Soma bila kupita , Kisha toa Maoni yako

professional ethics

Senior Member
Dec 24, 2023
108
352
Moja ya jambo serikali inatakiwa kutake kwa umakini sana ni eneo la mahusiano, naona kuwa serikali inatakiwa kuanzisha somo la mahusiano kuanzia primary hadi university level.

Naweza Sema mahusiano ni Kila kitu, vijana wengi wanapoteza dira ya maisha sababu hasa ukitazama ni eneo mahusiano, watu wanashidwa kufanya kazi kwa ukamirifu kwenye ofisi za Umma moja ya sababu ni eneo la mahusiano.

Tazama migogoro ya ndoa,watu wanauwana chanzo kikuu ni gap lilipo kwenye elimu na ufahamu wa mahusiano.

Hata haya mambo ya mapenzi ya jinsia moja, mambo ya wanaume kufanya mapenzi kupitia haja kubwa kwa wanawake naoana chanzo ni gap juu ya eneo la mahusiano

Kwa mjumuisho eneo la mahusiano linaweza kuamua hatima na ustawi wa taifa .
 
Malezi huanzia ngazi ya familia na jamii husika pamoja na mafundisho ya dini/imani. Serikali tutaionea hapa.
 
Zamani zilikuwepo kama 'informal education' Jando na Unyago huko vijana walipewa miongozo kulingana na mila na tamaduni za kabila husika.
Na athari chanya zinajulikana angalau kiasi chake wengine tulishuhudia na mengine kupitia simulizi za wazee tumesikia.


Nini kimeharibu,
1. Inter marriages (kuoa na kuolewa watu kutoka makabila mengine)
2. Kuhamia mijini
3. Elimu mpya za kutoka kwa watu weupe na ukuaji wa Teknolojia
4.Imani za Dini

Hayo yameleta mvurugano kila mmoja anabeba analotaka na kuweza.

Leo tupo hapa tumechanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom