basket!
 
Nilikuwa napenda kula ukoko wa ugali na wali enzi hizo form 1....Wangapi tumekula?
 
enzi nipo songea boys kuna cku 2kiwa wa2 km kumi 2metoroka shule njiani 2kaona toyota double cabin 2kasimamisha 2kapanda ile kwenda mbele 2kamuona mwalimu wa nidhamu anasimamisha ile gari ili apate lifti basi ile gari kabla haijasimama vizuri wa2 wote 2liruka km maninja 2kaingia zetu porini
 
Siku ya mtihani wadarasa la saba, form njuka wanakatwa mikia ili kutoka kwenye hali ya viluwuluwi na kuwa vyura kamili. Yaani form njuka watukutu walichezea kichapo balaa na uongozi wa shule uliruhusu. WALIOSOMA KIBITI SEC WANAELEWA HIYO.
 
Nakumbuka seminarini dah ilikuwa balaa ukiwa njuka
 
Mwanangu wewe ulimaliza Pugu boys mwaka gani maana mimi nimemaliza mwaka 2008 form iv.
 
Umenikumbusha enzi hizo nasoma mlimanicity high school, yani madarasa yetu yalikuwa pale samaki samaki! Alaf pale kwenye parking ndio zilikuwa bustani zetu! Nakumbuka pale vodashop ndio lilikuwa dom langu niliteseka sana kufata maji the game!

Sito sahau enzi hizo

wee kweli ni mtoto, kwenye kundi la mamba wewe ni keng.e
 
nakumbuka sana tabora girls nlipokuwa form2 tuliwazomea milambo kwny mechi kesho yake ilikua jmoc wakatulipizia wakatualika disco afu wakawa wanacheza na wadada wa mtaani luckily j2 kukawa na joint mass kwetu basi watu wakaandaa timu ya kuzomea yani walizomea balaa,usku sasa milambo walitembeza kichapo na kumwaga mavi mabwenini..watu waliumia sana hasa 4m5 walokua wageni
 
sitosahau jamaa moja alichomwa kisu pale pale stadium Arusha kipindi hicho kulikua na tour ya bongo records na ugali wa juma nature hakika sitosahau by then nilikua shule 1 ya vipaji Arusha.
 
Back
Top Bottom