Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha mbili

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,327
8,243
Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha baada ya miaka 7 kuanzia kidato cha kwanza.

Hapo juu ni mada:
Karibuni tujadili kiundani:
Mimi nitatoa highlights zangu chache hapa:

Kuanzia kidato cha kwanza wanafunzi wanabadirishiwa mfumo wa lugha ya kujifunzia kutoka kiswahili na kuanza kutumia kiingereza.

Wanaanza darasa la nane (8) (kidato cha kwanza) kama darasa la kwanza, wanaanza kupambana na lugha na kushika vitu wasivyo vielewa ili kuokoa muda. Wanaweza kutumia hata miaka minne yote wanashika tu vitu hawaelewi kiundani.

Walimu wanaita kushika point,

Mwanafunzi wa Marekani, China, Kenya, Urusi, Uganda, yeye anapofika darasa la nane hahitaji kukariri vitu asivyovielewa kwasababu tayali yeye alishaizoea lugha kila kitu anakwendwa kwa kuelewa. Hii ndio faida ya kutumia lugha moja kuanzia darasa la kwanza.

Hapo ilitakiwa waendelee na lugha ile ile waliyoizoea kuanzia darasa la kwanza.

Naweza kusema hapo kuanzia kidato cha kwanza ndipo uharibifu wa elimu yetu unapoanzia. Mtu hawezi kufanya vumbuzi kama wanazofanya wenzetu kwa kuwa na mfumo kama huo unaochanganya lugha mbili kwenye elimu. Inatakiwa tuwe systematic tuchague lugha moja ya kufundishia ndipo tutaweza kushindana na mataifa mengine katika elimu.

Note:
Wakuu tunapojadili hii mada tusisahau kwamba, lugha tunayo izungumzia ni lugha ya kujifunzia na kujibia mitihani. Tukumbuke lugha ndio nyenzo inayotumika kuhamisha Maarifa kutoka kwenye vitabu kuingiza kichwani. Je tunauhakika watoto wetu wanaelewa vitabu au wanajisomea point tu. Je tunauhakika wanaelewa concept ipasavyo au wanazikariri tu kwasababu hawawezi kuelewa sababu ya lugha.

Reference.
 
Sawa meneja
Point yako I naweza kuwa na ukweli Kwa asilimia isizidi 40%. Kwa sababu lugha ni tools inayotumika kuchukuwa Au kutafuta elimu.
Lakini elimu na lugha ni vitu viwili tofauti, Unaweza kujua lugha lakini ukawa huna elimu na Unaweza kuwa na elimu ukawa huna lugha, Ila haitokuzuia kuifanyia kazi elimu yako.
Mfano Unaweza kusoma katika nchi ya China Kwa kutumia kichana lakini unapokuja Tanzania ukatakiwa usomeshe wanafunzi Kwa kiswahili kupitia ulichokisoma China, kama nikweli elimu uliosomea China uliipata vizuri hutoshindwa kuisomesha Kwa kiswahili.
Conclusion.
Lugha ni Muhimu lakini haijastifiy kuwa wa Tanzania kushindwa kuitumia elimu zao katika kufanya utafiti ukiwemo wa kusayansi, kuwa kumesababishwa na kuchanganya lugha.
 
Pamoja na changamoto ya lugha, jamii yetu haina umakini kwenye mambo ya msingi. Tumekuwa tunasogeza siku tu. Mwalimu anayefundisha ni zao la kufeli, hajui lugha wala uelewa sahihi wa anachofundisha. Anayefundishwa hata akiwa na ndoto kubwa vipi, vikwazo vipo vingi Sana vya kumkwamisha njiani. Mwishowe tunaishia na mkubwa wa taasis ya utafiti wa tiba, mwanasayansi wa PhD mwenye mtazamo sawa na Polepole na Gwajima kwenye chanjo zilitotengenezwa na wanasayansi wenzake duniani, pengine ambao hata PhD hawana.
 
Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha baada ya miaka 7 kuanzia kidato cha kwanza.

Hapo juu ni mada:
Karibuni tujadili kiundani:
Mimi nitatoa highlights zangu chache hapa:

Kuanzia kidato cha kwanza wanafunzi wanabadirishiwa mfumo wa lugha ya kujifunzia kutoka kiswahili na kuanza kutumia kiingereza.

Wanaanza darasa la nane (8) (kidato cha kwanza) kama darasa la kwanza, wanaanza kupambana na lugha na kushika vitu wasivyo vielewa ili kuokoa muda. Wanaweza kutumia hata miaka minne yote wanashika tu vitu hawaelewi kiundani.

