Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Mungu hayupo.

Dini ni utapeli.
Mafundisho kuhusu uwepo wa Mungu yanapatikana katika Biblia, hasa katika sehemu kama vile Kitabu cha Mwanzo hadi Kitabu cha Ufunuo.

Kwa Uislam, mafundisho yanapatikana katika Quran.

Mkuu, Mungu yupo ila epuka manabii wa kizazi kipya, Maana vitabu vya kidini hakuna sehemu iliyo andikiwa kuwa kuna manabii wapya watakuja.
 
Kasome biblia imeandikwa kuwa shetani ujiinua kwa kila kiitwacho mungu kisicho mungu....maneno hayo maana yake ni pana sana...kwa kifupi shetani utina nguvu kila kitu potovu kinacho usishwa na mungu mfano mafundisho potovu ....ibada potovu ...mitume feki ...manabii feki ...watakatifu feki wote hao upokea nguvu kutoka kwa shetani iwe ni kwa kujua au kutokujua ...ndiyo maana ikaandikwa kuwa siku ya mwisho watasema je hatukutoa pepo kwa jina lako na kuponya kwa jina lako na yeye atawaambia wazi ondokeni kwangu nyinyi watenda maovu.
• Umetoa neno zuri mkuu, sasa kwa nini mungu anamua yote haya yatokee?,
• Je ametuchoka? Au ametupa mtego wa kiimani?
 
• Umetoa neno zuri mkuu, sasa kwa nini mungu anamua yote haya yatokee?,
• Je ametuchoka? Au ametupa mtego wa kiimani?
Sasa umesha ambiwa umejua mema na mabaya basi tenda mema usitende mabaya ...ukitenda mema utalipwa mema ukitenda mabaya utalipwa mabaya sasa mungu alaumiwe kwa lipi ? Au wewe ndiyo umekataa kulipwa mema kwa kutenda maovu ?
 
Wewe unao uwezo wa kuthibitisha kuwa hayupo ?
Labda atakua hana imani na muumba wake,
uumbaji wa binadamu, kama vile Mwanzo 1:26-27 inayosema kwamba Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake.
 
Ndg zangu wakati mwingine napata contradiction kuhusu nguvu na mamlaka ya Mungu hapa duniani ila tu niwaambie kweli Mungu mkuu mtakatifu na mwenye uwezo wa kila kitu yupo, pia ana kusudi kufanya yote haijalishi ya kheri au shari, yeye ndiye mwenye Siri kuu ya Dunia na ulimwengu.

Yeye ndiye Alfa na Omega
Yeye ndiye mwenye huruma
Yeye ndiye mwenye umiliki na mamlaka yote
Yeye ndiye hukiriwa na falme zote za kuzimu kwa uwezo wake wa ajabu

Mungu hachunguziki
Mungu nayemzungumzia hapa haeleweki
Mungu nayemsema hapa ndiye mwenye kusema iwe na ikawa, ndiye mwenye kukubali nakukataa kata kata

Mungu huyu ndiye mwenye kusudi kuu la kila jambo litokealo hapa Duniani

Pamoja na makosa yake shetani na falme zake zote za giza bado wanamkiri kwenye vinywa na nafsi zao kuye Yeye ndiye Bwana wa majeshi, yanayoendelea Duniani ni Ishara kuwa ndiye muweza wa yote, ndiye huwezi ukamtafakari ukammaliza, hachunguziki, haeleweki na haelezeki.

TABAKIA KUWA MUNGU TU. SIO MUNGU WAKUFIKIRIKA NI MUNGU ALIYE DHAHIRI NA KUNA SIKU WOTE TUTAPATA KUONA UKUU WAKE BILA KIFICHO.

Haelezeki naomba niishie hapa...

Ombi langu rudi kwake fanya toba, ni msikivu atakusikia atakusamehe atakupa bega lake uegemee, atakufuta machozi haijalishi ulimkosea kiasi gani, usione shida zinaendelea hapa dunia, mf vita, umasikini magonjwa ukasema sio Mungu wa huruma, hapana

Huyu ndiye mwingi wa huruma.
Asante sana mkuu, Kwa mchango wako mkubwa 🙏🙏
 
Mtume wala nabii siyo matokeo ya kutumwa na mungu ....maana mungu anaweza hakatuma hata mbuzi kufanya jambo fulani ...mtume na nabii ni madaraja ya watakatifu na uchamungu na dhawabu yoyote mwenye kiwango cha uchamungu na utakatifu na dhawabu ya juu huyo ni mtume au nabii hata kama hafanyi utume au unabii
Mkuu, Kwa hiyo unasadiki manabii waliopo sasa ni sahihi,???
 
Halafa sasa ukifatilia jinsi mvua inavyo tokea, kama unaakili timamu lazima ukiri mungu yupo.
Ni kweli mkuu, Katika muktadha wa Biblia, kuna maandishi mengi yanayozungumzia mvua. Kwa mfano, Agano la Kale linajumuisha hadithi ya Nuhu na safina, ambapo Mungu alileta mvua kwa siku 40 na usiku 40. Hii inapatikana katika kitabu cha Mwanzo, hasa Mwanzo 7:12.
 
Nuhu na safina , juma na uledi na ile ngoma kubwa ya kuchezea mpira.
 
Sasa umesha ambiwa umejua mema na mabaya basi tenda mema usitende mabaya ...ukitenda mema utalipwa mema ukitenda mabaya utalipwa mabaya sasa mungu alaumiwe kwa lipi ? Au wewe ndiyo umekataa kulipwa mema kwa kutenda maovu ?
Asante sana mkuu, Kwa mchango mzuri ✍️✍️✍️.
 
Mfano wa nabii wa kweli unaweza kuwa

1. kama Nabii Muhammad katika dini ya Kiislam, au

2. Nabii Isa katika Ukristo. Wote walikuwa viongozi wa kiroho na waleta ujumbe muhimu kwa watu wao
Sahihisho: kwenye Ukristo hakuna Nabii Isa.

Mada yako ni njema sana na fikirishi kwa Wakristo. Thanks.
 
Haijalishi hata kama ni wa uongo wapo wanaokolewa nao,wakishaijua kweli ujitenga nao.
Acheni magugu na ngano vimee kwa pamoja wakati ukifika vitatenganishwa
 
Sahihisho: kwenye Ukristo hakuna Nabii Isa.

Mada yako ni njema sana na fikirishi kwa Wakristo. Thanks.
• Nabii Isa ni jina la Kiarabu linalotumika kumtaja Yesu Kristo katika dini ya Kiislam.

• Yesu Kristo anachukuliwa kama nabii wa pekee na wa kweli.

Asante sana mkuu, Kwa masahihisho 🤝🤝
 
Haijalishi hata kama ni wa uongo wapo wanaokolewa nao,wakishaijua kweli ujitenga nao.
Acheni magugu na ngano vimee kwa pamoja wakati ukifika vitatenganishwa
Mkuu, Kama nabii ni wa uongo, ataokoa vipi wanadam kutoka kwenye shida zake.??
 
Back
Top Bottom