Elimu High School Bure; Je, tunawapa watu mashuka wakati wa joto na kuwanyima wakati wa Baridi?

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,496
19,533
Nimeona wamesema Elimu High school itakuwa bure, ni vema na Haki, Lakini hii kuwasaidia watu elfu 70 ambazo wazazi wanaweza kujichanga na kuomba omba wakapata na kule ambapo wanadaiwa mamilioni ya Pesa na kukosa hata mikopo (Kwenye Vyuo) Hawapewi kweli kuna tija?

Kwa kila mzazi kutoa elfu sabini sabini mzigo sio mkubwa individually kuliko kwenye fungu tunalochangia wote ili lifanye mengine, tunatoa hizo sabini mara maelfu ya wanafunzi ambao kutokana na kubana mikanda huenda wasipate elimu bora bali bora elimu.

Je, hatuoni ingekuwa bora either tuongeze uzalishaji pote pawe bure au tuboreshe kule juu ili kila kiumbe apate mkopo wa kuweza kupata huu ufunguo wa maisha.

Na kuondoa elfu sabini wakati watu wanachangishwa michango mingi nadhani its just a political statement ila uhalisia ni kuendelea kududumiza elimu yetu (Yaani sio kwamba tunawapa shuka wakati wa Joto bali hilo shuka lina Chawa hence tunawapa miwasho).
 
Kwenye shule za serikali na vyuo vikuu vya umma elimu inatakiwa kuwa bure, hii mambo ya loan board ni uhuni wa kunyanyasa watoto wa wanyonge kuweza kuendeleza vipaji vyao vya kielimu. Imagine huyu mtoto wa mnyonge kaanza kazi na mshahara kiduchu, hapo hapo ufyeke zaidi ya laki moja eti kulipia deni la loan board.​
 
Nimeona wamesema Elimu High school itakuwa bure..., Ni Vema na Haki....

I agree with you Mkuu, watu wakipata kazi nzuri juu..wakalipa Tax nzuri mambo yatakuwa sawa. Kutolipa kodi advance halafu kumuachia mzigo mtoto deni wakati wa kuingia chuo ni kumpa chakula na kumuacha afe njaa.

Either labda wasilipe ada Advance ila wakimaliza Advance kwa wale ambao wataona hawataweza ku afford kulipa deni/mkopo baada ya kupata kazi, wajengewe scheme ya kuwapa skills zitakazowafanya waingie kwenye ajira.

Itaongeza uzalishaji.
 
Kama Taifa tuna shida ya Kufikiria!

Tunapenda kutatua Matatizo yasokuwepo!

Ndo mana sishangai kuskia kuna Kiongozi kawejengea wananchi wake Mortuary, kule morogoro kuna Mbunge anasifiwa kwa kutoa Basi la kwenda Kuzikia as if kabla ya basi lile watu walikuwa hawazikwi. Naskia kuna mafao ya Mazishi. Na sasa unaondoa elfu ada 70, unaenda kumpa mkopo 20% univ... ataitoa wapi 80% uliemfutia ada ya elfu 70! Shabash
 
Kwenye shule za serikali na vyuo vikuu vya umma elimu inatakiwa kuwa bure,​
Yap inatakiwa ila uhalisia upoje? Duniani hakuna kitu cha bure hata wewe ukikipata bure kuna mwingine anakilipia.., sasa hizo shule inabidi zipewe ruzuku ambazo ni kodi zetu, (Je, hizo pesa zinafika / zitafika kwa wakati au ndio kuchelewa na watu kupata vitu sub-standard?

