Nimekuwa naangalia jengo la iliyokuwa Embassy Hotel kwa muda mrefu sana sasa imefungwa na hakuna hata dalili yoyote ya kufufuliwa au kutumika kwa shughuli nyingine ya kibiashara.
Jengo lipo mahali pazuri sana lakini linasikitisha sana linavyochakaa na sina hakika kama linalipiwa kodo stahili kwa jiji. Kitendo cha kuliacha jengo hilo katika hali ile ni hasara kwa Taifa.
Nimejiuliza sana kuwa ni kitendawili cha aina gani hicho kimeshinda wakuu wote wa mkoa wa Dar-es salaam na mawaziri wa ardhi na mawaziri wakuu kwa muda mrefu kiasi hicho?
Kama kuna mwenye habari zozote kuhusu Embassy Hoteli na hili jengo kwa ujumla tunaomba atuwekee hapa.
Natanguliza shukrani zangu.