Elimu bure ni usanii mtupu

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,552
1,512
Ndugu wana jamvi,

Nimeshangaa sana badala ya kuona kiasi cha fedha ambacho moja ya shule ya msingi iliyoko mkoa wa Pwani imepewa kwa ajili ya elimu bure.Shule hii ina wanafunzi 1120 na imepewa 447000tsh. Hii ni kwamba kila mwanafunzi amepewa shilingi 399.

Najaribu kuangalia mahitaji ya shule ikiwemo kulipa walinzi, kununua chalk, kununua karatasi pamoja na vifaa vingine muhimu shuleni naona kuwa fedha hizi hazitoshi hata kidogo. Hazitoshi kuendesha shule hata kwa week mbili.

Naiona elimu ya Tanzania ikididimia na ubora ukishuka zaidi.

Duc in Altum
 
Ndugu wana jamvi,
Nimeshangaa sana badala ya kuona kiasi cha fedha ambacho moja ya shule ya msingi iliyoko mkoa wa pwani imepewa kwa ajili ya elimu bure. Shule hii ina wanafunzi 1120 na imepewa 447000tsh. Hii ni kwamba kila mwanafunzi amepewa shilingi 399. Najaribu kuangalia mahitaji ya shule ikiwemo kulipa walinzi, kununua chalk, kununua karatasi pamoja na vifaa vingine muhimu shuleni naona kuwa fedha hizi hazitoshi hata kidogo. Hazitoshi kuendesha shule hata kwa week mbili. Naiona elimu ya Tanzania ikididimia na ubora ukishuka zaidi.

Duc in Altum
Wabongoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
HII si kweli nilimsikia MAGUFULI mm mwenyewe akisema pesa wamepelekewa kila shule zaid ya 1b kwa 3months

akatoa na onyo "ole wake yeye ataetumia vibaya"
 
HII si kweli nilimsikia MAGUFULI mm mwenyewe akisema pesa wamepelekewa kila shule zaid ya 1b kwa 3months

akatoa na onyo "ole wake yeye ataetumia vibaya"
Zimepelekwa bilion 15.7 kwa shule zote Tanzania za seconday na msingi so huo ndio mgao shule hii imepewa. Zipo shule zimepata chini ya laki mbili. Na ikumbukwe fedha hizo sio siri maana wamesema document zibandikwe kwenye mbao za matangazo.

Duc in Altum
 
Nchi ya Ajabu sana, kwenye mambo serious tunaweka siasa... Hivi tunatengeneza kizazi gani???? Tutaendelea kuyumbisha elimu yetu mpaka Lini??
 
Elimu bure haiwezi kuwa bora. Tujiongeze

kuna vitu kama pesa ya mlinzi, kulipia maji, pia kuna ile wanapewa walimu kufundisha baada ya mda wa kawaida, sidhani kama walimu
watakubali kufundisha bure huo mda wa ziada...

pia kuna ishu ya uniform, michango ilikuwa inakusanywa alafu wanashonea shuleni (najua walimu nao walikuwa wanapiga) ila faida
yake ni kuwa nguo zote zinashonwa kwa mtindo mmoja... sipati picha kwa hiki kizazi chetu kila mwanafunzi akashone sare mwenyewe

hali inaweza ikawa mbaya zaidi
 
Kwani rais alisema hapo ndiyo mwisho hawapewi zingine , Alisha sema kila mwezi shule zitakuwa zinapewa fedha
 
Kwani rais alisema hapo ndiyo mwisho hawapewi zingine , Alisha sema kila mwezi shule zitakuwa zinapewa fedha
Ninachesema ni kuwa fedha izo hazitosh hata kwa week mmbili najua ni za mwez

Duc in Altum
 
Mtoa mada amekurupuka, hiyo hela ni kila mwezi
Najua ni kila mwezi ninachosema ni kuwa fedha hizo hazitosh kwa mwez huo mmoja. Mwanafunz mmoja ni kama anapewa 399tsh kwa mwezi how can this be posible?

Duc in Altum
 
HII si kweli nilimsikia MAGUFULI mm mwenyewe akisema pesa wamepelekewa kila shule zaid ya 1b kwa 3months

akatoa na onyo "ole wake yeye ataetumia vibaya"
Mkuu sidhani kama hesabu zako ziko sahihi, kila shule I billion for 3 months kwa nchi nzima ni pesa nyingi sasa uwezo wetu hauruhusu
 
Mmi najua hayo hayawezekani. Ila inatakiwa wakumbuke elimu bure haiwezekani ila wajiandae tu.
 
HII si kweli nilimsikia MAGUFULI mm mwenyewe akisema pesa wamepelekewa kila shule zaid ya 1b kwa 3months

akatoa na onyo "ole wake yeye ataetumia vibaya"
Gazeti la mwananchi wameripoti Leo kuwa shule za sekondari iliyopata hela nyingi imepata 5m kihonda sec na iliyopata hela kidogo imepata 580k ambayo ni Bungodimwe
 
Back
Top Bottom