Ukweli ni kwamba hii cake ya taifa inayoliwa na wachache haitoshi kwahio inabidi tuendelee kukamuana ili kufidia hizo sabini sabini (ambazo hazina msaada sana) afadhali tungekamuana kusaidia kule kwenye mamilioni kwanza kabla ya huku kwenye elfu 70
hii mambo ya loan board ni uhuni wa kunyanyasa watoto wa wanyonge kuweza kuendeleza vipaji vyao vya kielimu. Imagine huyu mtoto wa mnyonge kaanza kazi na mshahara kiduchu, hapo hapo ufyeke zaidi ya laki moja eti kulipia deni la loan board.​
Bora huyo anayeanza kazi kuliko ambaye hata hio kazi haipo na alikosa huu mkopo na mzazi wake aliuza shamba ili aweze kupata huu ufunguo wa maisha ambao umegeuka kuwa ufunguo wa madeni.
 
Tunakoelekea mikopo ya elimu ya juu itafanywa 100% kwa wanafunzi wote. Mama anaupiga mwingi
Kwenye pesa atakayoitoa kwenye pochi yake?!!! Au Corona nyingine itakuja tupewe pesa? Au IMF

Sio kwamba inashindikana ingewezekana kama tungeacha kufuja pesa na kuondokana na matumizi mabovu ila sioni any time soon mawaziri na wengine wala keki kuanza kufunga mikanda, unadhani watapaki V8 zao ili wewe usome bure? (Ofcourse utasoma bure ila itakuwa ni kusoma jina tu, lakini hakuna quality)
 
Yap inatakiwa ila uhalisia upoje ? Duniani hakuna kitu cha bure hata wewe ukikipata bure kuna mwingine anakilipia.., sasa hizo shule inabidi zipewe ruzuku ambazo ni kodi zetu..., (Je hizo pesa zinafika / zitafika kwa wakati au ndio kuchelewa na watu kupata vitu sub-standard ?

Ukweli ni kwamba hii cake ya taifa inayoliwa na wachache haitoshi kwahio inabidi tuendelee kukamuana ili kufidia hizo sabini sabini (ambazo hazina msaada sana) afadhali tungekamuana kusaidia kule kwenye mamilioni kwanza kabla ya huku kwenye elfu 70

Bora huyo anayeanza kazi kuliko ambaye hata hio kazi haipo na alikosa huu mkopo na mzazi wake aliuza shamba ili aweze kupata huu ufunguo wa maisha ambao umegeuka kuwa ufunguo wa madeni
Jaribu kuelewa, serikali ina wajibu wa kusomesha raia wake, ndo maana nakwambia kwenye shule za serikali na vyuo vikuu vya umma elimu inatakiwa kuwa bure kwani itaendeshwa kwa kodi za wananchi. Nchi kama Norway elimu hadi ngazi ya vyuo vikuu ni bure kabisa kwa kuwa wanatambua jukumu la serikali kuelimisha watu wao.
 
Wajibu na reality / kinachofanyika ni vitu viwili tofauti...., kama mtu anatembea kwenye miba Je ni bora kuanza kumpa soksi kwa kutumia pesa yake ya mboga..., au kumpa ndala ili asichomwe miba wakati unaongeza pesa ya kununua soksi na yeye anendelee kula mboga yake ?
 
Hujui kwani uvhaguch hauko mbali mkuu?

Hizi ni political blander
Yaap Political Mileage..., nadhani ili twende vizuri kwa viongozi wa serikali tungeongeza kodi maradufu kwa wale wote wanaowapeleka watoto wao shule za nje, nadhani nao wakiwa wanapata huu upupu huku huenda wakaboresha
 
Nimeona wamesema Elimu High school itakuwa bure, Ni Vema na Haki, Lakini hii kuwasaidia watu elfu 70 ambazo wazazi wanaweza kujichanga na kuomba omba wakapata na kule ambapo wanadaiwa mamilioni ya Pesa na kukosa hata mikopo (Kwenye Vyuo) Hawapewi kweli kuna tija?

Kwa kila mzazi kutoa elfu sabini sabini mzigo sio mkubwa individually kuliko kwenye fungu tunalochangia wote ili lifanye mengine, tunatoa hizo sabini mara maelfu ya wanafunzi ambao kutokana na kubana mikanda huenda wasipate elimu bora bali bora elimu.

