Elon Musk: Tajiri mpya namba moja duniani

DIDAS TUMAINI

Senior Member
Nov 11, 2014
144
500
Mwanzilishi, Mkurugenzi Mkuu, Fundi Mkuu na Mbunifu Mkuu wa kampuni ya SpaceX inayojihusisha na utengenezaji wa vyombo vya kusafiri na kufanya uchunguzi katika anga za mbali; pia mwekezaji na Mkurugenzi Mkuu na Fundi Mkuu katika kampuni ya kutengeneza magari ya umeme -Tesla; pia mwanzilishi wa kampuni ya Boring (The Boring Company) inayojihusisha na uchimbaji matanuri na mahandaki kwa ajili ya usafiri wa magari na treni; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Neuralink inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kupandikiza kwenye ubongo na kuufanya ubongo uweze kuwasiliana na 'computer'; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni (ya kujitolea) ya OpenAI inayojihusisha na tafiti za kiteknolojia - Ellon Musk ametangazwa kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani.

Elon Musk alizaliwa jijini Pretoria nchini Afrika kusini mnamo mwaka 1971. Kwakuwa baba yake ni raia wa Afrika Kusini wakati mama yake ni raia wa Canada, Musk alipatiwa Uraia wa nchi hizo mbili; Afrika Kusini na Canada. Akiwa na miaka 17 alihamia nchini Canada na kujiunga na chuo kikuu cha Queens, lakini miaka miwili baadaye alihamia nchini Marekani na kijiunga na chuo kikuu cha Pennislvania. Hapo alifanikiwa kuvuna shahada mbili kwa pamoja; shahada ya Uchumi na shahada ya sayansi katika tawi la Fizikia.
Mwaka 1992 alipatiwa uraia wa Marekani na kuwa mtu mwenye uraia wa nchi tatu; Afrika Kusini, Canada na Marekani.

Mwaka 1995 alihamia jimboni California kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) katika masomo ya fizikia na sayansi ya nyenzo kwenye Chuo Kikuu cha Stanford, lakini baada ya siku mbili tu aliachana na masomo ya uzamivu na kuanza kujihusisha na biashara.

Akawa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Zip2 iliyokuwa ikitengeneza programu pepe za tovutini (web softwares). Mwaka 1999 kampuni hiyo ya Zip2 ilinunuliwa na kampuni maarufu ya Compaq kwa dola za kimarekani million 307. Baadaye Musk alianzisha kampuni ya X.com ambayo ni benki ya mtandaoni (online bank). Katikati ya mwaka 2002 kampuni ya X.com iliungana na kampuni ya Confinity na kupata kampuni mpya ya PayPal, ambayo Oktoba 2002 ilinunuliwa na kampuni ya eBay kwa dola za kimarekani bilioni 1.5

Kabla ya kuuza PayPal, Musk alikwisha anzisha kampuni ya SpaceX miezi mitano nyuma; mei 2002. Mwaka 2004 Musk aliomba kujiunga na kampuni ya Tesla Motors, Inc. (sasa Tesla, Inc) ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka mmoja nyuma, akawa mbunifu magari katika kampuni hiyo. Mwaka 2008 akawa mkurugenzi mkuu wa Tesla, Inc.

Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2020 Ellon Musk alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 27, akiwa nje ya watu 50 tajiri zaidi duniani. Lakini ndani ya kipindi cha miezi 12, Musk amevuna zaidi ya dola bilioni 150, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko utajiri wa Bill Gates aliovuna kwa maisha yake yote. Sasa Ellon Musk ana utajiri wa dola 185 za kimarekani, amempiku Jeff Bezo aliyekuwa akishikiria nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na dola 184.
Kupanda sana kwa thamani ya hisa za kampuni la Tesla, Inc. kunatajwa kuwa moja ya sababu za kumtajirisha kwa haraka mzaliwa huyo wa Afrika Kusini. Musk, baba wa watoto saba, anatajwa kuwa mtu anayetajirika kwa kasi zaidi katika historia ya utajiri na matajiri duniani.

Hizi mambo za hisa sasa inabidi kujifunza kwa nguvu.

By Dr.Christopher Cryrilo
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,253
2,000
HILI JAMBO NILILITEGEMEA SANA KWA ELON KUWA PALE JUU ILA AMENISHANGAZA SANA KACHUKUA MUDA MFUPI SANA KUFIKA PALE.

JAMAA ANA PROJECT ZA PESA NYONGI MNOOOO NDO MANA SIO AJABU KUFIKIA MAFANIKIO HAYO.
 
Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
1,866
2,000
Bill Gates nafasi ya 3 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 132 za kimarekani
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,002
2,000
Mwanzilishi, Mkurugenzi Mkuu, Fundi Mkuu na Mbunifu Mkuu wa kampuni ya SpaceX inayojihusisha na utengenezaji wa vyombo vya kusafiri na kufanya uchunguzi katika anga za mbali; pia mwekezaji na Mkurugenzi Mkuu na Fundi Mkuu katika kampuni ya kutengeneza magari ya umeme -Tesla; pia mwanzilishi wa kampuni ya Boring (The Boring Company) inayojihusisha na uchimbaji matanuri na mahandaki kwa ajili ya usafiri wa magari na treni; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Neuralink inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kupandikiza kwenye ubongo na kuufanya ubongo uweze kuwasiliana na 'computer'; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni (ya kujitolea) ya OpenAI inayojihusisha na tafiti za kiteknolojia - Ellon Musk ametangazwa kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani.

