maajabu makubwa, huko sio kuingilia mambo ya mpira? huoni hata afya za wachezaji zitayumba kwa timu yao kuyumba? mpaka wachezaji wenye asili ya Urusi wananyanyaswa kama vile na wao ni sehemu ya urais wa Urusi. Hii sio sawa aloo, double standardEngland imemuwekea vikwazo Roman pamoja na mali zake na Chelsea ni mali yake. Kwa kifupi tu England haijachanganya siasa na mpira ndiyo maana pamoja na kufungiwa mmiliki wao wamepewa special license kuendelea kufanya kazi.
Chelsea imevurugwa sana na wanasiasa katikati ya msimu bila kosa lolote la kimpira kwa mmiliki, uongozi, benchi la ufundi wala wachezaji. Abramovich hakuna ushahidi kama yeye ndiye ameamuru uvamizi wala kugharamia vita, ni vipi FIFA ikae kimya kwenye hili?Safari hii FIFA wameruka sarakasi 🤸 huku wakiwa wamevaa taulo.