Elimu imekusaidiaje?

Nani kakwambia m2 mwenye elimu ya darasa la saba hana fani yoyote???... Ndo maana ikaitwa msingi Bila huo msingi mwenye PhD asingepata hiyo PhD yake .. Matajiri wengi hapa bongo wana Elimu ya darasa la 7... Kwahyo ukisema mtu wa darasa la saba hana fani unajidanganya
 
Ni kwel pasipo shaka weng wa Graduates wa Tanzania wapo bench
Hapo ndo uhitaji na umuhimu wa mtaala unaoendana na mazingira halisi ya Tanzania unapoonekana

Kazi kubwa inahitajika kufanyika kubadilisha mindset ya walioko mashuleni na wahitimu kuwa shule zipo Kwa ajili ya maarifa na ujuzi na si vinginevo.


Asa mnaosema Elimu sio kuajiriwa mbona mmewaacha wasomi wengine Kwenye benchi ?? Unamfundisha mtu course chuo Ili aje Kukaa kwenye benchi? Something is wrong somewhere.... embu tufikirie deep...
 
Nimekuelewa sana kiranga
 
Ni elimu ya mhimu sana kwa kila Mtanzania kuipata

 
Umeeleweka.

Kwenye utamaduni wa kukariri na kulazimisha kukubaliana hapo kuna tabu sana.

One more story and then I am done for the day.

Nilipoanza chuo mwaka wa kwanza nilikuwa na kozi moja ya falsafa, elective.

Professor mzungu conservative anatoka upstate New York. Supporter wa George Bush. Republican. Judge. Mimi liberal, immigrant fresh off the plane from Bongo.

Darasa la introductory level philosophy, Western Philosophy, mainly pre-Socratic philosophy.

Basi nikataka kulianzisha siku ya kwanza kwa nini hawajaweka falsafa za sehemu nyingine. Lakini nikajirudi. Ukiwa mbishi kanuni ya kwanza ni kuusoma mchezo kabla ya kubisha.

Basi kutoka hapo, nikawa nabishana sana na Professor. Kila darasa ni ubishi. Halafu ubishi wa logic, arguments zangu Professor anazifahamu. Sibishi vitu ambavyo sijavisoma. Nabisha kwa kutumia hoja za wasomibwa falsafa ambazo hata Professor anazijua. Kwa hiyo nikibisha kwa point hii, Professor anajua hapo Locke, hapo John Stuart Mill, hapo Nietzche, hapo Aquinas, etc. Kuna wakati nikawa na dominate darasa mpaka nikaona imepita kiasi. Hususan topic za uwepo wa Mungu. Mpaka dada mmoja akaniuliza, vile unavyobisha unaamini kabisa au unafanya uzushi tu? Nikamwambia naamini hivyo.

Nikasema huyu Profesa atakuja kunifelisha. Kwa sababu nabishana naye sana, mtu mwingine anaweza kuona namvunjia heshima.

To cut a long story short, mwisho wa semester, professor aliniandikia email anasema usije kwenye mtihani wa mwisho wa semester. Nikaona tayari, Professor kashanifelisha kwa sababu ya ubishi wangu darasani. Nikamuuliza imekuwaje tena? Akaniambua hili darasa umeshapasi, umelionea sana. Zile arguments zako za darasani ni za graduate school level. Ni arguments za darasa la masters la falsafa. Hili darasa hata hukutakiwa kuwemo umelionea sana. Nakupa A+. Usije kwenye mtihani.

Nikasema mfumo wa elimu wa Marekani ni tofauti sana na Tanzania.

Nina hakika kama ingekuwa vyuo vyetu Profesa angenifelisha kwa kukosa nidhamu.

Wakati wenzetu Profesa anakubishia anaangalia umesoma na unaelewa nini. Akikuona unaweza kutetea arguments zako anakupitisha.

Kwa kweli yule Profesa alinitafuta sana urafiki akawa anataka niwe naenda kwenye mikutano yao ku network. Ila na mimi nikawa nina kazi zangu nyingi nikawa sina muda naye.

Kama unataka habari za kugezeana wote mseme sawa sehemu kama hiyo, hata kama una kipaji chako kiko tofauti, hakiwezi kuonekana.
 
Mangi lemule;
Hujanikosea hadi uniombe msamaha mkuu
Kiukweli kabisa kwa kozi niliyosoma mm haijwahi kuniingizia hata laki. Nimejikita zaidi kutumia ujuzi mwingine kabisa ambao nimezaliwa nao na kusoma soma vitabu tu.