Elon Musk alizaliwa jijini Pretoria nchini Afrika kusini mnamo mwaka 1971. Kwakuwa baba yake ni raia wa Afrika Kusini wakati mama yake ni raia wa Canada, Musk alipatiwa Uraia wa nchi hizo mbili; Afrika Kusini na Canada. Akiwa na miaka 17 alihamia nchini Canada na kujiunga na chuo kikuu cha Queens, lakini miaka miwili baadaye alihamia nchini Marekani na kijiunga na chuo kikuu cha Pennislvania. Hapo alifanikiwa kuvuna shahada mbili kwa pamoja; shahada ya Uchumi na shahada ya sayansi katika tawi la Fizikia.
Mwaka 1992 alipatiwa uraia wa Marekani na kuwa mtu mwenye uraia wa nchi tatu; Afrika Kusini, Canada na Marekani.

Mwaka 1995 alihamia jimboni California kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) katika masomo ya fizikia na sayansi ya nyenzo kwenye Chuo Kikuu cha Stanford, lakini baada ya siku mbili tu aliachana na masomo ya uzamivu na kuanza kujihusisha na biashara.

Akawa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Zip2 iliyokuwa ikitengeneza programu pepe za tovutini (web softwares). Mwaka 1999 kampuni hiyo ya Zip2 ilinunuliwa na kampuni maarufu ya Compaq kwa dola za kimarekani million 307. Baadaye Musk alianzisha kampuni ya X.com ambayo ni benki ya mtandaoni (online bank). Katikati ya mwaka 2002 kampuni ya X.com iliungana na kampuni ya Confinity na kupata kampuni mpya ya PayPal, ambayo Oktoba 2002 ilinunuliwa na kampuni ya eBay kwa dola za kimarekani bilioni 1.5

Kabla ya kuuza PayPal, Musk alikwisha anzisha kampuni ya SpaceX miezi mitano nyuma; mei 2002. Mwaka 2004 Musk aliomba kujiunga na kampuni ya Tesla Motors, Inc. (sasa Tesla, Inc) ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka mmoja nyuma, akawa mbunifu magari katika kampuni hiyo. Mwaka 2008 akawa mkurugenzi mkuu wa Tesla, Inc.

Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2020 Ellon Musk alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 27, akiwa nje ya watu 50 tajiri zaidi duniani. Lakini ndani ya kipindi cha miezi 12, Musk amevuna zaidi ya dola bilioni 150, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko utajiri wa Bill Gates aliovuna kwa maisha yake yote. Sasa Ellon Musk ana utajiri wa dola 185 za kimarekani, amempiku Jeff Bezo aliyekuwa akishikiria nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na dola 184.
Kupanda sana kwa thamani ya hisa za kampuni la Tesla, Inc. kunatajwa kuwa moja ya sababu za kumtajirisha kwa haraka mzaliwa huyo wa Afrika Kusini. Musk, baba wa watoto saba, anatajwa kuwa mtu anayetajirika kwa kasi zaidi katika historia ya utajiri na matajiri duniani.

Hizi mambo za hisa sasa inabidi kujifunza kwa nguvu.

By Dr.Christopher Cryrilo

Daaaah Jamaa ana 49 Le mutuz anakimbilia 60.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
60,054
2,000
Kuna unabii kutoka Bible Africa itakuwa namba moja kiuchumi
Isaya 19:

21 Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
22 Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.
23 Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
24 Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia;
25 kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
 
Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,361

Andiko hili lina husiana vipi na post ya jamaa?
 
PNC

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
7,997

wasabato nimewavulia kofia
 
Hapo ametajwa Misri na sio Africa yote.Jitahidi kuelewa.
 
Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,921
2,000
wasabato nimewavulia kofia
Hakuna msabato mwenye mafundisho kama hayo. Wasabato wameshaaminishwa kupitia vitabu vya mwana mama Ellen White kuwa, hakuna taifa litakaloibuka duniani na kuipiku Marekani.

Simply saying, wasabato wanaamini kuwa Marekani ndilo taifa la mwisho kuwa na uchumi na sauti duniani
 
East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,829
2,000
Kuna unabii kutoka Bible Africa itakuwa namba moja kiuchumi
Isaya 19:

21 Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
22 Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.
23 Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
24 Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia;
25 kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
Na mir ndio nitakuwa tajiri nambali one
 
East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,829
2,000
Mbona amekaa wiki mbili tu namba moja kisha kawa namba mbili? Mbona kina Billgate walikaa namba moja kwa zaidi ya miaka?
Mdogo mdogo tu, atakaa hapo juu hadi wamchoke.. software zake hapo mbeleni zitaenda kuuzika kwenye company nyingi sana za magari ya umeme.. na sehemu zingine
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom