Eneo la Selander Bridge limekuwa ni makao ya wauaji

Eneo la Selander Bridge limekuwa ni makao ya wauaji

hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, salender bridge iko karibu kabisa na kituo cha polisi, sasa majamaa lakini bado yanaweza kujiicha hapo kusubiri mawindo yao. Morogoro road maeneo ya jangwani nayo ni hatari mno, sasa pale hata kituo cha polisi hakuna karibu. Lakini maeneo mengi dar kwa sasa ni hatari sana kupita usiku.


hawa askari huwa wanakula na awa wahuni
siwaiti majambazi awana hadhi ya ujambazi,..hata ukienda pale kituon mit 40 unasikia askari wanakutajia atakuwa salehe,ama mtu fulani,...aliibiwa mtoto wa kigogo mmoja jamani kama mnakumbuka mliokuta siku hiyo defender zilimwagika wakaingia ule msitu wakakusanya simu,,,camera...wahuni...na vingine vingi mpaka leo aijulikana viliishia wapi...mwisho wa siku nahisi wanapeleka vitu ambavyo wameiba usiku kwa wakuu pale salender kituon
 
Salender bridge hata mchana nilashashuhudia jamaa anachomoa side mirror wakati gari ikiwa kwenye follen na akaishia nayo baharini. Juzijuzi walimvunja mchina mmoja mkono na kumuumiza sana. Inasemekana polisi walimwona mchina huyo akiwa kwenye mazoezi na kamera yake wakamwambia asiendelee mbele ya daraja ni hatari lakini mchina akawa mbishi, dakika chache tu akarudi yuko hoi na mkono umevunjika. Polisi wakubaliana na hiyo hali.
 
Jamani Bongo inatisha,na siyo hapo tu ni ukanda wote wa Ocean Road kuanzia Ferry hadi Agakhan Hospital,usidhubutu kushuka kama utapata tatizo kwenye gari na hata kama unatembea kwa miguu pia,kuna vijana hujitokeza wakitembea kujifanya kama wanaelekea uelekeo wako na hata sometimes opposite direction lakini baada ya mita chache wanakugeuka na kukupora! take care.
 
Jamani Bongo inatisha,na siyo hapo tu ni ukanda wote wa Ocean Road kuanzia Ferry hadi Agakhan Hospital,usidhubutu kushuka kama utapata tatizo kwenye gari na hata kama unatembea kwa miguu pia,kuna vijana hujitokeza wakitembea kujifanya kama wanaelekea uelekeo wako na hata sometimes opposite direction lakini baada ya mita chache wanakugeuka na kukupora! take care.

bongo inasikitisha,nchi sijui inaelekea wapi?haya maeneo salender bridge,ocean road,oysterbay,masaki tulikuwa tunatembea kwa miguu usiku kucha leo hii hata ukiwa kwenye gari roho juu?sasa maisha gani haya kutoana roho kwa visimu na camera??
 
Wadau wa JF,
Akafungua mlango aliposhuka tu,mara likaja kundi la vijana kama kumi wakamzunguka wakampiga sana, wakamyanganya laptop.hand bags,simu,na vitu vingine vilivyokuwa kwenye gari.jamani habari ndiyo hiyo.ya msitu wa salander bridge.

Mimi mtu akiniibia Simu namuongezea na Salio kabisa ili aitumie, akiitumia tu kwa kupiga au kuhamisha Salio namkamata
 
.
hii habari imebase kwenye ukweli kabisa, imemtokea mtu huyo kweli, na mimi ninajua imetokea.
Poleni sana wandugu.
hili eneo ni ukanda wa hatari sana, na Jeshi la Police linajua, lakini wanasubiri mpaka binamu ya Mwema afe pale.
Kwa sisi tunaotumia njia hiyo tumeshazoea,yaani ni kama viuno unyagoni,na sisi tunaamini kabisa kuwa na polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine,kwasababu pale pana kituo cha polisi na makazi yao kabisa,na chakushangaza ni kwamba zamani eneo lile lilikuwa linalindwa full time,why not now?
 