OK, Mkuu

Lakini ukifanyacho kwa sasa, darasa ulilokwenda miaka 16 au na zaid ya hapo, alijafanya chochote ?
 
Mkuu hongera lakini kuna kitu nakiona cha ziada hapo. Kuna utafauti wa mazingira ya jinsi anavyoipata elimu.
Funguka zaidi.

At a basic kevel mtoto anayekua huku anaangalia bookshelf la baba yake lina kila kitu kuanzia magazeti ya Times na Newswek, vitabu vya Charkes Dickens mpaka michoro ya architecture ya nyumba, na akawa na utashi wa kusema hapa kama sintoweza kuielewa hii michoro ya nyumba basi hata hivi vitabu vya Dickens na haya magazeti ya Newsweek na Times nisishindwe kusoma, si sawa na mtoto ambaue kwao hata umeme hamna.

Ndiyo maana nakataa simplification ya "hawa wameshindwa mitihani ni vilaza".

Inawezekana wanahitaji miwani, halafu hawajui hata kwamba wanahitaji miwani, kwa sababu kijijini kwao miwani ni anasa ya juu sana ambayo hawawezi hata kuifikiria.
 
Binafsi elimu rasmi imenisaidia zaidi ya asilimia 90.

<Ushauri>
Watanzania Tujenge utamaduni wa kujisomea vitabu.
 
Elimu yangu imenisaidia kumjua MUNGU MUUMBA wa mbingu na dunia na viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Elimu imenisaidia pia kupambana na hali tofauti za maisha ikiwa ni pamoja ni kujipatia mkate wangu wa kila siku na kuishi na jamii inayonizunguka kwa amani.

Zaidi ya yote hayo ninalolifurahia zaidi kuhusu elimu yangu ni kunisaidia kujua BWANA MUNGU anataka nini kutoka kwangu nikiwa kama binadamu kwenye hii dunia aliyoiumba kwa mikono yake na uwezo wake usiopimika kwa jinsi ya kibinadamu.

So kwangu mimi elimu imenisaidia kwa 99%

Cc. Kiranga
 

Ni kweli mkuu ..

.hili jambo ni la kuliangalia pia...

mie nahisi wanafundishwa vitu general

na sio specific

mfano madaraja yetu mvua ikinyesha yanavunjika,

sababu wamefundishwa kujenga daraja

but not specific kulingana na mazingira yetu …

pia Kama wangefundishwa kilingana na mazingira yetu wangekua na knowledge ya kuexplore opportunities zilizopo hivyo kujiajiri...
 
Mfumo wa Tanzania unalazimishana kukarir

Nakumbuka kipindi nasoma lecturer kwa ujasir kabisa, pasipo kupepesa macho ananena kuwa "Ukidefine Econometric tofaut na Gerhard Tintner
utakuwa umejibu swali lako ulilojitungia"
Hi ikanifanya nmeze kama ilivo tu ili nifaulu paper lakin nijua ni ujuha sana wa kiwango cha lami

Kukarir kuna muondolea mtu critical thinking, kunamfanya mtu aone elimu ngumu sana

Tanzania Tanzania Tanzania yetu.


 
Haswa elimu inatakiwa iendane na mazingira ya msomaji, na imuwezeshe kuyakabili hayo mazingira kikamilifu katika kujipatia mahitaji yake mhimu ya kibidamu kila siku


 
Hivi ndivyo ninavyomaanisha. Wazazi wananafasi kubwa ktk kumfanya mtoto awe na mafanikio ya kielimu( Ku "ekseli"). Hii ilijenga dhana kuwa mtoto was mwalimu lazima afaulu tena huku kwetu uswazi walikuwa wanasema kapasishwa. Kumbe mzazi kuelimika kunatengeneza mazingira ya mtoto kuelimika zaidi.
Mf: Familia ya prof Kabudi, baba prof mama PhD holder hapo kuna mazingira mazuri kwa mtoto kusoma na kuelimika.
Sasa sisi huku wa katani ni tabu tupu kwakweli
 
Kwa uelewa wako huu sidhani kama ulipata shida kwa mitaala yetu hapa bongo.....

Na kama ulisoma arts na uhakika ulifanya vizuri mno.....

Nikupe tu Hongera yako wewe jamaa unajiamini kinouma halafu kama unakifahamu kitu bhasi unakielezea vizuri tena chote bila kuacha kitu hata bongo lala yoyote ataelewa na hakutokuwa na maswali kabisa.....

Na imani ungezaliwa kwa wazungu huko sasa hivi tungekuwa tunakusoma kwa articles mbalimbali za uvumbuzi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…