SoC02 Elimu ya Mahusiano ianze kutolewa shuleni

Stories of Change - 2022 Competition

ReTHMI

Senior Member
Jul 17, 2022
181
318
Wengi watapigwa na butwaa kwanini natamani elimu ya mahusiano itolewe mashuleni tena mahusiano ya kimapenzi. Nitabaki kusimamia kwamba elimu ya mahusiano ya kimapenzi itolewe mashuleni, ikiwezekana kama somo la lazima kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka elimu ya sekondari.

Elimu inatakiwa isaidie katika kupambana na matatizo yanayoikumba jamii. Katika jamii zetu mahusiano yanasababisha madhara kila uchwao na kuvipamba vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari na mitandao. Imefikia hatua watu wanaweka mzaha kwenye matukio ambayo yamegharimu maisha ya watu. Ila cha kusikitisha hakuna nguvu inayoelekezwa katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.

Zama zilizopita vijana walifunzwa jinsi ya kuishi kwenye ndoa na kutimiza majukumu yao kwenye familia kupitia jando na unyago. Zama hizi utamaduni huu umekufa, tumeshindwa kuendeleza kwa kuboresha mazuri na kuyaacha mabaya yaliyokua yanafanyika kwenye jando na unyago.

Ukosefu wa elimu ya mahusiano unapelekea jamii kukumbana na athari nyingi zitokanazo na mahusiano;
Watu wanakufa, wanauwawa na wenza wao au watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi.

Ukatili wa kijinsia umeongezeka maradufu kwenye ndoa na mahusiano. Watu wanapata ulemavu kutokana na vipigo na kushambuliwa na wenza wao.

Magonjwa ya ngono, watoto wa mitaani, utoaji wa mimba, mimba katika umri mdogo, watoto kulelewa na mzazi mmoja (single mother) yote haya yanaongezeka kila uchwao.

Afya ya akili imedorora miongoni mwa watu wengi, wameathirika kisaikolojia kutokana na maumivu waliyopitia/wanayopitia kwenye mahusiano hali inayopelekea wengine kuwehuka kabisa.

Takwimu za kwenye chapisho la BBC la tarehe 1 Juni 2022 zinabainisha;
Kituo cha Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania, LHRC, kwa mwaka 2017, kilikusanya matukio makubwa 13 na mwaka 2020 matukio yaliongezeka mpaka 39 yaliyotokana na wivu wa kimapenzi. Lakini kituo hicho kinasema mwezi Mei pekee mwaka huu (2022), kumeripotiwa matukio 7 ya mauaji yatokanayo na wivu wa kimapenzi huku mwaka 2021 kuliripotiwa kuwa na mauaji ya ina hiyo 35, ambapo wanaume waliouawa walikuwa 4 na wanawake 31 sawa na asilimia 89%.
Pia katika chapisho la DW la tarehe 24/01/2022, linalozungumzia kuhusiana na ukatili wa kijinsia linaonyesha;
Ripoti iliyotolewa Septemba 2021 na Jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia Tanzania miongoni mwa wanandoa, imeonyesha kuwa, asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kijinsia, ambapo asilimia 36 walifanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 walifanyiwa ukatili wa kingono.
Kwenye suala la mimba na ndoa za utotoni zinashuhudiwa pia katika jamii zetu ikiwemo kupelekea watoto kukatiza masomo yao. Kwa mujibu wa takwimu za Unicef za kati ya mwaka 2010 na 2017;
Tanzania ni ya tatu kwa kuwa na viwango vya juu vya ndoa za utotoni baada ya Sudan Kusini na Uganda. Sudan Kusini kiwango cha watoto wa chini ya miaka 18 wanaoozwa ni asilimia 52 na nchini Uganda ni asilimia 40 na Tanzania ni asilimia 31.
Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko mei 19,2022 alibainisha kuwa,
“Hali ya maambukizi ya UKIMWI nchini Tanzania inaonyesha kuwa kama nchi tunapiga hatua kubwa, makadirio ya takwimu kwa mwaka 2021 yanaonyesha kwamba maambukizi mapya ni watu 54,000 kwa mwaka huku, upande wa vifo vimeshuka kutoka watu 32,000 mwaka 2020 hadi watu 29,000 mwaka 2021” (Chanzo cha habari, Mtanzania digital).
Inaonekana maambukizi mapya ya UKIMWI yameshuka ila bado ni mengi. Kwa asilimia kubwa maambukizi ya UKIMWI yanatokana kushiriki ngono zembe mbali na njia nyingize zinachochangia maambukizi kwa asilimia chache.

Kupitia takwimu hizi chache inaonyesha ni jinsi gani jamii inahitaji msaada wa dharura na wa muda mrefu ili kutengeneza msingi imara utakaosaidia kuimarisha mahusiano ya mapenzi. Wengi huchukulia kawaida na hata kuweka utani pale wengine wanapokumbana na madhara yatokanayo na mahusiano ya mapenzi. Ila wanashindwa kuyakwepa yanapowafika wao kutokana na ukosefu wa elimu ya mahusiano.

