Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Akili yako ndo ya kupima! Umewahi kufanya utafiti kujua ni wanazuoni wangapi wa kiwango cha ubobezi ambao wanatoka katika mataifa ambayo kiingereza si lugha yao mama na bado wakafanikiwa sana kwenye maeneo yao ya umahiri? Amka dude..kiingereza ni lugha tu kama kimakua,kindali na kisambaa!
Kwa Tanzania Proffessor ni lazima ajue Kiingereza vizuri kwakuwa wanasomea kwa lugha hiyo.
 
Utumwa ni mbaya sana. Na huu utumwa uko hasa Afrika

Huwezi kuona Wajerumani, Wafaransa, Wachina, Wajapan, Warusi wakiwalaumu wenzao kwa kushindwa kuongea Kiingereza fasaha

Engineers wa China wakija Bongo kwenye miradi ye ujenzi wanaongea Kichina wanawatafuta translators wa Kiswahili.
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
ecademic qualification haiwezi kukufanya uwe na ujuzi mzuri wa kuongea ngeli ya hadharani (verbal communication skills)
 
Mnaleta uharo tu kujustify ujinga, profesa hata awe wa kiswahili anaprofess nini sasa kama hajui lugha zingine za kimataifa? Ujinga tu umetukalia kutafuta sababu za kujitetea kulinda upumbavu wetu! So kama ni profesa wa kiswahili akikutana na profesa wa English akajifiche chooni? Na hayo malinguistics na masemantics anajifunza kutoka kwa msukuma (Mb) then afundishe watoto wetu? Kweli ujinga mzigo mkubwa sana na uapodomia hautatuacha (Mtikila C., N.D)
 
Mleta mada ana hoja asikiizwe. HAIWEZEKANI USOME KIINGLISH TOKA UKIWA DARASA LA 3 HADI LEVO YA UDOKTA AU PhD halafu ni mbongo na et hujui hiyo lugha mleta mada usikilizweee
hata ukisoma level zote kwa kiswahili, unaweza ukawa na poor verbal and written swahili skills
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Ona huyu mbumbumbu bado anajua kuongea kiingereza ndio Elimu. Watu wa aina hii ndio mtaji mkubwa wa Braza K
 
Mleta mada ana hoja asikiizwe. HAIWEZEKANI USOME KIINGLISH TOKA UKIWA DARASA LA 3 HADI LEVO YA UDOKTA AU PhD halafu ni mbongo na et hujui hiyo lugha mleta mada usikilizweee
Kama mleta mada anasema hivyo basi yeye ndio muongo kwa sababu haiwezekani uweze kufika level hiyo ya elimu halafu et uwe hujui lugha iliyokuwa inayotumika kufundishiwa.
 
Kwanini hajatumia kiswahili ikiwa anajua Ana poor verbal communication skills .
 
Mnaleta uharo tu kujustify ujinga, proesaf hata awe wa kiswahili anaprofess nini sasa kama hajui lugha zingine za kimataifa? Ujinga tu umetukalia kutafuta sababu za kujitetea kulinda upumbavu wetu! So kama ni profesa wa kiswahili akikutana na profesa wa English akajifiche chooni? Na hayo malinguistics na masemantics anajifunza kutoka kwa msukuma (Mb) then afundishe watoto wetu? Kweli ujinga mzigo mkubwa sana na uapodomia hautatuacha (Mtikila C., N.D)
kiswahili chenyewe hatuko vizuri kuongea na kukiandika vizuri, je ni ujanja na kuwa proficiency njema ya lugha ya kigeni ambayo ni wachache sana wanielewa?.. hiyo ngeli kwa TZ ilikuwa ni academic tool tu.
 
Kama mleta mada anasema hivyo basi yeye ndio muongo kwa sababu haiwezekani uweze kufika level hiyo ya elimu halafu et uwe hujui lugha iliyokuwa inayotumika kufundishiwa.
ngeli ni tool ya kufundishia, so profiency yake ipo kwenye jargon za taaluma tu, na ukiajiriwa serikalini lugha ya mawasiliano ni kiswahili, so ni kwaida msomi kuwa na ngelii mbaya ya kuongea kwa public
 
Back
Top Bottom