Walimu wanaita kushika point,

Mwanafunzi wa Marekani, China, Kenya, Urusi, Uganda, yeye anapofika darasa la nane hahitaji kukalili vitu asivyovielewa kwasababu tayali yeye alishaizoea lugha kila kitu anakwendwa kwa kuelewa. Hii ndio faida ya kutumia lugha moja kuanzia darasa la kwanza.

Hapo ilitakiwa waendelee na lugha ile ile waliyoizoea kuanzia darasa la kwanza.

Naweza kusema hapo kuanzia kidato cha kwanza ndipo uharibifu wa elimu yetu unapoanzia. Mtu hawezi kufanya vumbuzi kama wanazofanya wenzetu kwa kuwa na mfumo kama huo unaochanganya lugha mbili kwenye elimu. Inatakiwa tuwe systematic tuchague lugha moja ya kufundishia ndipo tutaweza kushindana na mataifa mengine katika elimu.
Hilio la mwingiliano was lugha mbili liondoe , ila utayari was kisiasa au wanauita political will, ndio shida na zaidi hii yote ikichangiwa na uvivu wa matumizi ya akili na badala yake tumbo hufikiriwa kwanza Kwa ulafi na ubinafsi wa mwafrika na zaidi Mtanzania
 
Marekani ,ulaya na Japan wagunduzi wa teknolojia sio wanasiasa hilo la political will ha li apply!!! Ni tatizo letu waafrika Kama watu binafsi!!!
 
Pamoja na changamoto ya lugha, jamii yetu haina umakini kwenye mambo ya msingi. Tumekuwa tunasogeza siku tu. Mwalimu anayefundisha ni zao la kufeli, hajui lugha wala uelewa sahihi wa anachofundisha. Anayefundishwa hata akiwa na ndoto kubwa vipi, vikwazo vipo vingi Sana vya kumkwamisha njiani. Mwishowe tunaishia na mkubwa wa taasis ya utafiti wa tiba, mwanasayansi wa PhD mwenye mtazamo sawa na Polepole na Gwajima kwenye chanjo zilitotengenezwa na wanasayansi wenzake duniani, pengine ambao hata PhD hawana.
Point yako ingeweza kuwa na maana nzuri sema imeharibiwa na kuwashambulia watu badala ya hoja zao.
 
Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha baada ya miaka 7 kuanzia kidato cha kwanza.

Hapo juu ni mada:
Karibuni tujadili kiundani:
Mimi nitatoa highlights zangu chache hapa:

Kuanzia kidato cha kwanza wanafunzi wanabadirishiwa mfumo wa lugha ya kujifunzia kutoka kiswahili na kuanza kutumia kiingereza.

Wanaanza darasa la nane (8) (kidato cha kwanza) kama darasa la kwanza, wanaanza kupambana na lugha na kushika vitu wasivyo vielewa ili kuokoa muda. Wanaweza kutumia hata miaka minne yote wanashika tu vitu hawaelewi kiundani.

Walimu wanaita kushika point,

Mwanafunzi wa Marekani, China, Kenya, Urusi, Uganda, yeye anapofika darasa la nane hahitaji kukalili vitu asivyovielewa kwasababu tayali yeye alishaizoea lugha kila kitu anakwendwa kwa kuelewa. Hii ndio faida ya kutumia lugha moja kuanzia darasa la kwanza.

Hapo ilitakiwa waendelee na lugha ile ile waliyoizoea kuanzia darasa la kwanza.

Naweza kusema hapo kuanzia kidato cha kwanza ndipo uharibifu wa elimu yetu unapoanzia. Mtu hawezi kufanya vumbuzi kama wanazofanya wenzetu kwa kuwa na mfumo kama huo unaochanganya lugha mbili kwenye elimu. Inatakiwa tuwe systematic tuchague lugha moja ya kufundishia ndipo tutaweza kushindana na mataifa mengine katika elimu.
Unaujua mfumo wa elimu wa China?Hongkong ? Au hata Marekani majiimbo kama Texas na majimbo yenye idadi kubwa ya watumiaji wa kispania na kichenku? Poland je? Russia na.North Korea? Even South? To cut it short kujua ama kufundishwa kwa Kiingereza bila maarifa haina tofauti na kizaramo tena Bora ya kizaramo ama kimatumbi

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Marekani ,ulaya na Japan wagunduzi wa teknolojia sio wanasiasa hilo la political will ha li apply!!! Ni tatizo letu waafrika Kama watu binafsi!!!
Nilichomuelewa haraka haraka ni kwamba maamuzi ya kisiasa au kutoka kwa wanasiasa ndio yanayoathiri elimu yetu.
Wanasiasa wanatumia elimu ya yetu kufanya siasa au kupata uungwaji mkono katika siasa/chaguzi za kisiasa,
Mfano matokeo ya mitihani yanatumika katika kuombea kura kwa wapiga kura.
 