Hivyo basi, kutolewa kwa elimu ya mahusiano shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hili. Hii ni kutokana na watu wengi pindi wanapomaliza elimu yao hupuuzia kujifunza mambo mapya, hata zinapoandaliwa semina mbalimbali ushiriki ni hafifu sana.

Wapo wanaochukulia kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ni kumharibu kabisa mtoto. Zipo njia nzuri na zinazofaa kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ambazo ni tofauti na zile zitakazotumiaka kumfundisha mtu mzima. Watoto pia wanahitaji elimu hii kwasababu nao pia ni waathiriwa wakubwa wa mahusiano ya kimapenzi. Ikiwemo kukatiziwa masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Ila pia kupitia michezo yao watoto hucheza michezo ambayo huigiza kama familia inadhihirisha ni jinsi gani nao wanahitaji elimu hii ya mahusiano kwakua nao wanayashuudia yanayotendeka kwenye jamii zao hali inayopelekea kuyaakisi wanapokua watu wazima.

Elimu ya mahusiano ikitolewa mashuleni itapunguza vifo vitokanavyo na wivu wa kimapenzi na ukatili wa kijinsia. Hii ni kwasababu watu watafundishwa uaminifu kwenye mahusiano, na uaminifu utapunguza migogoro kwenye mahusiano. Ila pia wataweza kutambua yapi ni mahusiano sahihi na yapi sio sahihi. Watatambua njia za kutumia kutatua migogoro kwenye mahusiano bila kumuumiza mwingine.

Itasaidia kupunguza maambukizi wa UKIMWI kutokana na ngono zembe. Watu wengi wanaingia kwenye mahusiano bila kupima virusi vya UKIMWI, wakiamini kwamba kua na afya nzuri basi mtu hana maambukizi ya UKIMWI. Elimu hii itawasaidia kutambua kwamba UKIMWI haupimwi kwa macho, mtu anaweza akaonekana mzuri kiafya ila ana maambukizi hivyo ni vyema kutumia njia zitakazomkinga. Pia itasaidia watu kuwa waaminifu kwenye mahusiano ikiwemo kutokua na michepuko.

Elimu ya mahusiano ikitolewa vizuri shuleni itawasaidia pia wanafunzi kutimiza malengo yao ya kimasomo. Hasahasa kwa upande wa wanafunzi wa kike wanaokatiza masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Hii ni kwa sababu wanafunzi watatambua ni kwa namna gani mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuathiri masomo. Pia wataelekezwa ni wakati upi sahihi wa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwisho kabisa, nipende kusema ni bora kutatua tatizo kwa kulishughulikia kuliko kuacha tatizo litutafune kwa kulionea aibu. Ni dhairi kua japokua mahusiano ya kimapenzi yanachangamoto nyingi sana ila hakuna maisha bila mahusiano ya kimapenzi. Ili kupunguza changamoto hizi basi serikali ikae na itafakari kwa kina ni kwa namna gani iliyo bora wanaweza kuandaa somo kuhusu mahusiano litakalofundishwa shuleni. Hii ni kwa minajili tu ya kulikomboa taifa kutokana na nguvu kazi zinazopotea kutokana na mahusiano ya kimapenzi.
 
Wengi watapigwa na butwaa kwanini natamani elimu ya mahusiano itolewe mashuleni tena mahusiano ya kimapenzi. Nitabaki kusimamia kwamba elimu ya mahusiano ya kimapenzi itolewe mashuleni, ikiwezekana kama somo la lazima kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka elimu ya sekondari.

Elimu inatakiwa isaidie katika kupambana na matatizo yanayoikumba jamii. Katika jamii zetu mahusiano yanasababisha madhara kila uchwao na kuvipamba vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari na mitandao. Imefikia hatua watu wanaweka mzaha kwenye matukio ambayo yamegharimu maisha ya watu. Ila cha kusikitisha hakuna nguvu inayoelekezwa katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.

Zama zilizopita vijana walifunzwa jinsi ya kuishi kwenye ndoa na kutimiza majukumu yao kwenye familia kupitia jando na unyago. Zama hizi utamaduni huu umekufa, tumeshindwa kuendeleza kwa kuboresha mazuri na kuyaacha mabaya yaliyokua yanafanyika kwenye jando na unyago.

Ukosefu wa elimu ya mahusiano unapelekea jamii kukumbana na athari nyingi zitokanazo na mahusiano;
Watu wanakufa, wanauwawa na wenza wao au watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi.

Ukatili wa kijinsia umeongezeka maradufu kwenye ndoa na mahusiano. Watu wanapata ulemavu kutokana na vipigo na kushambuliwa na wenza wao.

Magonjwa ya ngono, watoto wa mitaani, utoaji wa mimba, mimba katika umri mdogo, watoto kulelewa na mzazi mmoja (single mother) yote haya yanaongezeka kila uchwao.

Afya ya akili imedorora miongoni mwa watu wengi, wameathirika kisaikolojia kutokana na maumivu waliyopitia/wanayopitia kwenye mahusiano hali inayopelekea wengine kuwehuka kabisa.

