Endapo 1985 Nchi yetu ilikuwa imeendelea kwa kiwango Cha kuruhusu vyombo vya habari kuripoti kesi ya uhaini kesi ya Mbowe ina nini?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179

Kesi ya uhaini hukumu yake Ni kifo na Ugaidi hukumu zake Ni hafifu zaidi Ni kitu gani kinaipa serikali yetu hofu ya kutaka watu wasijue kinachoendelea mahakamani?​

Ingekuwa nchi za wenzetu kesi hii ingekuwa live luningani hapa kwetu Kuna shida gani?
Kama mnabisha ushahidi upo hapa kesi kuripotiwa sio Jambo geni hata hapa Tanzania.

Kesi ya uhaini 1985: Mkurugenzi Usalama wa Taifa atoa ushahidi -23​

Wednesday March 17 2021​



Baada ya Luteni Kanali Davis Mwamunyange wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoa ushahidi wake mahakamani, baadaye alikuja shahidi wa 20 wa upande wa mashtaka ambaye siku hiyo, Jumatano Februari 6, 1985, alitajwa mahakamani kama ‘Shahidi X’ ambaye alisema alichukua hatua ya kuimarisha ulinzi wa karibu kwa Rais na viongozi wengine mashuhuri nchini mara baada ya kupata taarifa kwamba mshtakiwa wa pili, Christopher Kadego, alikuwa Arusha kutafuta risasi za kumuulia Rais





william-shaopic-data.jpg

IN SUMMARY
  • Baada ya Luteni Kanali Davis Mwamunyange wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoa ushahidi wake mahakamani, baadaye alikuja shahidi wa 20 wa upande wa mashtaka ambaye siku hiyo, Jumatano Februari 6, 1985, alitajwa mahakamani kama ‘Shahidi X’ ambaye alisema alichukua hatua ya kuimarisha ulinzi wa karibu kwa Rais na viongozi wengine mashuhuri nchini mara baada ya kupata taarifa kwamba mshtakiwa wa pili, Christopher Kadego, alikuwa Arusha kutafuta risasi za kumuulia Rais

Baada ya Luteni Kanali Davis Mwamunyange wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoa ushahidi wake mahakamani, baadaye alikuja shahidi wa 20 wa upande wa mashtaka ambaye siku hiyo, Jumatano Februari 6, 1985, alitajwa mahakamani kama ‘Shahidi X’ ambaye alisema alichukua hatua ya kuimarisha ulinzi wa karibu kwa Rais na viongozi wengine mashuhuri nchini mara baada ya kupata taarifa kwamba mshtakiwa wa pili, Christopher Kadego, alikuwa Arusha kutafuta risasi za kumuulia Rais.

Shahidi X ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, aliiambia Mahakama Kuu kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa hatua tatu alizochukua mara moja baada ya kuletewa taarifa ya Kadego kuwepo Arusha akitafuta risasi. Wakati uhaini huo ukisukwa, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni Dk Augustine Philip Mahiga.

Mahiga, ambaye katika kesi hii alipewa jina la ‘Shahidi X’, ambaye wakati akitoa ushahidi huo alikuwa mshauri wa kijeshi katika ubalozi wa Tanzania nchini Canada, alisema kuwa mjini Dar es Salaam hatua aliyochukua na idara yake baada ya kupata taarifa hiyo ni kuhakikisha iwapo katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuna askari mwenye jina la Christopher Kadego.

Hatua ya kuwasilishwa mahakamani kama ‘shahidi X’ kulifuatia ombi la kiongozi wa timu ya mashtaka, William Sekule, kwamba kwa sababu za kimsingi shahidi huyo wa 20 ajulikane kama ‘shahidi X’ na mwingine wa 21 ajulikane kama ‘Shahidi Y’ ili kukwepa majina yao yasitangazwe na vyombo vya habari.

Alisema hata hivyo, majina kamili ya mashahidi hao yamo katika taarifa zao na kwamba lengo lilikuwa ni kuepuka vyombo vya habari kuyatumia. Jaji Kiongozi, Nassor Mzavas alilikubali ombi hilo ambalo halikupingwa na mawakili wa washtakiwa.

Akitoa ushahidi wake kwa kuongozwa na Sekule, ‘Shahidi X’ alisema Desemba 15, 1982 alipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Abdallah Shaban Mhando (shahidi wa kwanza, dereva teksi) na alimweleza kuwa alikuwa na jambo kubwa la kumfahamisha.
‘Shahidi X’ alisema kuwa alipanga kuonana naye siku ya pili yake saa mbili ili amueleze habari hizo baada ya yeye kumpa namba za gari lake na kukubaliana mahali pa kukutana.

“Siku hiyo nilisubiri kwa muda wa nusu saa lakini hakutokea mtu huyo,” alisema.

Aliiambia mahakama kuwa baada ya kumkosa alimtumia mtu ambaye alimuagiza ampatie Mhando simu yake kwa vile yeye ‘Shahidi X’ alikuwa hamfahamu kwa sura.

Baada ya kujaribu kumtafuta alikokuwa akiegeshea gari lake na kumkosa, alisema alizidi kumwelekeza mtu huyo (wa kati)amtafute siku ya pili, hasa baada ya kumwambia kuwa Mhando angeenda Harare (Zimbabwe).

‘Shahidi X’ aliieleza mahakama kwamba alifanikiwa kuonana na Mhando Januari 2, 1983 na kwamba walipokutana alimweleza kuwa alichelewa kufika sehemu waliyokubaliana Desemba 15, 1982 kwa sababu gari lake liliharibika. Pia alimfahamisha kuwa Desemba 17 alisafiri kwenda Harare.