Marekani ,ulaya na Japan wagunduzi wa teknolojia sio wanasiasa hilo la political will ha li apply!!! Ni tatizo letu waafrika Kama watu binafsi!!!
Hapo ndipo tunapolaumu upungufu wa matunizi ya akili. Niambie mbunge ni mwanasiasa au mwanasayansi? Ni nani mtunga sera, na ni nani anayeidhinisha bajeti ya kutekeleza sera za taifa.
 
Bill Gates kugundua Microsoft products zake bajeti hakupewa na serikali Wala Toyota hakupewa na serikali au mwanasiasa!!!

Hata wewe ruksa kugundua chako na kukiuza hakuna bajeti utapewa ugundue Wala hakuna sera ya kikuzuia usigundue Tukubali tu vichwa vyetu watu weusi vitupu havina kitu ndio maana hatugundui kitu
 
Mbona kuna wabongo wameenda kusoma Japan kwa Kijapani na wanafanya mambo makubwa ya kiubunifu ?

Yaani ni mtu aliyesoma Kiswahili shule ya msingi, akaingia Sekondari na Chuo kwa kiswahili na kwenda elimu ya juu zaidi kusoma kwa Kijapani.

Tatizo letu ni kubwa zaidi ya lugha.
 
Bill Gates kugundua Microsoft products zake bajeti hakupewa na serikali Wala Toyota hakupewa na serikali au mwanasiasa!!!

Hata wewe ruksa kugundua chako na kukiuza hakuna bajeti utapewa ugundue Wala hakuna sera ya kikuzuia usigundue Tukubali tu vichwa vyetu watu weusi vitupu havina kitu ndio maana hatugundui kitu
Acha kukariri mazingira ya bill gates huwezi kuyafananisha na mazingira ya kazuramimba hata kama unawazo mazingira haya yanaua wazo lenyewe .
 
Ulichoandika sio kweli Tanzania Kuna maelfu ya watoto wanaanza kusoma kiingereza English medium kuanzia chekechea hadi shule za msingi darasa la saba
Kweli kabisa. Ambacho anapaswa kuelewa mtoa mada ni kwamba elimu ni matokeo ya mfumo mzima wa maisha ya jamii ama nchi husika.

Mzazi anampeleka shule mtoto lkn yeye mwenyewe anavyoishi na huyo mtoto hachqngii chochote kwenye kumpa maarifa huyo mtoto. Mtoto akifika shule anakutana na mwalimu ambaye kazi yake ni kumkaririsha notes mtoto.

Mtoto akienda mtaani anakutana na watu wanaishi kimagumashi siyo kwa kutumia akili na ujuzi.
 
Point yako I naweza kuwa na ukweli Kwa asilimia isizidi 40%. Kwa sababu lugha ni tools inayotumika kuchukuwa Au kutafuta elimu.
Lakini elimu na lugha ni vitu viwili tofauti, Unaweza kujua lugha lakini ukawa huna elimu na Unaweza kuwa na elimu ukawa huna lugha, Ila haitokuzuia kuifanyia kazi elimu yako.
Mfano Unaweza kusoma katika nchi ya China Kwa kutumia kichana lakini unapokuja Tanzania ukatakiwa usomeshe wanafunzi Kwa kiswahili kupitia ulichokisoma China, kama nikweli elimu uliosomea China uliipata vizuri hutoshindwa kuisomesha Kwa kiswahili.
Conclusion.
Lugha ni Muhimu lakini haijastifiy kuwa wa Tanzania kushindwa kuitumia elimu zao katika kufanya utafiti ukiwemo wa kusayansi, kuwa kumesababishwa na kuchanganya lugha.
Meneja kasema ndugu
 
Wanafunzi wenyewe wamechanganyikiwa na maisha
Ukitaka kujua Hilo fuatilia wakati wanaenda shule na kutoka kupitia magari Yao maalumu wanayoyajua ,, utajua kama walishachanganyikiwa zamani, achilia mbali mfumo wetu wa elimu na changamoto zake,ikiwa ni pamoja na utayari wetu kuona mfumo wetu unatengeneza watu sahihi kulisaidia taifa baadae.Jaribu kulinganisha mfumo wetu na wenzetu tukianzia TU na baadhi ya majirani zetu makini kabla ya kuifikiria ulaya ,Amerika ,uchina na urusi.
 
Hilo no kweli. Mtu aliyekariri hawezi kuwa mbunifu. Na huu mfumo wa kusoma kwa kiingereza kuanzia sekondari hauna usawa, unawapendelea matajiri na kuwaweka maskini katika disadvantage.
 
Back
Top Bottom