Fakyuol
Senior Member
- Nov 26, 2023
- 142
- 311
Kanuni za mpira tulipokuwa watoto:
1. Mtoto mnene daima alikuwa mlinda mlango.
2. Mmiliki wa mpira ndiye anayeamua na niacheza.
3. Kama hukushiriki kutengeneza mpira, huchezi mechi.
4.Mwenye mpira akikasirika, mchezo unakwisha.
5. Ukigonga vidole vyako kwenye jiwe na damu inatoka, unafunika eneo la jeraha kwa mchanga kama huduma ya kwanza na mchezo unaendelea.
6. Humpigi chenga sana mmiliki wa mpira, hii inaweza kumsababishia kuchukua mpira wake na kumaliza mchezo.
7. Hakuna kuotea.
8. Hakuna refa.
9. Kuna kosa tu ikiwa kosa ni kubwa.
10. Wachezaji bora wawili hawawezi kuwa kwenye timu moja, kila mtu anachagua wachezaji wake.
11. Mchezaji bora uwanjani daima yupo kwenye timu moja na mmiliki wa mpira.
12. Daima kuna nyumba ambapo mpira ukidondoka huko, tulijua mchezo umemalizika. Hivyo lazima mjilinde usiende huko mpira!
13. Kutofautisha timu, moja ya timu inavua mashati yao.
14. Mchezo unamalizika wakati wa giza na hatuoni mpira vizuri, tunatawanyika katika makundi tukichekeshana hadi tunapofika nyumbani kukutana na adhabu nyingine kutoka kwa wazazi wetu.
Utoto raha sana aisee!
C&P owner