Mara baada ya kuonana, shahidi huyo aliieleza mahakama kwamba Mhando alimwambia kuwa akiwa kama teksi dereva alikuwa amekodishwa kuwaendesha watu wawili aliomtajia majina yao kuwa Hatibu Gandhi na Kapteni Martin ambao alisema ni Watanzania waliokuwa wakiishi Kenya.

“Alinieleza kuwa Martin (Mohamed Tamimu) alikuwa hatoki nje na kama akitoka basi ilikuwa ni usiku na kwamba vitendo vya watu hao wawili na mienendo yao ilikuwa ikimtia wasiwasi,” Shahidi X aliiambia mahakama.

Shahidi huyo alidai alielezwa na Mhando kuwa watu hao wawili walikuwa wakiendesha mikutano mbalimbali ya siri iliyowajumuisha raia na wanajeshi na kwamba walikuwa wakifunga milango wakati wakifanya mikutano hiyo.

Alisema alielezwa pia kwamba kazi yake (Mhando) ilikuwa ni kuwasafirisha wajumbe wa mikutano hiyo kwenda na kurudi kutoka mkutanoni na kwamba walionekana kuwa na fedha nyingi kutokana matumizi yao yasiyo ya kawaida.

“Aliendelea pia kwamba aliyekuwa akitoa fedha hizo alikuwa akijulikana kwa jina la Father Tom na alikuwa ametokea Ulaya,” alidai ‘Shahidi X’ na kuongeza kwamba alielezwa hivyo na Mhando na pia kila alipokuwa akimwendesha Gandhi alikuwa akilalamika kuhusu hali mbaya ya uchumi.

Alidai, alielezwa na Mhando kwamba yeye aliwahi kuambiwa na Gandhi wakati mmoja alipokuwa akimwendesha kwamba hali hiyo mbaya ya uchumi watairekebisha kwa kuiangusha Serikali na kumuua Rais.

‘Shaidi X’ alisema baada ya kuelezwa hayo alimuomba Mhando amwonyeshe moja ya nyumba zilizokuwa zikitumika kwa mikutano hiyo na kuwa nyumba ambayo alimuonyesha ilikuwa karibu na Drive Inn Cinema.

“Baadaye nilimwagiza aendelee kuwasiliana na mimi kuhusu yale aliyokuwa akisikia kutoka kwa watu hao na hasa nilimsisitiza ajaribu kukumbuka majina ya watu hao na wengine kama watakavyokuwa wakitajwa,” aliiambia mahakama.

Alisema baada ya kupata taarifa ndipo walipoanza kuifanyia kazi Januari 3, 1983, kwanza kwa kuifanyia uchunguzi kuithibitisha na kwamba aliishughulikia taarifa hiyo akiwa na wasaidizi wake wawili—Mkurugenzi wa Usalama wa Ndani na Mkuu wa Idara ya Ulinzi.
Aliiambia mahakama kuwa mkuu huyo ambaye alitambulishwa mahamakani kama Shahidi ‘Y’ ndiye aliyepewa jukumu la kuratibu utekelezaji na ufuatiliaji wa taarifa hiyo na kwamba baadaye alimchukua ‘Y’ na kumtambulisha kwa Mhando na kumwagiza taarifa zote za kila siku ampatie ‘Y’ badala ya yeye.

“Januari 4, 1983, ‘Y’ alinipa taarifa aliyoipata kutoka Makao Makuu ya JWTZ iliyohusu kuwapo nchini na kutambulika kwa Kapteni Mohamed Tamimu iliyosema alikuwa ameonwa na Luteni Kanali Mbwile (shahidi aliyekwishatoa ushahidi wake) na kwamba Mbwile alishapeleka taarifa hiyo kwa Mkurugenzi wa Usalama Jeshini,” alisema katika ushahidi wake.

Shahidi ‘X’ aliendelea kusema kwamba (Shahidi) ‘Y’ alimwambia kuwa Jeshi lilikuwa likitaka kumkamata Tamimu na kumshtaki kwa kosa la utoro akiwa jeshini, “Lakini ‘Y’ aliwaeleza wasifanye hivyo kwa sababu kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea kuhusu watu waliokuwa wakiishi katika nyumba aliyokuwa ameonyeshwa na Mhando,” alisema.

Alidai pia kwamba baadaye uchunguzi ulipokuwa ukiendelea alifahamu kuwa nyumba iliyo karibu na Drive In Cinema ilikuwa ya George Banyikwa.

Alidai pia kwamba siku hiyo ya Januari 4, 1983, aliletewa taarifa na ‘Y’ kwamba mwanajeshi mmoja kwa jina la Sajini Temu alienda Ikulu kutoa taarifa kuwa amekuwa akishawishiwa na mkuu wake wa kazi, Kapteni Mbogoro (mshtakiwa wa saba) ashiriki katika mipango ya kuipindua serikali akiwa na jukumu la kutafuta askari watano.

‘Y’ alimpa jukumu Sajini Temu kuendelea kuhudhuria mikutano hiyo na kuendelea kutoa taarifa kila siku kwake, shahidi ‘X’ alidai mbele ya mahakama hiyo. Mapema aliiambia mahakama kwamba Sajini Temu alihudhuria mmoja wa mikutano hiyo kwa kupelekwa na Mbogoro ambako alitambulishwa kwa wajumbe wa mkutano huo.

Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, alihojiwa na mawakili wa utetezi. Je, aliulizwa nini na alijibu nini? Tukutane toleo lijal
 
Back
Top Bottom