Mimi kinachoniudhi ni kuwa, few days ago, Kova alikuwa anakula coverage kwa issue ya Jerry Muro; wakati kuna maswala kama haya yanayofahamika na anayakalia tu kimya baba yule; ananikera kama nini. Swala la kuibiwa side mirrors siku hz limekuwa kama ubabe kwenye mataa / foleni. Yaani mtu anakuja anakushikia kisu kwenye mataa hasa hasa pale ubungo, na kuichomoa side mirror kama yake hv na huku wananchi wanamwangalia. Clouds wameshapaongelea sana pale Ubungo kwenye Power Breakfast, and wananchi wamelalamika sana polisi but nothing has been done mpaka sasa. Yaani Kova yeye anakimbilia kazi zisizomuhusu za kina Jerry Muro, kazi ambazo angeweza kuwapa Takukuru au vijana wake wa kazi, na kuconcentrate kwenye major issues za Dar kama huu ubabe wanaofanyiwa wananchi. Issue ya SB imekuwa kama jambo la kawaida, yaani mchana saa nyingine wakiwa na uhakika kuwa umebeba cash and wakailocate by chance, yaani wanavunja hadi kioo, imeshatokea once pale.

Haya tuache hayo, tuangalie pia swala la wizi wa magari pale Mlimani City na sehemu nyingine hapa bongo, inakera sana. Imagine mtu unaibiwa power windows then zinapelekwa Gerazani / Mnadani / Buguruni / Dodoma and polisi wanajua kabisa hz sehemu and wanakaa kimya day and night na wananchi wanaishia kuconclude tu kuwa hakuna msaada wa polisi na kuishia kununua mali zao wenyewe. Huu ni ubabe usio na msingi hasa kama tuna jeshi la polisi. Otherwise litakuwa ni bora jeshi and not jeshi bora kama wananchi wanafanyiwa ubabe live.

Mwema, Kova na wapambe wao wananikera sana and sana kutokana na namna wanavyoshindwa kuzingatia maswala ya muhimu...!!!
 
Kwa sisi tunaotumia njia hiyo tumeshazoea,yaani ni kama viuno unyagoni,na sisi tunaamini kabisa kuwa na polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine,kwasababu pale pana kituo cha polisi na makazi yao kabisa,na chakushangaza ni kwamba zamani eneo lile lilikuwa linalindwa full time,why not now?

we mwema alipata breakdown ndugu ama mtoto wa mwema kaka wakamtenda asbh tunaeleke makazini mwetu tunakuta salenda imejaa defender 4 pale traffic light mbili zimekaa katikati kama zina breakdown..alafu upande mmoja ukafungwa kama dk 25 tukaona jamaa wanakimbia wanatokea kule porini we palikuwa oatamu wakaanza kupiga risasi angani vijana wakasimama wakawakamata kama mende wengi tu ...sasa aisaidii tatizo lao wakiwataja wahhusika wanaachiliwa wanadili na waliohusika na tukio matokeo yake ndi hao maharamia wanaendelea na kazi zao ila wanajulikana fika
 
Hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, Salender bridge iko karibu kabisa na kituo cha Polisi, sasa majamaa lakini bado yanaweza kujiicha hapo kusubiri mawindo yao. Morogoro road maeneo ya Jangwani nayo ni hatari mno, sasa pale hata kituo cha Polisi hakuna karibu. Lakini maeneo mengi Dar kwa sasa ni hatari sana kupita usiku.
Ndugu yangu kwa hali ya sasa ukiwategemea hawa polisi basi hakuna atakayepona,dawa ni kuwa makini funga vioo ufikapo eneo hilo, pili kama gari likihalibika basiwajulishe ndugu na jamaa, wewe ukiwa ndani ya gari lako. Tukiwategemea sana hawa polisi wakati tukijua wanagawana na hawa watu hakuna lolote la maana watakalofanya.
 
It is really realy weird kama ni eneo lipo karibu sana na kituo cha polisi cha Osterbay na kuona jinsi gani Mapolisi wetu walivyo wazembe
 
Dar siku hizi ilishakuwa kama Movie za kimafia. Inabidi kukata tamaa tu, kuwa ukiibiwa gari basi shukuru Mungu uhai wako bado unao.
 
hakuna jiji lisilo na matukio makubwa kama hayo pamoja na kuwepo askari polisi,la msingi ni kujilinda mwenyewe kwanza.
 
Back
Top Bottom