Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha mbili

Hilo no kweli. Mtu aliyekariri hawezi kuwa mbunifu. Na huu mfumo wa kusoma kwa kiingereza kuanzia sekondari hauna usawa, unawapendelea matajiri na kuwaweka maskini katika disadvantage.
Swali la kujiuliza kwanini sisi masikini? Kwani uchina hawakuwa masikini, kwani uingereza na marekani hawakuwa masikini, waliwezaje kufikia mapinduzi ya viwanda na kuweza kujiendeleza katika maeneo yote, najua mwingine atasema walifikia huko kupitia unyonyaji na utumwa Kwa waafrika, ila tujiulize, kwanini na Afrika hatukuweza kuwa na makoloni yetu ulaya , Amerika na Asia, mbali na utajiri waliouiba wasia, waamerika na uchina wakatosheka na wakaonawatupe uhuru?
 
Hili ni somo refu la kusoma mavitabu kabisa.
 
Meneja kasema ndugu
Mkuu lugha tunayo izungumzia ni lugha ya kujifunzia na kujibia mitihani. Tukumbuke lugha ndio nyenzo inayotumika kuhamisha Maarifa kutoka kwenye vitabu kuingiza kichwani. Je tunauhakika watoto wetu wanaelewa vitabu au wanajisomea point tu.
 
Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha baada ya miaka 7 kuanzia kidato cha kwanza.

Hapo juu ni mada:
Karibuni tujadili kiundani:
Mimi nitatoa highlights zangu chache hapa:

Kuanzia kidato cha kwanza wanafunzi wanabadirishiwa mfumo wa lugha ya kujifunzia kutoka kiswahili na kuanza kutumia kiingereza.

Wanaanza darasa la nane (8) (kidato cha kwanza) kama darasa la kwanza, wanaanza kupambana na lugha na kushika vitu wasivyo vielewa ili kuokoa muda. Wanaweza kutumia hata miaka minne yote wanashika tu vitu hawaelewi kiundani.

Walimu wanaita kushika point,

Mwanafunzi wa Marekani, China, Kenya, Urusi, Uganda, yeye anapofika darasa la nane hahitaji kukariri vitu asivyovielewa kwasababu tayali yeye alishaizoea lugha kila kitu anakwendwa kwa kuelewa. Hii ndio faida ya kutumia lugha moja kuanzia darasa la kwanza.

Hapo ilitakiwa waendelee na lugha ile ile waliyoizoea kuanzia darasa la kwanza.

Naweza kusema hapo kuanzia kidato cha kwanza ndipo uharibifu wa elimu yetu unapoanzia. Mtu hawezi kufanya vumbuzi kama wanazofanya wenzetu kwa kuwa na mfumo kama huo unaochanganya lugha mbili kwenye elimu. Inatakiwa tuwe systematic tuchague lugha moja ya kufundishia ndipo tutaweza kushindana na mataifa mengine katika elimu.

Reference.

Tanzania kinachotuangusha sio lugha. Ni utamaduni. We are docile society! That cultural practices are simply suicidal. Unless we change.
 
Back
Top Bottom