Je, hatuoni ingekuwa bora either tuongeze uzalishaji pote pawe bure au tuboreshe kule juu ili kila kiumbe apate mkopo wa kuweza kupata huu ufunguo wa maisha.

Na kuondoa elfu sabini wakati watu wanachangishwa michango mingi nadhani its just a political statement ila uhalisia ni kuendelea kududumiza elimu yetu (Yaani sio kwamba tunawapa shuka wakati wa Joto bali hilo shuka lina Chawa hence tunawapa miwasho).
Ni kiini macho mkuu
 
Yaap Political Mileage..., nadhani ili twende vizuri kwa viongozi wa serikali tungeongeza kodi maradufu kwa wale wote wanaowapeleka watoto wao shule za nje, nadhani nao wakiwa wanapata huu upupu huku huenda wakaboresha
Hapa wanatafuta starter ya kuingia nayo kwenye kampeni kwamba"watoto wenu tumewafutia ada ya kidato cha tano na sita" na wazazi wetu watawapa kura tu .

Matatizo yako mengi makubwa kuliko hili la 70 elfu lakini kama hawaoni tukianza na hili la mfumuko wa bidhaa ambazo zingine zinazalishwa hapa hapa nchini kwetu..!

Hawaoni kabisa,haya mwaka jana wanafunzi wengi wamekosa mikopo ya elimu ya juu sijui sababu ni nini?
 
Mimi nadhani hii elimu ya high school Hawa waliongia mwaka huu ndo mwisho wa kuchaguliwa high school iwapo mapendekezo ya wadau wa elimu kwenye wizara ya elimu yatapita, wengi wamependekeza elimu ya school iwe mwisho form four alafu wanafunzi wote wachaguliwe shule za ufundi kama inavyofanyika kwa walimu na vyuo vya kati, sasa hizi high school zitageuka vyuo vya kati au ufundi hapo naona serikali imeanza kujiandaa na mpango wake wa kuwakopesha vyuo vya kati iwapo hiyo high school haitakuwepo na waliahidi utekelezaji kuanza mwaka ujao 2023.
 
Nimeona wamesema Elimu High school itakuwa bure, ni vema na Haki, Lakini hii kuwasaidia watu elfu 70 ambazo wazazi wanaweza kujichanga na kuomba omba wakapata na kule ambapo wanadaiwa mamilioni ya Pesa na kukosa hata mikopo (Kwenye Vyuo) Hawapewi kweli kuna tija?

Kwa kila mzazi kutoa elfu sabini sabini mzigo sio mkubwa individually kuliko kwenye fungu tunalochangia wote ili lifanye mengine, tunatoa hizo sabini mara maelfu ya wanafunzi ambao kutokana na kubana mikanda huenda wasipate elimu bora bali bora elimu.

Je, hatuoni ingekuwa bora either tuongeze uzalishaji pote pawe bure au tuboreshe kule juu ili kila kiumbe apate mkopo wa kuweza kupata huu ufunguo wa maisha.

Na kuondoa elfu sabini wakati watu wanachangishwa michango mingi nadhani its just a political statement ila uhalisia ni kuendelea kududumiza elimu yetu (Yaani sio kwamba tunawapa shuka wakati wa Joto bali hilo shuka lina Chawa hence tunawapa miwasho).

Wametoa wlf70 ila gharama mpaka aende hiyo shule alipangiwa ni laki 6 mpaka 7
 
Wametoa wlf70 ila gharama mpaka aende hiyo shule alipangiwa ni laki 6 mpaka 7
Naam ila wamepata pa kuongea come uchaguzi na wala hatuhoji kuhusu mapungufu mengine ya hii Bajeti wala madudu yanayoendelea...

Politics 101
 
Back
Top Bottom