Takwimu za kwenye chapisho la BBC la tarehe 1 Juni 2022 zinabainisha;

Pia katika chapisho la DW la tarehe 24/01/2022, linalozungumzia kuhusiana na ukatili wa kijinsia linaonyesha;

Kwenye suala la mimba na ndoa za utotoni zinashuhudiwa pia katika jamii zetu ikiwemo kupelekea watoto kukatiza masomo yao. Kwa mujibu wa takwimu za Unicef za kati ya mwaka 2010 na 2017;

Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko mei 19,2022 alibainisha kuwa,

Inaonekana maambukizi mapya ya UKIMWI yameshuka ila bado ni mengi. Kwa asilimia kubwa maambukizi ya UKIMWI yanatokana kushiriki ngono zembe mbali na njia nyingize zinachochangia maambukizi kwa asilimia chache.

Kupitia takwimu hizi chache inaonyesha ni jinsi gani jamii inahitaji msaada wa dharura na wa muda mrefu ili kutengeneza msingi imara utakaosaidia kuimarisha mahusiano ya mapenzi. Wengi huchukulia kawaida na hata kuweka utani pale wengine wanapokumbana na madhara yatokanayo na mahusiano ya mapenzi. Ila wanashindwa kuyakwepa yanapowafika wao kutokana na ukosefu wa elimu ya mahusiano.

Hivyo basi, kutolewa kwa elimu ya mahusiano shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hili. Hii ni kutokana na watu wengi pindi wanapomaliza elimu yao hupuuzia kujifunza mambo mapya, hata zinapoandaliwa semina mbalimbali ushiriki ni hafifu sana.

Wengine watahisi labda kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ni kumharibu kabisa. Zipo njia nzuri na zinazofaa kumfundisha mtoto juu ya mahusiano ya kimapenzi ambazo ni tofauti na zile zitakazotumiaka kumfundisha mtu mzima. Watoto pia wanahitaji elimu hii kwasababu nao pia ni waathiriwa wakubwa wa mahusiano ya kimapenzi. Ikiwemo kukatiziwa masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Ila pia kupitia michezo yao watoto hucheza michezo ambayo huigiza kama familia inadhihirisha ni jinsi gani nao wanahitaji elimu hii ya mahusiano kwakua nao wanayashuudia yanayotendaka kwenye jamii zao hali inayopelekea kuyaakisi wanapokua watu wazima.

Elimu ya mahusiano ikitolewa mashuleni itapunguza vifo vitokanavyo na wivu wa kimapenzi na ukatili wa kijinsia. Hii ni kwasababu watu watafundishwa uaminifu kwenye mahusiano, na uaminifu utapunguza migogoro kwenye mahusiano. Ila pia wataweza kutambua yapi ni mahusiano sahihi na yapi sio sahihi. Watatambua njia za kutumia kutatua migogoro kwenye mahusiano bila kumuumiza mwingine.

Itasaidia kupunguza maambukizi wa UKIMWI kutokana na ngono zembe. Watu wengi wanaingia kwenye mahusiano bila kupima virusi vya UKIMWI, wakiamini kwamba kua na afya nzuri basi mtu hana maambukizi ya UKIMWI. Elimu hii itawasaidia kutambua kwamba UKIMWI haupimwi kwa macho, mtu anaweza akaonekana mzuri kiafya ila ana maambukizi hivyo ni vyema kutumia njia zitakazomkinga. Pia itasaidia watu kuwa waaminifu kwenye mahusiano ikiwemo kutokua na michepuko.

Elimu ya mahusiano ikitolewa vizuri shuleni itawasaidia pia wanafunzi kutimiza malengo yao ya kimasomo. Hasahasa kwa upande wa wanafunzi wa kike wanaokatiza masomo yao kutokana na mimba na ndoa za utotoni. Hii ni kwa sababu wanafunzi watatambua ni kwa namna gani mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuathiri masomo. Pia wataelekezwa ni wakati upi sahihi wa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwisho kabisa, nipende kusema ni bora kutatua tatizo kwa kuliongelea kuliko kuacha tatizo litutafune kwa kulionea aibu. Ni dhairi kua japokua mahusiano ya kimapenzi yanachangamoto nyingi sana ila hakuna maisha bila mahusiano ya kimapenzi. Ili kupunguza changamoto hizi basi serikali ikae na itafakari kwa kina ni kwa namna gani iliyo bora wanaweza kuandaa somo kuhusu mahusiano litakalofundishwa shuleni. Hii ni kwa minajili tu ya kulikomboa taifa kutokana na nguvu kazi zinazopotea kutokana na mahusiano ya kimapenzi.
Andiko zuri sana hili.
 
Hiki kitu kinafanyika kwa baadhi ya nchi, ila kwa huku kwetu nadhani itakua ni vigumu sana
Ni ngumu lakini kama ikiwekwa mikakati mizuri ya kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu ya mahusiano shuleni inawezekana kabisa.
 
Pia haya yameshuhudiwa yakiongezeka kwenye jamii,
-Mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja
-Ufanyaji wa mapenzi kinyume na maumbile
-Ulawiti wa watoto wadogo
Haya yote ni kutokana na ukosefu wa elimu ya mahusiano.
 
1660322964499.png
 
Back
Top Bottom