Hizo zote stori tu,mwisho wa maelezo ni UMBWE BOYS,siku tunaingia shule tulikuta raia kibao wamevaa vyuti,wanapokea wazazi,kumbe ni madenti,ukiwapa tranka lako tu,imekula kwako,,,ukiingia domitory unakuta vitanda vyote havina chagga,inabidi uende dorm 6,kwa ma 4m six ukanunue chaga,chaga moja ni buku,kama hutakilala chini.....
Mambo ya toilet tulikuta choo kimoja tu kizima,,,kama atm ya crdb saa 12 jioni...mtu nyomiiiii, ukiwa f5 au f1 ukiingia tu lazima "ukatwe mkia", yaani hiyo siku ni fimbo kwa kwenda mbelee, mtarushiwa mawe chumbani, immagine mtu anakuja kunoa panga dirishani kwako usiku wa manane,,,,,,,,,
uji tulikua tunauita fongo, watoto wanaojiweza ndo waliweza kununua sugar, sisi tulikuwa tunapiga fongo chuma-yaani bila sukari au tunachanganya super-deep(jussi kola) tunapata mafleva, uji wenyewe umechanganywa na pumba yaani full kutematema,.
Siku ya nyama au wali ni vita balaa,yaani ukuifanya utafiti,watu wengi sana wanarudi kwao na ngeu za wali....mwisho kabisa ni kwenye vita kati ya sisi na lyamungo boys,,,tulikuwa tunapigania uwanja flani mkuuuubwa tulikua tunapaita desert,tulikua na division of labour ya kutosha,form six walikuwa wapiganaji wakuu,form five kuvunja stoo na kuchukua zana kama majembe, shoka,panga etc....
Form four walikua warusha mawe na kuleta noma,form three walibeba viti,kuni,kuwavunjia wenzetu vioo,kama tungeshinda viti,,form two na one ni waokota mawe na kuwapa wakubwa ili wawarushie maadui na wasindikizaji cz hamna mtu kubaki nyuma.
UMBWE was something else,,,,,siku ya graduation wababe wanabeba mabench na wanaweka kambi kwenye familia yoyote waliokuja kumpongeza mwanao,wanagonga diko then wanahamia familia nyingine.....siku za kwenda shule za girls ni full kuanua nguo za watu na kupiga "butterfly" matranka ya watu ili kupata pamba,,,,,,,
Migomo ya ndani ,watu wanaenda kukata umeme kwenye transformer,,,,,,,,,wezi walikuwa ni wakali mithili ya carlos,watu wanaiba hadi bendera na bunduki ya mlinzi,kuiba ndizi kijijini,,,kuvamia soko la pale kijijini,,,,duuuh,,,,,,embu mwanaUMBWE mmoja aendeleze zile swagg zetu,maana nadhani hamna kambi kama lile