Elimu imekusaidiaje?

Mkuu Kiranga moja ya vitu ambavyo napenda sana kutoka kwako ni namna ya unavyoweza kuelezea jambo in deep. Hapo kwenyewe umenipa mambo mengi sana nikajikuta nawish uendelee.
Haaa, mkuu, kuna watu wengine ukiendelea sana wanakuona show off na wao nawapa nafasi nisiwakwaze.

Hahaa.

Mimi hii kitu ipo kwenye damu, hata mshua wangu ni mtu wa "personal stories and testifying anecdotes".

Halafu nishapata vindication kwa bosi wangu mmoja, nilikuwa nafanya global project moja, basi yeye kila siku ananiambia anapenda sana ninavyoandika, ananiambia "paint a picture, tell a story".

Yani kuelezea vitu bila hata anecdotal stories naona kama sijakamilisha mambo vile.
 
Hahahahahaha... Mtu wa fact sana wewe. Tena kizuri zaidi mambo mengi huwa unauelewa nayo.

Mfano mzuri sana wakuigwa wengi tunadhani Elimu ni kile tulichosomea pekee na hapa ndiyo shida inapoanzia.
 
sasa wakuu kama umesoma na hufanyii kazi ulichosomea,wewe una utofauti gani na mtu wa la saba ambae hana fani yeyote…?
Mimi niliyesomea Uhandisi alafu nikaamua kuuza Samaki nitafanya kitaalam zaidi kuliko yule ambae kaishia la 7.
Elimu imenisaidia kujua mambo mengi yanayotendeka Duniani, kufanya kazi zangu in proffesional na kutatua changamoto zinazonikabili kisomi na sio kwa kukurupuka
 
unavitu vingi sana vya kutufundisha nakushauri usiwe mchowe make a thread everyday una madini mtu wangu
 
unavitu vingi sana vya kutufundisha nakushauri usiwe mchowe make a thread everyday una madini mtu wangu
Haina noma, nipo sana hapa najitahidi angalau kila siku niwe natoa uzoefu tunabadilishana mawazo.

Nimegundua kwamba kuna vitu fulani mtu unaweza kuona vya kawaida sana kwako, halafu mimi vikanipa changamoto na hamasa sana, na mimi pia naweza kuona vitu fulani kawaida sana, lakini wewe vikakupa changamoto na hamasa.

Kwa hiyo kama hatubadilishani mawazo, hatuwezi kujua mengi kuhusu changamoto na hamasa hizi.

Moja ya uzuri wa thread kama hii ni pale tunapoweza kuona kukosa matumaini, watu wanahoji kitu kama umuhimu wa elimu, kwa haki kabisa katika muktadha wa dunia ya leo ambayo haina guarantee kwamba elimu itatoa ajira nzuri mtu aliyosomea, halafu wakaja watu wengine na michango mbalimbali ikaonesha kwamba, umuhimu wa elimu unaenda mbali zaidi ya kurahisisha ajira tu, unabadilisha mfumo mzima wa maisha ya mtu.
 
Elimu ni nyenzo ya fikra. Muda mwingine athari zake katika jamii hazijidhihirishi katika umbo ambalo kila mtu anaona.
 
Elimu ni nyenzo ya fikra. Muda mwingine athari zake katika jamii hazijidhihirishi katika umbo ambalo kila mtu anaona.


Exactly wengi wanapima uthamani wa elimu kwa kupata kazi nzuri,

They're totally wrong
 
Mkuu upo vyema sana katika nyanja mbalimbali .Hongera sana kwa hilo Mkuu

 

Asante Sana kaka mkubwa... naona umefunguka haswaa ..ni vizuri mkuu kutuelimisha wengine ....Hilo la confidence nimekupata sawia..kufanya presentation Becky ujanja wote kwishney LOL....Ila nimegundua sio peke yangu LOL....

.... nimegundua nchi nyingine mfumo Wao wa elimu unawa encourages watoto kujisomea , kuongea mbele ya darasa wakiwa wadogo, hivyo ni skills anakua nayo...by the time Yuko Chuo ni mtu anajiamini ....Leo wameweka presentation kwa course nyingi za chuo ,watu wanastruggle sababu ni vitu vigeni kwao! Wangekua wanafundisha kuanzia secondary....ingewajengea watu confidence taratibu

tuna culture ya kukariri pia, Enzi zile unakuta essay darasa zima limeandika vitu hivyo hivyo LOL na mwalimu anatick siku zinakwenda...... inabidi huo mfumo huu wa elimu ...ubadilike watu wademonstrate ujuzi wao na kuleta vitu vipya Dunia hii....

Binafsi,siamini umfundishe vitu complex mtu kwa miaka mitatu tu atoke hapo amepikika unless Huyo mtu seriously asome vitabu .... Jambo ambalo hata mtu wa darasa la Saba anaweza kufanya hivyo,,,,

Nimeona mahali pia,watu kwa kuwa wamesoma vitabu kuanzia utotoni, by the time amemaliza form six ana knowledge kubwa kushinda mtu aliyeenda chuo....

Sijui km nimeeleweka lol
 
....

Nimeona mahali pia,watu kwa kuwa wamesoma vitabu kuanzia watoto by the time amemaliza form six ana knowledge kubwa kushinda mtu aliyeenda chuo....

Sijui km nimeeleweka lol
Hapana.

Nahitaji subtitles ili nikuelewe vizuri.

Nisameheni jamani
 
Elimu yangu imenisaidia kujua Dunia inakwendaje tu lakini kiuchumi ina mchango wa 0%
 
Asa mnaosema Elimu sio kuajiriwa mbona mmewaacha wasomi wengine Kwenye benchi ?? Unamfundisha mtu course chuo Ili aje Kukaa kwenye benchi? Something is wrong somewhere.... embu tufikirie deep...
 
We mzee Mtata sana
 
Elimu yangu imenisaidia kujua Dunia inakwendaje tu lakini kiuchumi ina mchango wa 0%


Japo sikujui wala sikufahamu lakini kwa hilo ulisemalo sina imani nalo sana

Mkuu kuna sehemu elimu yako imekusaidia tu tofaut na hapo , hata kuweza kuja JF na kusoma jinsi ya kulima nyanya ni zao la darasa ulilokwenda

Kwahyo wataka kusema hakuna lolote elimi yako imekufanyia zaid ya kufahamu dunia inakwendaje ?

Kama ntakuwa nimekwenda mbali sana unisamehe Mkuu
 
Mkuu hongera lakini kuna kitu nakiona cha ziada hapo. Kuna utafauti wa mazingira ya jinsi anavyoipata elimu.
 
Point sana Mkuu Rebeca 83 , Watu wengi wanababika sana wanapohitajika kuzungumza mbele za watu,
Naamin ni mfumo wetu wa elimu haumjengei mwanafunzi uwezo wa kukabiliana na mazingira ya mbele za watu wengi katika muktadha wa kuzungumza kwa ujasiri


wa
 
Mangi lemule;
Hujanikosea hadi uniombe msamaha mkuu
Kiukweli kabisa kwa kozi niliyosoma mm haijwahi kuniingizia hata laki. Nimejikita zaidi kutumia ujuzi mwingine kabisa ambao nimezaliwa nao na kusoma soma vitabu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…