Elimu ya biashara kwa vijana wanaotaka kuanza

Joh97

New Member
Sep 6, 2022
2
0
Vijana tulio wengi mara nyingi tunakwama sana kwenye biashara kutokana na kupeana mawazo ya maandishi na siyo ya mazoezi unakuta vijana wengi tunakuwa na mitaji ambayo kweli tuki isimamia vyema ni rahisi kufanikiwa ila tunashindwa namna ya kufanya bishara kinachotufelisha mara nyingi ni kuchukua mawazo ya darasani na kuyafwatisha asilimia zote kwenye kufanya biashara nataka nikupe mfano ambao unaweza kukupa maarifa ya namna ya kufanya biashara.

Mimi nilikuwa na milioni tano za kitanzania mwaka 2019 nikapewa mawazo ya kuwa endapo nikiwekeza kwenye biashara ya pikipiki ni rahisi kufanikiwa, nilipewa bei ya pikipiki na faida kiujumla kweli ilinishawishi sana kufanya lakini mimi nilitumia mbinu nyingine pasipo kutumia pesa yangu

Nilitafuta pikipiki ya mkataba nikaanza kupambana kwa miezi 12 ambayo kwa siku ni Tsh 12,000. Nilifanya kazi kwa miezi sita nikazoea mazingira na changamoto zake nikazijua nikasema sasa naweza kununua pikipiki moja kwanza huku na mimi nikiendelea kufanya kazi baada ya mwaka

Nikamiliki pikipiki 2 ambayo moja nilimpa mtu afanye kazi aniletee hesabu baada ya hapo nikawa na pikipiki mbili na akiba yangu ya bank ya shilingi milioni 2 na laki tano. Mwaka mwingine nilifanya kazi kwa miezi 6 nikatengeneza 1,800,000 huku pikipiki niliyompa mtu ikinitengenezea sh 4,320,000 ambayo jumla ni sh 6,120,000 ukijumlisha na 2,500,000 jumla nilipata 8,620,000 nikanunua pikipiki 2 ukiachana na niliyompa mtu mkataba nikawa na pikipiki 3 mpya 2 na ya zamani 1

Nilipambana mwaka ulivyoisha pikipiki zile 2 zikaniingizia 8,640,000 ukiachana na akiba yangu ya bank ambayo ilibaki 3,440,000 ambayo jumla kuu ni 12,080,000 mtaji wangu ulipaa kila mwaka mpaka kufikia milioni 18,00,0000

USHAURI
Unapotaka kufanya biashara fulani kwanza hakikisha umepata uzoefu wa Kutosha kabla ya kuweka pesa zako hata kwenye kilimo cha jitahidi kulima kwanza angalau kwa mwaka ukishapata uzoefu wa kutosha ambao unaweza kukusaidia kutatua changamoto za kilimo chako cha biashara na utafanikiwa kirahisi. stori za mtaani zinaweza kukusababisha ukafeli vibaya mno pata uzoefu mzuri usikimbilie mafanikio ya mara moja

John Andrew
 
Vijana tulio wengi mara nyingi tunakwama sana kwenye biashara kutokana na kupeana mawazo ya maandishi na siyo ya mazoezi unakuta vijana wengi tunakuwa na mitaji ambayo kweli tuki isimamia vyema ni rahisi kufanikiwa ila tunashindwa

John Andrew
Vijana wengi wanafeli kwenye kufanya kitu wasichokijua vinzuri
 
Umenena vyema kuhusu uzoefu il hapo Kwenye pkpk mbili kkpa milion nane kwa mwaka HAPANAAAAAA
 
Back
Top Bottom