Elimu ya bure kuhusu Azam TV

Elimu ya bure kuhusu Azam TV

msaada wapendwa.mwenzenu mpaka leo star tv siipati na huwa nalipia elfu ishirini cha television yote..naomba msaada wenu kwann star tv siipati na nimeshafanya auto search lakini wapi!inakuwaje wengine waekewe halafu wengine bado?
 
msaada jamani, Chanel 1tu ya morningstar inakataka sauti upande wa Continental zingine ziko poa. natumia rcv ya wiztech 8055

wiztech na continental ni kama paka na nyoka.. tafuta rcvr nyingine zaidi ya io.
 
Ph-25 sijaelewa ses@5 na amos@17 unaandikaje kusearch satellite, natumia WizTech 8030

hakuna cha kuandika apo mkuu apo ni kuchukua tp na kuingia windoni, anza na kuitafuta amos5 kama uko ndani ya beam,kisha juu kidogo sana ya io ku ya amos weka ku nyingine kwaajili ya ses@5

au chini ya mkono wa lnb yako kisha unga na disq kazi kwisha.
 
msaada wapendwa.mwenzenu mpaka leo star tv siipati na huwa nalipia elfu ishirini cha television yote..naomba msaada wenu kwann star tv siipati na nimeshafanya auto search lakini wapi!inakuwaje wengine waekewe halafu wengine bado?

Kama upo Dar, ni bora ubebe decorder yako uende nayo Azam tv. Maana naona Star tv inapatikana tu bila tatizo...
 
msaada wapendwa.mwenzenu mpaka leo star tv siipati na huwa nalipia elfu ishirini cha television yote..naomba msaada wenu kwann star tv siipati na nimeshafanya auto search lakini wapi!inakuwaje wengine waekewe halafu wengine bado?

We ipige factory default ikimaliza usikubali isachi yenyewe izime kisha washa itaanza na ku update software ikimaliza itajisearch yenyewe na star itaingia.
 
Naona tangazo hapa, Azam wameongeza bei za vifurushi kuanzia 1 Julai 2015. Mbona wanazidi kutuumiza?!
 
kwanza natoa pongezi kwa muanzishaji wa huu uzi
kuna frequency nilizipata kwenye google baada ya kuingiza nimepata chanel za zuku tatizo hazionyeshi picha inayo onyesha ni zuku zone
SWALI je hizi nyingine nikiset dish vizuri zinaweza onyesha au tatizo ni nini
 
msaada wapendwa.mwenzenu mpaka leo star tv siipati na huwa nalipia elfu ishirini cha television yote..naomba msaada wenu kwann star tv siipati na nimeshafanya auto search lakini wapi!inakuwaje wengine waekewe halafu wengine bado?

Hapa kwangu king'amuz cha azam kina side 3,redio then tv ambako unapata kina itv,eatv na tv kibao za nnje za kizungu then kuna side ya 3 ya menu uko pia kuna tv nyingi za kihindi na huko utamkuta star tv ndugu
 
Naona tangazo hapa, Azam wameongeza bei za vifurushi kuanzia 1 Julai 2015. Mbona wanazidi kutuumiza?!

Mimi pia nimepata ujumbe huo wa kuongeza bei za vifurushi. Kifurushi cha 10,000 ▶12,000 cha 15,000▶20,000 cha 20,000▶30,000. Hapo ni maumivu kwakweli. Ila wanetoa sababu za msingi, ongezeko la VAT na kushuka kwa sh. Yetu.
 
azam weka mbali na watoto. fta daimaaa

Mkuu sijakuelewa umemaanisha nini?? Samahani ni mgeni katika uzi nimeshawishika katika kununua kingamuzi cha Azam so nilikuwa naangalia maoni ya watu yakoje??

Maana ya FTA mkuu?? Naona hapa mnaelewana wenye kufahamu haya mambo. Samahani kwa usumbufu.
 
Swali Jengine. Tv yangu ina support HDMI na kingamuzi cha azam kina HDMI. Nikinunua waya wa HDMI channel zitaonekana vizuri zaidi au inakuwaje??
 
FTA means free to air yani channels za bure
 
Swali Jengine. Tv yangu ina support HDMI na kingamuzi cha azam kina HDMI. Nikinunua waya wa HDMI channel zitaonekana vizuri zaidi au inakuwaje??

Kiasi, ila si sana. Mimi natumia HDMI cable, ila sioni tofauti sana na mtu anayetumia component cables...na nadhani sababu channels zao nyingi ni SD, na si HD. Za HD utaziona vizuri zaidi, ila SD zitakuwa kawaida tu
 
Mkuu sijakuelewa umemaanisha nini?? Samahani ni mgeni katika uzi nimeshawishika katika kununua kingamuzi cha Azam so nilikuwa naangalia maoni ya watu yakoje??

Maana ya FTA mkuu?? Naona hapa mnaelewana wenye kufahamu haya mambo. Samahani kwa usumbufu.

mbali na watoto nilimaanisha kuwa gharama zake zinazidi kupanda kila kukicha ndio maana binafsi naiogopa na kuamua kutumia fta.(free to air)
 
Swali Jengine. Tv yangu ina support HDMI na kingamuzi cha azam kina HDMI. Nikinunua waya wa HDMI channel zitaonekana vizuri zaidi au inakuwaje??

Tofauti ipo mkuu kwenye kwaliti ya picha..kwenye waya wa kawaida picha inakuwa kama imepauka kidogo ukilinganisha na kama unatumia hdmi..
 
Wadau nimeona azamtv wamepost kuwa wataonyesha la liga, mwenye idea anisaidie, wataonyesha mechi zote? Na je kwa kupitia channel gani?
 
Back
Top Bottom