Enyi mliooa, mlipataje wake?

Kumbe nanyi mnakuwaga desparate🙆🙆
Ila mnavyojikutaga miungu sasa😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 

Mkuu

Don't trust any woman you see kwenye daladala,sijui Mlimani City,sijui sokoni,sijui kanisani,sijui barabarani...

Ni too much of a risk mzee...

Easiest and safe ni uulizie kijiijini/mkoa unaotoka wakupe actual referrals!

Kwanini referrals zilizotoka kwenu ni more appropriate ni kwasababu hao wasichana unaopewa referral wanawajua tangu wakiwa wadogo na wanajua walipo now na wanafanya nini na walikua wana behave vipi wakiwa wadogo!

Kuna probability ya wakengeukaji ila ukichukua sample ya 10 girls,utapata mmoja hapo ambae ni perfect fit!

Don't trust any woman in Dar es Salaam unaemuona tu hivi!
 
Dah nimekuelewa saaana mkuu nashukuru sana
 
Hapa watu watakuambia *Sali Sana Mungu atakuonesha*
Wakati wao walikula na kuliwa mingo mpaka kuolewa.
99% ya wanandoa hakuna aliyekaa tu na kusali Mungu akamuonesha.
Tamaa za mwili ndio zilianza.
Hiyo moja nayo nimeiacha kwa kuwa huwa Sina uhakika na yanayoongelewa.!!

Tumejaa uongo uongo tu.
Mwambieni kijana atongoze wanawake!!
 
Kama huko Dar utapata taabu sana, kila demu unayeona anakufaa atakwambia anasoma chuo au anasubir kujiunga na chuo,kila demu mjuaji,kwao wamejenga, sasa wewe uje kumbahatisha anayelala kwenye kochi umri utakuwa umekuacha, ili kurahisisha mambo tembelea sehemu za clinic utapata single mother, hao hawana mizengwe.
 

Hahah
 
Aiseee kuwa makini sana mkuu katika hiyo sekta.
Unamuona mwenzio gwajima na skendo zake zote bado anatetewa na mkewe,si umemuona mkewe alivyokuwa na msimamo thaibiti Ndugu?

Alafu chonde chonde usiyafite mke wakati una genye zimekupanda,kila mke utamuona mzuri sana kwa sababu ya tamaa za mwili.

Mke ambae unaweza kudumu nae ni yule ambae ukimuona tu yanakujia mawqzo ya kumuoa zaidi ya kufanya nae mapenzi tu.maana yake ni kwamba kuna wanawake ukiwatazama tu mavazi yao basi wanakuvutia upate hamu ya kuzini nao.sasa mke akiwa hivyo tahadhari sana.

Nakumbuka wakati nipo kijana nasoma kabla sijaoa kulikuwa na dada falani anavaa hijabu vizuri sana ikawa namzimia sana kwa kweli mpaka nikimuona napata picha ameshakuwa mke wangu tayari na tunaishi vizuri sana,lakini kuna wadada wengine nikiwaona nawaza uchafu tu moja kwa moja.sasa wewe angalia sana sana sana.

Alafu angalia dini yako mkuu,kama ni mkristo basi pahala safi pa kupata mke ni kanisani.sasa kanisani NAKO UCHAGUE,SIO KWA KUWA NI KANISA BASI UNACHUKUA YEYOTE.utajuta na kuleta uzi hapa.kuwa makini kanisani uangalie na kuwashirikisha wazoefu wa sehemu hiyo.

Lakini pia naomba kama una mama basi mtumie kumuulizia akutafutie binti mwenye tabia njema sana anayemjua,wanamama wanajuana sana mtaani wanajua kabisa kwamba nyumba flani yule binti ametulia au hajatulia.kwa hiyo wanajua sehemu sahihi.
Alafu badala ya hapo sasa umwambie akutafutie mke,mama hawezi kukuimgiza chaka hata siku moja,ataeatumia wenzie wamtafutiee nyumba gni kuna binti mzuri.

Akipatikana unawaambie wasiambiwe hapo kwa binti kama una lengo fulani,wewe ufanye mipango kumuona huyo binti na kumtafakari nama alivyo,huku na wewe ukiulizia wadau mbali mbali juu ya mwenendo wake,ukiona umempenda namna alivyo na tabia ziko fressh basi hapo anza kutupa ndoana na kupeleka taarifa rasmi kwa huyo dada mdogo mdogo ili naye tuone kama atakuwa amekukubali.

Ila tu mkuu...

Ukitaka mke mwema basi kuwa wewe mwema kwanza.anza kutengenea mda huu tulie na kutuliza akili sio useme utatulia ukioowa shauri yako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…