Azamtv kwa maoni yangu ndio runinga bora kwa zile runinga za akina mimi,kutokana na hali ya maisha ilibidi niache DSTv (baba yao) na pia Zuku nimewaacha na nimejiunga na Azam tv na sija regret hata kidogo,nafikiri ndio TV stesheni pekee ambayo utapata channels nyingi kutoka Kenya,Uganda na Zambia,pia kwa wale wanaopenda kuchkuch (I am a disco dancer) zipo station nyingi tu pia za uarabuni ndio usiseme.Kasoro niliyoiona na ambayo sina uwezo nayo ni station za kimataifa zinazotumia Kiingereza kuwa 2 tu yaani BBc na Al-Jazeera kwa hiyo kwa tuliozoea makala,habari za kimataifa inakuwa shida ,pia channel ya Nature haipo,kwa wale wapenda wanyama.
Kuhusu EPL wanatumia WBS ya uganda ambao huonyesha EPL siku ya Jumamosi tu tena ni mechi moja tuna mwisho katuni kwa watoto chanel zipo mbili tu moja ya kiarabu na mojaya kiingereza,lakini kwa kifupi kwa kulipia 12500 kwa mwezi Azam wameturahishia gharama,bado sijafikisha mwezi toka nijiunge kwa sijajua FTA kama wanaonyesha hata kama salio limeisha ingawa wameandika kuwa wanaonyesha.